Sio kosa wala sio jambo la kisiasa kuwakilishwa na mawakili 386, kwasababu sheria za nchi zinatoa haki kwa washtakiwa wote kutetewa na mawakili mbele ya mahakama (Natural Justice - Right To Be Represented).
Ila cha ajabu CCM wataligeuza jambo hilo la Gaidi Freeman Mbowe kuwa la kisiasa zaidi, kama alivyotangulia IGP Sirro kuligeuza la kisiasa jana kwenye press na waandishi wa habari. Akaenda mbele zaidi na kumtia hatiani hata kabla mtuhumiwa Gaidi Freeman Mbowe hajafikishwa mbele ya mahakama.
Cha ajabu IGP Sirro hakuwahi kuongelea kwenye vyombo vya habari swala la viongozi wa umma kutumia vijana wake wa police kufanya uhalifu. Mfano, Paul Makonda na Ole Sabaaya walivokua wakitumia vijana wa IGP Sirro kufanya uhalifu wa kutumia silaha na risasi (Kama alivosema jana tunanunua kwa hela zetu) kuteka na ujambazi Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Kilimanjaro.
IGP Sirro mungu anakuona, usichokifahamu kesi ya Gaidi Freeman Mbowe umeishaivuruga kwa kuiongelea mbele ya vyombo vya habari, na mmeshaisiriba kinyesi Tanzania kwenye swala la mbowe.