Mauaji ya kutisha yafanyika Wilayani Mwanga. Rais tafadhali ingilia kati uisaidie hii familia

Mkuu dadamlamayao , huyo bibi baada yakupata vitisho, wanae walimchukua na kuishi nae Arusha, sasa 2 wks ago, Maradona aliwapigia simu watoto wa huyo mama akawaambia wamrudishe nyumbani kwani yeye kama diwani anamuhakishia usalama huyo mama, sasa baa ya huyo mama kurudishwa nyumbani, haijapita wk akauliwa....
Baada ya mama kupata vitisho wao kama familia walichukua uamuzi upi ili kuhakikisha usalama wake unazingatiwa? Chanzo Cha ugomvi ni Nini haswa?
 
Namba za wahanga ni: 0766430284 0689512555 & 0672740412
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT.

Jana nilifanikiwa kufika Wilayani Mwanga katika Kijiji cha Mangyo, kitongoji cha Vongo B. Kuna Mama mwenye umri wa zaidi ya miaka 80, ambaye tarehe 01/11 majira ya saa 1:45 Usiku, wakati akipika chakula chake cha usiku, alivamiwa na kuchinjwa shingo yake kama kuku! Haijaishia hapo, watu hao walimpiga mume wa marehemu kichwani na kumkata mkono, na baada ya mauaji hayo watuumiwa walitokomea kusikojulikana!

Cha kushangaza baada ya polisi kupewa taarifa, walifika 2/11 na kiuchukua mwili na kuupeleka mochwari ya Kijiji inayoitwa Kifula, na 3/11 ndugu wa marehemu waliofuatilia hilo suala wakaambiwa na CID wa wilaya kwamba wanaweza wakauzika huo mwili!

Msaada hii familia inayohitaji ni ifuatayo:

1. Kwanini police iruhusu mwili uzikwe angali upelelezi/majibu ya mauaji hayajakamilika/hayajatolewa kwa familia?

2. Mauaji haya siyo ya kwanza kwani Kuna watu wengine walishauliwa katika mazingira kama haya na hakukuwa na ufuatiliaji wa polisi, hivyo inaonekana mauaji haya Yana baraka ya polisi/Mkuu wa wilaya!

3. Diwani wa eneo hilo (Maradona), wiki mbili kabla ya mauaji haya, aliitaka familia hii imrudishe marehemu nyumbani kwake kwani aliwahakikishia usalama wake, na baada ya marehemu kurudi tu, ndipo mauaji haya yakafanyika! Je bwana Maradona hajahusika katika mauaji haya? Pia izingatiwe kuwa Maradona ana undugu na watuhumiwa (mfano ni urafiki/ukaribu wake na bwana Mashauri ambaye ni kati ya watuhumiwa wa mauaji haya), hivyo anatumia cheo chake cha udiwani kuiangamiza hii familia.

4. Je, usalama wa hiyo familia itakuwa mikononi mwa nani? Ikizingatiwa hii familia inaendelea kupokea vitisho kutoka katika familia ya Mashauri? Ikumbukwe, mume wa marehemu ni mgonjwa Sana baada yakukatwa kichwani na kuvunjwa mkono, pia mtoto mkuwa wa marehemu (Judika Yohana Mfinanga) anaendelea kupokea vitisho toka Kwa bwana Mashauri.

Maziko yanatakiwa kufanyika kesho juma tatu, ila chondochonde Mheshiwa Rais, naomba uingilie kati mauaji haya na ikiwezekana marehemu asizikwe kesho mpaka uchunguzi wakina ufanyike.

CC:
1. Mkuu wa wilaya ya mwanga
2. CID mwanga
3.Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro
4. @PaulMakonda
5. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa
6. Mh. Rais
7.Vyombo vya habari mkoa wa Kilimanjaro

NB: Samahani kwa uandishi mbaya.
CC: Dkt. Gwajima D
 
Marehemu alipelekwa wapi alikotakiwa arudishwe, diwani anasema atahakikisha usalama wake, maana yake aliondoka sababu hakuna usalama, nani alietishia usalama wake, mtoto wake unadai anatishwa, kafanya nini hadi atishiwe, kwa nini unadhani polisi wako kinyume na marehemu?

Mtoa mada umeficha vitu vingi kuhusu familia ya maeehemu ambavyo vingetuongezea uelewa wa tukio
Au kuna mambo ya kishirikina nyuma.ya hayo mauwaji!!?
 
