Matukio na Masimulizi ya Wazee wa Mwaka 47

Matukio na Masimulizi ya Wazee wa Mwaka 47

Sahihi, changamoto kubwa ni ukosefu wa uaminifu

Kama ulivyosema, badala ya kuweka milioni 20 peke yako, unajikuta unaweka 10 na mwenzio anaweka 10

Kwahiyo mkiwa serious mnaweza kupiga hatua pamoja na kufika mbali kibiashara na mafanikio
Nilikuwa nasoma article za biashara asubui, nikasoka business insight ya otedola na dangote hawa majamaa wame anza kitambo.

Just trust na kuvumiliana tu, imagine dangote ana anzisha energy refinery juzi, otedola ana weka mpunga bila kuwaza.
 
Nilikuwa nasoma article za biashara asubui, nikasoka business insight ya otedola na dangote hawa majamaa wame anza kitambo.

Just trust na kuvumiliana tu, imagine dangote ana anzisha energy refinery juzi, otedola ana weka mpunga bila kuwaza.
Wenzetu hawana tamaa, kibongo bongo mbia mwenzio anapambana kukumaliza ili vyote ulivyowekeza viwe vyake
 
Tukio la kuhama Kijiji kutokana na kufanana na mtoto wa jirani

Miaka mingi iliyopita,nilikuwa nikiishi kwenye kijiji X baada ya kuhamia pale kutokea kijiji Y nilichokuwa nikiishi awali kwaajili ya shughuli zangu za kilimo. Kama mnavyofahamu, miaka ile, sheria zilikuwa kali mno kwa wageni, ukiwa mgeni, ilikuwa ni lazima upelekwe kwa mjumbe wa nyumba kumi ili aweze kukutambua.

Baada ya mjumbe kunitambua kwamba nilikuwa mgeni kijijini kwake, nilirudi kwangu nilipofikia na kuendelea na shughuli zangu za shamba. Mjumbe alikuwa ni Mzee wa kama miaka 67 hivi enzi zile, na alikuwa na wake watatu, huyo mke wake wa tatu, alikuwa ni binti wa kama miaka 19 hivi na alikuwa mchangamfu sana kwa wageni.

Huyo mke mdogo wa balozi kwa kuwa alikuwa ndiyo mdogo kwa umri kuliko wenzake, kazi nyingi pale nyumbani kwa balozi, alikuwa anafanya yeye, kuanzia kuhudumia wageni watakaofika kwa balozi hadi shughuli za kwenda kuchota maji.

Nyumba niliyokuwa naishi pale kijijini, ilikuwa karibu na kisima cha maji kilichokuwa ndiyo kisima pekee kilichotegemewa pale kijijini.

Kwahiyo ilitokea yule mke mdogo wa balozi, kuwa tunaonana mara nyingi kila alipokuwa anakwenda kuchota maji hadi tukazoeana.

Baada ya miezi kadhaa ya kufahamiana naye, siku moja nilipokwenda kumsalimia balozi, nikamwona huyo mke wake mdogo akiwa ni mjamzito wa miezi 4 ama 5 hivi

Lakini safari hii hakuwa akinichangamkia kama ilivyokuwa awali, bali alinichukia waziwazi hadi wake wenzie wa balozi wakawa wanashangaa

Hata nilipomsalimia siku moja nilipokutana naye wakati anatoka shambani, hakuweza hata kuitikia salamu yangu

Baada ya miezi 9 ya ujauzito wake, hatimaye alijifungua salama mtoto wa kiume ambaye kwa maajabu nilifanana naye sana.

Baada ya miezi mitatu hivi tangu mkewe ajifungue, niliandaa zawadi na kwenda kumsalimia balozi pamoja na kumpa hongera kwa kuongeza familia.

Nilipewa mtoto na kumpakata kisha kumkagua kisirisiri kama kweli alikuwa akifanana na mimi maana kijiji chote walisema mke wa balozi amezaa mtoto aliyefanana mno na mimi, yule mtoto utasema nilikata kichwa changu na kumpachika, yaani alikuwa tumefanana mno.

Wale wake wengine wa balozi, pamoja na balozi mwenyewe wakasema mtoto nimefanana naye kwa kuwa mkewe alipokuwa mjamzito alinichukia, hivyo kuzaa mtoto aliyefanana na mimi.

Baada ya mtoto kuacha kunyonya, yule mke mdogo wa balozi akaanza tena kuja kunisalimia kila alipokuwa akienda kuchota maji.

Kwa kuwa nilikuwa nimeshamaliza kuvuna mazao yangu, niliamua kuhama moja kwa moja kile kijiji, niliona dalili ya kuchukiwa tena na yule mke wa balozi iwapo atabeba tena mimba.

Tangu tukio hilo litokee mwaka 47, limefanya nibadiri mtazamo wangu kabisa kuhusu mahusiano
 
Upo sahihi kwa mtazamo wako, ila nikueleze jambo, nyakati zinabadirisha watu

Wewe mwenyewe msimamo ulionao leo, unaweza jikuta umeubadiri miaka 30 ijayo

Jambo la kuzingatia, tuishi kwa malengo
Zinabadirisha = zinabadilisha ✔

Umeubadiri = umeubadili✔

Upo sahihi , ila jinsi taifa lilivyo nimatunda ya nyie wazee ving'ang'anizi.
 
Ukienda kwenye maduka ya vipodozi, watakueleza

Kwa sasa kupata wanawake weusi itakuwa vigumu mno, wengi wanajichubua

Juzi nilivunja ndoa ya mwanangu wa kiume alipokuwa anataka kuona

Niliagiza niletewe picha ya binti alipokuwa shule ya msingi

Picha ililetwa binti mweusi ti, alafu wasasa alikuwa mweupe utasema Mzungu

Nika mwambia kijana wangu, hapa hakuna mke
Sasa umeivunjia nini😅
 
Back
Top Bottom