Matumizi yako kwa siku ni sh. ngapi? Je, niko vizuri au mimi ni mwananchi mnyonge?

Matumizi yako kwa siku ni sh. ngapi? Je, niko vizuri au mimi ni mwananchi mnyonge?

Kwenda kazini natumia nauli ya 2000, kwenda 1000 kurudi 1000, asubuhi haiwezi kuzidi 1000 chai na harakati zingine, mchana hapa napiga sahani ya wali na nyama/dagaa/migebuka daily, ni 2000 nashushia na juice ya buku, kwa hiyo mchana jumla ni 3000, usiku ratiba yake ni kama mchana tu, 3000 lazima nitumie, kwa hiyo kwa siku nzima natumia 8000/= vocha natumia 5000 kwa week japo week haifiki mwisho, kwa hiyo kwa siku lazima nitumie 10,000/=
Hapo sina familia, kwa mwezi natumia 300,000/= ...nyumba nakaa ya 80,000/= hapo sijapiga mahesabu ya zaka na sadaka na michango mingine ya kanisa na jumuiya, kwa hiyo kwa mwezi natumia 450K hata nijibane kivipi, kila mwezi kwenye account nabakiza kiasi cha laki moja kama akiba so tokea nimepata hiki kibarua nina akiba ya 1.5m kipato changu kwa mwezi ni laki tano tu,

Sina cha kujivunia sana kwa sababu sina plot ninayomiliki, wala asset yoyote ile, nachukia sana kwenda church Jumapili nakutana na watu wengi wakiendesha magari n.k najiona kama myonge sana lakini najipa matumaini tu kwamba ipo siku moja, Age bado sijafika 30, nina 26.

Wewe mdau matumizi yako kwa siku ni yapi? Shusha Nondo zako tupate kujifunza na sisi.
Kula ugali alfajiri......mchana kunywa maji(beba maji kutoka nyumbani).....jioni pika nyumbani....FUNGUA BIASHARA NDOGO JAPO GENGE...baada ya kazi shinda gengeni mwako.......Fanya hivi kwa miezi 3 halafu njoo tupe mrejesho.
 
Ila watu mpo vizuri sijaona bajeti ya mnyanduo, pombe kidogo & invoice za marafiki, ndugu na wengn
Mnyanduo sina milupo kwa sasa, japo wanakuwepo wanaondoka sio wa mizinga mikubwa hiyo, nachukua low profile akishapokea rungu anaondoka na 15,000/= na sio kila siku kwa mwezi maramoja moja, marafiki mimi sio mtu wa kujichanganya nashinda ndani nacheck movies,ndugu wanaonizunguka mimi ndio mnyonge kuliko wote kwa hiyo hakuna anaeniomba hela.
 
Mnyanduo, sina milupo kwa sasa, japo wanakuwepo wanaondoka sio wa mizinga mikubwa hiyo, nachukua low profile akishapokea rungu anaondoka na 15,000/= na sio kila siku kwa mwezi maramoja moja, marafiki mimi sio mtu wa kujichanganya nashinda ndani nacheck movies,ndugu wanaonizunguka mimi ndio mnyonge kuliko wote kwa hiyo hakuna anaeniomba hela.
Kigoma unayokaa ni mjini au Vijijini?
Mda wa kazi ni masaa mangapi?
 
Niko kigoma mjini, Mimi ni mwalimu kwa hiyo muda unajulikana, naenda saa mbili, kutoka inategemeana naweza toka saa 7/8 /9 mwisho.
Aisee kumbe unatoka saa 9 muda wa kupika unao kabisa! Unaonaje ukipika zako wali jioni unaobaki unanywea chai kama Grahams alivyosema
Wewe uwe unanunua tu chakula cha mchana.
 
Aisee kumbe unatoka saa 9 muda wa kupika unao kabisa! Unaonaje ukipika zako wali jioni unaobaki unanywea chai kama Grahams alivyosema
Wewe uwe unanunua tu chakula cha mchana.
Nimeshaanza kulifanyia kazi mkuu, jana nilienda kununua mchele kilo 10, maharage kilo 2, na unga kilo 5 , dagaa nimechukua nusu sado, nataka nione mwisho wa mwezi kama nitaweza kusave laki mbili.
 
