Matokeo ya darasa la Saba kwa Mwaka 2024 yatoka, ufaulu wapanda kwa asilimia 0.29

Matokeo ya darasa la Saba kwa Mwaka 2024 yatoka, ufaulu wapanda kwa asilimia 0.29

Huku kayumba sisi wazazi tunakimbia majukumu ya kuwasimamia watoto. lakini huku kayumba ukiamua kuchukua majukumu ya mzazi nyumbani shule za kayumba mtoto anatoboa vizuri sana
Upo sahihi kabisa mkuu. Usimamizi hafifu tu wa baadhi ya wazazi.

Wa kwangu huwa anakuja na homework kila siku namsaidia kumuelekeza namna ya kutafuta majawabu sio kumsaidia kumwandikia majawabu.

Matokeo yake nayaona ni mazuri sana anafanya vizuri mno darasani na ana uelewa wa mambo nje ya anachofundishwa darasani maana nimemjenga hivyo kuwa na general understanding wa masuala ambayo ni common kwenye maisha ya kila siku.
 
Wakuu matokeo ya mtihani wa darasa la vii kwa mwaka 2024 yametoka.
View attachment 3138047
Matokeo ya Darasa la saba yatangazwa leo Oktoba 29, 2024 yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Necta Dkt. Said Ally, ambapo watahiniwa 974,229 kati ya wanafunzi 1,230,774 waliosajiliwa kufanya mtihani wamefaulu kwa kupata madaraja A, B na C.

Aidha, imeeleza kuwa kwa mwaka huu wa masomo 2024, ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 0.29 na kufikia asilimia 80.87 kutoka asilimia 80.58 mwaka 2023.

BONYEZA HAPA KUSOMA MATOKEO
Mkurugenzi wa necta ni mwislam kichaka walichokuwa wanatumia kujificha kimechomwa moto watafute sababu nyingine za kifeli
 
Ndio maana nasema hakuna umuhimu wowote wa kujistress kulipa mamilioni kwenye shule za English Mediums.

HAYA sasa twende kazi. Toa watoto wako kwenye shule za EM wapeleke Kayumba haraka sana.

Thank me later.

🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
kwa sasa EMS ni kutafuta tu misifa za kijinga
 
Matokeo ya nyakati hizi hayana amsha amsha. Hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 matokeo ya darasa la 7 yalikuwa ni stori kubwa mno. Kwa sisi tuliomaliza miaka ya 90 ilikuwa ni kawaida shule kupeleka form one watoto wawili au pengine hakuna kabisa. Mimi nilifaulu la saba ila kuna wenzangu ambao hawakwenda kidato cha kwanza na kuishia la 7 kielimu ninawaheshimu mno... jamaa walikuwa vichwa hatari na huenda wangefika mbali sana kielimu kwa zile jitihada zao ila kwa sababu ya umaskini wa familia na serikali wakati huo ndoto zao zikazimika. Ninawapongeza baadhi waliopita shortcut ya kwenye ishu za utalii na kutoboa kimaisha kuliko tuliofika chuo kikuu.
 
Mijadala yenyewe hii ya kina P.Diddy? Unataka mtoto wako aanze kulishwa propaganda za ushoga akiwa shule ya msingi eti eeh?
Endelea
Unaelewa kwa nini wakenya huwa wanakuja kuchukua top corporate post hapa kwetu,? Unakumbuka vodacom Ceo post ilivyoleta malalamiko. When people learn English language they automatically become smart
 
Matokeo ya nyakati hizi hayana amsha amsha. Hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 matokeo ya darasa la 7 yalikuwa ni stori kubwa mno. Kwa sisi tuliomaliza miaka ya 90 ilikuwa ni kawaida shule kupeleka form one watoto wawili au pengine hakuna kabisa. Mimi nilifaulu la saba ila kuna wenzangu ambao hawakwenda kidato cha kwanza na kuishia la 7 kielimu ninawaheshimu mno... jamaa walikuwa vichwa hatari na huenda wangefika mbali sana kielimu kwa zile jitihada zao ila kwa sababu ya umaskini wa familia na serikali wakati huo ndoto zao zikazimika. Ninawapongeza baadhi waliopita shortcut ya kwenye ishu za utalii na kutoboa kimaisha kuliko tuliofika chuo kikuu.
Sasa unakuta mko mzima una shule ya secondary moja tu
 
Back
Top Bottom