Matokeo ya CO mwaka wa pili yashikiliwa NACTE Tanzania nzima

Matokeo ya CO mwaka wa pili yashikiliwa NACTE Tanzania nzima

Kwaiyo tunamwita Kwa neno moja maana tunajua majukumu yake hebu tufafanulie usiishie kudefine tu pengine unajua zaidi!!???

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo mengi sana CO anayasoma akiyazingatia haswaa na akajiongeza na akawa anawaza nje ya box na kujiuloza kwa nini hiki kinakuwa hivi na kisiwe vile,akiwa na akili hii basi anakuwa yuko njema saaana katika utabibu wake na wagonjwa watampenda sana na kuelekezana waende kwake pale wanapoumwa.

Haya mambo tunayashuhudia sana

Ipo wazi hio......
 
Sisi wenyewe tulivya ya tume ya ajira tra ikafuja sas tumeambiwa turudie tena
 
Lakini tukubaliane kwamba hawa watu wanatofautina sana kimaarifa na mazoezi. Tunaweza tukawa tunatibu ugonjwa sawa lakini tukatumia mbinu tofauti kulingana na hali ya mgonjwa na dawa zilizopo hospitali.
Kinachpwafanya watu waone Co NI sawa na daktari ni kwa sababu ya lengo lao na sio njia wanazotumia kufikia lengo hilo.

Na lengo lenyewe ni kutibu mgonjwa.
Unadhani kama dhima ilikuwa ni kutibu tu na hakuna tofauti, basi CO asingekuwa ana uwezo wa kwenda specialization yeyote pasipo hata kupitia MD, wakati MD huwa anaunganisha tu kwenye specialization.
Haya ni mambo ya kimfumo tu mkuu.

Kule italy mtu unaweza ukasomea diploma ya umeme na degree ukachukua ya udaktari,hiyo ni kwa sababu ya mfumo tu.

Kuwa na mfumo wa kutokumruhusu CO asiende kuspecialize hiyo haina maana kwamba haiwezekani kuwa hivyo.

Lakini pia kama wanafanana kwa unavyodai, kwa nini mtu aliyetoka form six akienda kusoma MD atapiga miaka 5 na mmoja tena wa internship, na vivyohivyo kwa mtu wa CO hana added advantage kwenda kusoma anacukua na yeye miaka 5 na mmoja wa internship. Ni kama vile vyuo vikuu havioni utofauti wa form six na huyu CO

Lakini pia kama wanafanana kwa unavyodai,
Sijasema wanafanana nimesema wote ni madaktari japokuwa wanatofautiana maarifa,nisome tena mkuu wangu.
kwa nini mtu aliyetoka form six akienda kusoma MD atapiga miaka 5 na mmoja tena wa internship, na vivyohivyo kwa mtu wa CO hana added advantage kwenda kusoma anacukua na yeye miaka 5 na mmoja wa internship.
Kwani mwalimu wa diploma akitaka kwenda kusoma degree akipiga miaka mitatu ile ile bila kujali kama ana diploma je hiyo itamfanya yeye wakati ana diploma asiitwe mwalimu ?

Kusoma degree ya kozi husika kwa miaka kamilifu hakufanyi wewe usinasibishwe na diploma ya jambo hilo,hayo ni mambo ya utaratibu ya kimfumo tu.

Kama ambavyo watu wanacomplain kwamba masomo baadhi yapunguzwe huko mashuleni au mfumo wa elmu ubadilike sasa huwezi jua pengine na hili nalo likaingia humo.

Usijaalie jambo lililowekewa vikwazo vya kimfumo kwamba haliwezekani.

Lakini nikuulize swali,JE CO NI MBADALA WA NANI KATIKA VITUO VIDOGO VYA AFYA ?


Ni kama vile vyuo vikuu havioni utofauti wa form six na huyu CO,
Mtu ana div one ya point 3 anataka kuwa CO,unadhani atapewa tu cheti cha uCO kwa kuwa kapita form six ?

Mtu kamaliza form six je serikali inaweza kumuajiri kama CO katika vituo vidogo vya afya ?
Kama hapana why useme kana kwamba hakuna utofauti wa CO na form six ?
lakini wewe hapa upo hapa kutuaminisha kwama MD na CO wanafanana!.😳😳😳
Nakazi akwamba WANAFANANA KATIKA LENGO LAO KWA MGONJWA na lengo ni kutoa muongozo na kutibu.