Mnyanduo sina milupo kwa sasa, japo wanakuwepo wanaondoka sio wa mizinga mikubwa hiyo, nachukua low profile akishapokea rungu anaondoka na 15,000/= na sio kila siku kwa mwezi maramoja moja, marafiki mimi sio mtu wa kujichanganya nashinda ndani nacheck movies,ndugu wanaonizunguka mimi ndio mnyonge kuliko wote kwa hiyo hakuna anaeniomba hela.
Hongera sana Bw Mdogo.
Hapo Kigoma kwa Mtaji wako wa 1.5M waweza anza na Biashara ndogo.
1. Nunua Freezer, Baiskeli na Dell la barafu. Agiza kijana toka Kibondo. Funga barafu za Vikaratasi kijana anasambaza mmashuleni nk. Ukiweza vijana wawe zaidi ya mmoja.

2. Tafuta Vijana uzza mayai ya kuchemsha kwa Trey.

3. Tafuta Vijana wauze Kahawa, Kashata, Karanga nk.

4. Tengeneza Matoroli 5 peleka pale sokoni kijana anakuwa anakodishia wanaobeba mizigo mind you waendesha mikokoteni sio wote wanaomiliki wengine wanakodisha.

5. Mtaji ukikua fungua kijiwe cha spea za Pikipiki

Zingatia, Wenyeji wa Kigoma Wanaamini sana Ushirikina kwenye biashara nk, kuwa nao makini maana nimeyapitia.
 
Nimeishi Dar mzee, nimesoma Mugabe secondary japo nimezaliwa Morogoro, usijifanye mjuaji, nimeishi kwa kwa kipato cha laki 3, kabla sijaajiriwa, nimesoma hapo udsm miaka 3, nikamaliza nikabaki kupambana hapo mpaka nilipoajiriwa mwaka jana, kwa hiyo Dar sio kigezo cha matumizi makubwa.
Labda Dar matumizi yanaongezeka Kwa upande Wa nauli, maana utajikuta unaishi nje YA mji mfano Bunju,Goba au Kijichi, ambapo unakuta unapenda Gari mbili Kwa siku sometimes Na daladala

Mfano Mimi nauli Kwa siku nisipotumia Gari, nikutumie public transport, kwenda Na kurudi natumia 6,000 Na hapo nimejibana sana

Nyumba Kwa Dar minimum price Ni laki moja Na nusu, chumba Na sebure hapo Kwa single..ukiwa Na familia..mke watoto Na house girl..minimum price Ni 250,000
 
Hongera sana Bw Mdogo.
Hapo Kigoma kwa Mtaji wako wa 1.5M waweza anza na Biashara ndogo.
1. Nunua Freezer, Baiskeli na Dell la barafu. Agiza kijana toka Kibondo. Funga barafu za Vikaratasi kijana anasambaza mmashuleni nk. Ukiweza vijana wawe zaidi ya mmoja.

2. Tafuta Vijana uzza mayai ya kuchemsha kwa Trey.

3. Tafuta Vijana wauze Kahawa, Kashata, Karanga nk.

4. Tengeneza Matoroli 5 peleka pale sokoni kijana anakuwa anakodishia wanaobeba mizigo mind you waendesha mikokoteni sio wote wanaomiliki wengine wanakodisha.

5. Mtaji ukikua fungua kijiwe cha spea za Pikipiki

Zingatia, Wenyeji wa Kigoma Wanaamini sana Ushirikina kwenye biashara nk, kuwa nao makini maana nimeyapitia.
Hiyo namba 5 ndio inanifanya nisiweze au niwe mnyonge wa kuanzisha biashara huku, nilipokua DSM nilikua na mtaji wa laki 5 tu na ulinitosha kufanya harakati zangu hapo karume sokoni nilikua nakula na nilipanga bungeni hapo, kigoma huku kati ya watu 100, wote 100 wanaamini uchawi upo, 99 kati ya hao wanaupractise kabisa, nina uwezo wa kwenda bank wakanipa mkopo wa milion 20 lakini nashindwa kwa sababu huu mkoa, hautoi ruhusa ya mtaji au ubora wa bidhaa kufanya vizuri sokoni bali unae mganga gani mzuri? Kama mawazo ya biashara ninayo mengi tu, nimeshaenda sehemu wanapaita kibirizi, kuangalia namna ya mimi kuleta dagaa wa Mwanza huku (wanatoka sana) lakini watu wa huku sasa, wanakuona kama mshindani wao, hawatadhuru biashara tu, watafika na kwenye afya yako, uchawi na ushirikina ni mwingi mno.
 
Back
Top Bottom