I concur with you Mkuu. Just imagine, despite the fact that have shared the numbers here, no one has just even dare to call the victims[emoji848]
Mkuu nakuhaidi litafanyiwa kazi na wahusika,ni swala la muda tu utaona!!
 
Asante Sana Mkuu. Ila mpaka Sasa hivi nasikitika kukujulisha kwamba wahanga hawajapigiwa simu yoyote na kwa maagizo ya CID wilaya wanatakiwa wazike kesho, angali hata primary investigation result hawajapatiwa! Can someone please assist them🤔!!!! Mama Samia please do something 🙏🏾
 
Mashauri na hiyo family wana ugomvi wa nini?
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT.

Jana nilifanikiwa kufika Wilayani Mwanga katika Kijiji cha Mangyo, kitongoji cha Vongo B. Kuna Mama mwenye umri wa zaidi ya miaka 80, ambaye tarehe 01/11 majira ya saa 1:45 Usiku, wakati akipika chakula chake cha usiku, alivamiwa na kuchinjwa shingo yake kama kuku! Haijaishia hapo, watu hao walimpiga mume wa marehemu kichwani na kumkata mkono, na baada ya mauaji hayo watuumiwa walitokomea kusikojulikana!

Cha kushangaza baada ya polisi kupewa taarifa, walifika 2/11 na kiuchukua mwili na kuupeleka mochwari ya Kijiji inayoitwa Kifula, na 3/11 ndugu wa marehemu waliofuatilia hilo suala wakaambiwa na CID wa wilaya kwamba wanaweza wakauzika huo mwili!

Msaada hii familia inayohitaji ni ifuatayo:

1. Kwanini police iruhusu mwili uzikwe angali upelelezi/majibu ya mauaji hayajakamilika/hayajatolewa kwa familia?

2. Mauaji haya siyo ya kwanza kwani Kuna watu wengine walishauliwa katika mazingira kama haya na hakukuwa na ufuatiliaji wa polisi, hivyo inaonekana mauaji haya Yana baraka ya polisi/Mkuu wa wilaya!

3. Diwani wa eneo hilo (Maradona), wiki mbili kabla ya mauaji haya, aliitaka familia hii imrudishe marehemu nyumbani kwake kwani aliwahakikishia usalama wake, na baada ya marehemu kurudi tu, ndipo mauaji haya yakafanyika! Je bwana Maradona hajahusika katika mauaji haya? Pia izingatiwe kuwa Maradona ana undugu na watuhumiwa (mfano ni urafiki/ukaribu wake na bwana Mashauri ambaye ni kati ya watuhumiwa wa mauaji haya), hivyo anatumia cheo chake cha udiwani kuiangamiza hii familia.

4. Je, usalama wa hiyo familia itakuwa mikononi mwa nani? Ikizingatiwa hii familia inaendelea kupokea vitisho kutoka katika familia ya Mashauri? Ikumbukwe, mume wa marehemu ni mgonjwa Sana baada yakukatwa kichwani na kuvunjwa mkono, pia mtoto mkuwa wa marehemu (Judika Yohana Mfinanga) anaendelea kupokea vitisho toka Kwa bwana Mashauri.

Maziko yanatakiwa kufanyika kesho juma tatu, ila chondochonde Mheshiwa Rais, naomba uingilie kati mauaji haya na ikiwezekana marehemu asizikwe kesho mpaka uchunguzi wakina ufanyike.

CC:
1. Mkuu wa wilaya ya mwanga
2. CID mwanga
3.Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro
4. @PaulMakonda
5. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa
6. Mh. Rais
7.Vyombo vya habari mkoa wa Kilimanjaro

NB: Samahani kwa uandishi mbaya.
Duu hii mbaya
 
Hakuna binadamu mwenye akili timamu atatunza hasira Kwa muda mrefu kulingana na maelezo ya Mleta mada na baadae kutimiza azma yake kikamilifu, ni LAZIMA nyuma kuna sababu za msingi...

Kama ni uchawi hata ingekuwa ndugu yangu acha auwawe, hv unajua mambo anayofanya mchawi wewe?

Makanisa Misikiti mchawi ataingia mule na kufanya kufuru, mchawi haoni shida kufanya mapenzi na mwanae wa kumzaa acheni kutetea mambo ya ajabu...

Usilazimishe watu kuamini unachoeleza unajuaje hata diwani alikuwa Muhanga?
 
Back
Top Bottom