Kimaarifa WAKO TOFAUTI KABISA MD ANAJUA MAMBO MENGI SANA KULIKO CO.
Kikubwa wote lengo letu ni kutibu wagonjwa na kutengeneza pesa pia, lakini haitufanyi tusione utofauti baina yetu
Utofauti wa maarifa haufanyi kuwepo na utofauti wa lengo.

Mimi nazungumzia usawa katika lengo na sio usawa kkatika maarifa,ni mpbavu pekee atakayeamini kwamba CO na MD wanafanana katika maarifa.
Na hii kitu ipo kwenye kada zote, Kuna mwalimu wa primary na mwalimu wa chuo wote ni 'WAALIMU' japo kazi yao wote kimuundo zinafanana kwa asilimia kubwa,
Sasa hiyo ndio nayo ipo katika udaktari ipo hivyo hivyo kwamba MD na CO wote ni madaktari kwa sababu kazi yao kimuundo inafanana kwa asilimia kubwa sana
lakini tofauti zipo kuanzia njia za ufundishaji, wanafunzi , mitaala na kadhalika.
Sasa hizi ni njia ndizo zinaleta utofauti,lakini wote lengo lao ni kufundisha.
 
MD ni CO aliyechangamka..full stop..zingine ni mbwembwe zisizo natija wala faida kwa wagonjwa zaidi ya kuwatibu.

#MaendeleoHayanaChama
Unaweza kuwa umesoma lakini hujaelimika bado, utakapoelimika utaelewe vizuri nini maana ya professions.
 
Hayo mambo yako wapi wewe? Daktari amuonee wivu Pharmacist? Pharmacist yupi huyo anagombana na daktari? Kwanza utayafahamiana wapi hayo wakati ulipo huoni interaction ya daktari na pharmacist.

Shida ni nyie ambao mliingia kwenye afya mkidhani mtafanana na wenzenu waliosoma masomo ya juu. Mnajitutumua kwa vitu msivyovijua. Ushauri wa bure mkasomee udaktari. Msijitie moyo kwamba ninyi ni madaktari. Shauri yako.
Kichwa chako kina shida. Wenzako tulishapita huko hata kuudharau udaktari wenyewe.
 
Hakuna Tofaut yeyote kati ya MD na CO kwenye kufanya kazi

Wote ni watu wa kaunta , anachofanya CO kwenye zahanat au kituo cha afya n hicho hicho anafanya MD hospital au kituo cha afya, kazi zao ni general

Diagnosis ya Malaria atakayo kufanyia MD n hiyo hiyo anayokufanyia CO , na Jambo ambalo litashindikana kwa CO n nadra sana MD kua na ujanja nalo , yanapilitiza moja kwa moja kwa wenye uwezo wao
Medicine doctor tunasoma miaka mitano kuna baadhi ya vitu CO anakuwa hafahamu mpaka na yeye akasome miaka mingine mitano... Vitu vingi sio vichache... Ingawa experience ya kazi huwa inawabeba ma co wengi hupata experience ya kazi.. Unafahamu kwamba baadhi ya manesi wakongwe wanaweza kufanya oparesheni kabsa ambayo kijana mbichi wa Md hajaizoea.... Kozi za afya ni kutegemeana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo mengi sana CO anayasoma akiyazingatia haswaa na akajiongeza na akawa anawaza nje ya box na kujiuloza kwa nini hiki kinakuwa hivi na kisiwe vile,akiwa na akili hii basi anakuwa yuko njema saaana katika utabibu wake na wagonjwa watampenda sana na kuelekezana waende kwake pale wanapoumwa.

Haya mambo tunayashuhudia sana
C. O ana shallow knowledge kwenye baadhi ya vitu mfano parasitology, medical microbiology.. Pathology huo ni mfano tu C. O anahtaji miaka sita tena kusoma Bachelor

C. O ana uwezo wa kutibu lakini uwezo wake hautofanana na MD, utofauti wao utakuja pale ambapo CO atakua amefanya kazi muda mrefu... Na more experience kuliko new MD...

