Matumizi yako kwa siku ni sh. ngapi? Je, niko vizuri au mimi ni mwananchi mnyonge?

Njia nzuri ya kusave hela nunua kila kitu uweke ndani ,

Kaa mbali na wanawake, pombe

Kula vizuri Fanya mazoezi

Toa sadaka kwa wazazi Kama wapo

Tafuta passive income Kama kununua na kuuza hasa siku za weekend


Kuhusu bajeti yangu kwa siku huwa haitabiriki ila Mara nyingi siwezi kuzidi 50k maana sina familia.


Kitu kingine ukinunua chakula ukaweka ndani inasaidia Sana hasa kwa vijana tunaojiafuta maana chakula kinaleta utulivu wa kukufanya uwaze mambo mengine positive na sio kila siku kuwaza chakula.
 
Kama ulichoandika ni kweli na ukaendelea hivyo kwa muda mrefu, lazima utakuwa tajiri...

Maana hujasema hela unayotumia bar, au ile unayovihonga vitoto vya uswahilini kule kawe Ukwamani.
 
Ndio naanza kuapply, mwezi huu nafanya research kati ya kupika na kula hotelini kwa mtu mmoja gharama yake ikoje?
 
Matamizi yangu

Nauri kwenda na kurudi 1500 Tzs
Asubui sili
Mahana nakula 500 Tzs
Usiku nakula 1000 Tzs au Nadundia
Bando 300 Tzs (1000 siku tatu)

Jumla 3500 Tzs au 2500 Tzs

NB: mwenye connection ya kazi ofisi aniunganishe maana haya sio matumizi kabisa nakonda nabaki mifupa
 
Mimi ni fukara jamaa yangu lakini wewe inabidi wadau wakusaidie, unaweza kukauka.
 
Wewe ni mlalahoi tu. Hujafikia kuwa mlalahai.

Kaza buti.
 
Nimefurahi kuona nyumba unayopanga hamlipii umeme wala maji,
Kwa kuwa unaanza maisha ni mwanzo mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…