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Natamani kuchangia hii mada ila naona imejaa ushabiki sana! CO na MD lao ni moja, majukumu ya kazi yanafanana, Bodi ya kuwasimamia ni moja, kiufupi kazini huwezi kuona tofauti yao wakiwa kwenye majukumu yao ya kawaida!

MD tofauti yake na CO ni Level ya Elimu na si vinginevyo! Kama ni issue ya uwezo wa kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.... Pia kuna MD ambao ni vilaza wa kutupa na wakati huo huo kuna ambao wako vizuri sana, hivyo hivyo kwa CO kuna wenye uwezo mkubwa sana na vilaza wapo pia.

MD zenyewe hizi za St. Joseph, Kampala n.k unakuta ni tofauti sana na MUHAS, UDOM n.k

Pia CO anayetoka Bombo Tanga, kibaha, Machame, Sengerema mara nyingi unakuta wana tofauti kubwa na hawa wa City collage, Tabdabui , DECCA n.k
 
C. O ana shallow knowledge kwenye baadhi ya vitu mfano parasitology, medical microbiology.. Pathology huo ni mfano tu C. O anahtaji miaka sita tena kusoma Bachelor

C. O ana uwezo wa kutibu lakini uwezo wake hautofanana na MD, utofauti wao utakuja pale ambapo CO atakua amefanya kazi muda mrefu... Na more experience kuliko new MD...

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Sahihi mkuu nakubaliana na wewe katika hili kwamba MD lazima awe na maarifa mengi kuliko CO
 
Ngoja turahisishe hivi.

Ualimu kuna ualimu ngazi ya certificate diploma na degree.

Je mwalimu mwenye diploma hastahiki kuitwa mwalimu kwakuwa ana diploma ?
Unazungumzia jina au maarifa?
 
Kwani lengo ni hizo steps ama lengo ni kutibu hiyo typhoid ?

Hizo steps ni njia tu ya kufikia diagnosis na kutibu tatizo lenyewe,lengo hasa ni kujua ugonjwa na kuutibu.

Kwa mantiki hiyo CO na MD wana lengo moja la kutibu na huo ndio udaktari wemyewe
Unazungumzia lengo au uwezo wa kufikia diagnosis?
 
Huwa nasikia majina haya
1: mkunga
2: nesi
3 :tabibu
4: daktari
KWA AKILI yangu Hawa wote wanahusika na afya za binadamu, pia kwenye ujenzi Kuna
1: Technician
2:mhandisi
SWALI: KWANINI KUNA UTOFAUTI WA MAJINA KWA MFANO KWA NINI WASIITWE WOTE WAHANDISI? badala yake wakaweka technician?
Kwenye jeshi Kuna Luteni na komandoo, naamini Luteni hawezi kujiita komandoo wakati hajawahi hata kuhudhuria hayo mafunzo ya ukomandoo, ingawa wote Ni Askari. Ninyi CO Ni Askari mgambo na Hawa MD Ni Askari kamili. Na CO KWANI MMENUNA?
 
Medicine doctor tunasoma miaka mitano kuna baadhi ya vitu CO anakuwa hafahamu mpaka na yeye akasome miaka mingine mitano... Vitu vingi sio vichache... Ingawa experience ya kazi huwa inawabeba ma co wengi hupata experience ya kazi.. Unafahamu kwamba baadhi ya manesi wakongwe wanaweza kufanya oparesheni kabsa ambayo kijana mbichi wa Md hajaizoea.... Kozi za afya ni kutegemeana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
fact
 
Hizo mbwembwe hazina msaada kwa wagonjwa..ingia night shift ukatibu wagojwa..MD ni CO aliyechangamka..unless mmoja awe anaua...ndio tutawatofautisha.

#MaendeleoHayanaChama
Mimi sijafanya kazi hospital lakini malezi yangu na hospitali huwezi kuyatenganisha, Nilikuwa nikimtembelea mzazi wodini(kazini) nikimkuta busy namsaidia kazi, nafahamu umuhimu wa nesi katika kutibu wagonjwa, Dakitari anapita round kwa masaa, nesi yuko na mgonjwa wakati wote, Hiyo night shift unayoisema najua ladha yake, Nesi ana kazi KUBWA kuliko hata huyo CO na MD.
 
Back
Top Bottom