Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Hoja nzuri- sasa wakili Kibatala angalia alikopotezea mda
ulitumiwa 500,000 ukatoa 499000 umemwambia mh. Jaji 1000 imeenda wapi? halafu watu mnasema kaupiga mwingi na unaona una uwezo wa kupima uwezo wangu wa kufikiri- kwanza hicho kipimo hakipo
Kesi nzima hapo ndo unaona kukosea kuuliza 1000 ilienda wapi? Ilikuwa ni lazima iulizwe labda shahidi angeweza kusema hiyo 1000 sasa ndo ilikuwa inunue vilipuzi, mabomu, ikate magogo,n.k
 
Mwanzoni katika kesi ya Mbowe, Kila Pingamizi la utetezi lilikuwa linagonga mwamba na vielelezo vikawa vinapokelewa “by hooks and crooks”

Utetezi ukabadili mbinu kuokoa muda wa wateja kwani walijua mapingamizi yao yangekula muda na yangetupwa.

Ikabuniwa mbinu mpya

Utetezi ukawa unakubali vielelezo na ushaidi uingie mahakamani.

Wakawa wana challenge ushahidi na vielelezo kwa mlango wa nyuma wa cross examination.

Mashaidi wakapwaya na vielelezo vikapwaya mbele ya jaji watanzania wakishuhudia.

Wakabainisha blunders mbali mbali zifuatazo

1. Washtakiwa walikamatwa kabla hata jalada halijafinguliwa. Hii inamaanisha waliwakamata ndipo jitihada za kupika kesi ndio zikaanza. Inaonekana wapangaji wa hili walihamaki kuona makomandoo wakimlinda Mbowe na Lissu. Pengine mawasiliano yao yakafatiliwa yakawaongoza kwa Urio

Inaonekana Urio “akafinywa” (Haya yanathibitishwa na maelezo ya watuhumiwa katika kesi ndani ya kesi kuwa walimuona urio akipigwa kituo cha Tazara)

Baada ya kufinywa Urio akaeleza jinsi alivyowatafutia kazi lakini akalazimishwa kuwa shaidi wa Jamuhuri ili kulinda kazi yake.

Katika hali ya kupanick wapangaji wa kesi hii wakahisi inawezekana makomandoo wote waliofukuzwa kazi watakuwa wameenda kufanya kazi kwa Mbowe hivyo katika kamata kamata ndipo Komandoo MHINA akakamtwa Tabora na kina Kingai na Mahita. (Mhina alitoa ushahidi akiwa defense side)

2. Nyaraka zilikuwa zinaungwaungwa. Utetezi uliooomba Detention register ya Chang’ombe na Central kwa tarehe walizokamtwa watuhumiwa, kwa kuwa Mashtaka hawakujiandaa na hili wakafoji nyaraka kwa kubackdate ikainekana wazi lakini Jaji akaamuru daftari lipokelewe.

3. Extraction report ya Tigo inaharibu kila kitu kwani inaumbua kuwa file lilifunguliwa 2021 lakini mashtaka walifai file lilifunguliwa 2020. Ripoti ya tigo inajibu file la polisi lenye refence ya mwaka 2021. Kipengele hiki kina legal implication kubwa sana kwa faida ya defense

4. Prosecution wameshindwa kuipa kesi miguu kwa kuonyesha ni jinsi gani pesa alizotuma mbowe ziliweza kuprocure ugaidi. Pesa zinaonekana ni za nguo,chakula, nauli. Pesa nyingine upelelezi hawakusema zilitumika vipi bali ukawa unajibu ni transaction fees.

Katika hoja ya transaction fee Kibatala alikuwa na swali moja tu.

Swali: Ulimwambia mheshimiwa jaji maswala ya transaction fee?

Jibu: Sikumwambia

Swali:Katika maelezo yako kuna sehemu tutaona umeelezea hivyo?

Jibu: Sikueleza

Hapa ndipo kesi ilipokatwa mtama

5. Polisi hawakijui kitendea kazi chao PGO. Kila ilipogusiwa PGO walikuwa wanatoa macho kama wanasoma talaka.

Hawajui Fomu ya Kuzuia mali, Fomu ya Gari la polisi, Fomu ya kulebbel vizibiti, nk.

View attachment 2121994
Mhe. Jaji, naomba kwenda washroom.....spana zikizidi mkojo unambana kwenye suruali.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni kwamba Mbowe na wenzake watatu ni magaidi, ila Rais ameombwa kuifuta kesi yao kama msamaha!? Au ni vipi? Nisaidieni hapo.

Cc WIGWA
Hata mimi sijaelewa hapa, siasa ni michezo kama michezo nyingine.

Tumsubiri chifu arudi nchini tuone kama atasema lolote.
 
Umenena vizuri sana mkuu ili Taifa lisonge mbele, tuanze upya. Lakini kama ingekua ni kitu kinawezekana kufanyika, unaona mtu kama ACP Kingai akiulizwa, anaweza kuongea ukweli na kuomba msamaha ili awe huru kwenye nafsi yake kwa yale aliyoyafanya kuifikisha hii kesi ilipofika?
Ni ngumu sana kuisemea nafsi ya mtu. Lakini naamini akijua hakuna adhabu ya ziada baada ya kuomba msamaha naye anaweza kukiri ukweli na kuomba msamaha.

Na hii dhana ya kuomba msamaha ni dhana ngumu sana kwetu Tanzania kwasababu mara nyingi viongozi wanakosea lakini badala ya kuwaomba msamaha wananchi utasikia wanakanusha au wakati mwingine wanajikausha kabisa kama sio wao waliokosea wananchi.

Na wakati mwingine tu hata katika ngazi ya familia suala la kuombana msamaha linakuwa gumu sana. Lakini kama taifa lazima tufike mahali tuwe na sehemu ya kuanzia. Na ingependeza zaidi tukanzia hapa kwenye kesi ya Mbowe jumlisha kumharibia vitega uchumi vyake na Lisu kupigwa risasi kisha tusonge mbele pamoja kama taifa.
 
Na kwa muonekano wa huo mguu, jamaa angepigwa mzinga parefuu.

Cc Tate Mkuu
Yaani nipe tu pole, nikweli sijapata chochote valentine hii tofauti na maneno matamu amabayo kwangu sio muhimu.

Ila kupitia valentine hii nimetega mtego nina uakika utanasa, si unajua kuwekeza kidogo ukaja pata kkikubwa baadae.
Mzinga wa valentine ntaupata indirectly si unajua sisi tunaojielewa hatuombi indirect? Tunasubiriaga nafasi itokee mtu alipe deni bila kujua.
 
Hii kesi imedhihirisha kwamba kuna watu wengi wako magerezani kwa kukosa wa kuwatetea.Polisi walio wengi hukamata wangu na kuwafungulia kesi kwa makosa ambayo hayakufanyika.Nyie mbolisi Mungu atawaumbua na mtakuja kulia kilio cha mbwa.
 
Kesi nzima hapo ndo unaona kukosea kuuliza 1000 ilienda wapi? Ilikuwa ni lazima iulizwe labda shahidi angeweza kusema hiyo 1000 sasa ndo ilikuwa inunue vilipuzi, mabomu, ikate magogo,n.k
Huyo uwezo mdogo wa kuchambua.maswali madogo madogo yenye logic kubwa.
 
Nafikiri wanachadema na wapenda haki wote Tanzania wanapaswa kuweka akiba mpaka hapo jaji atakapotoa hukumu yake. Naona wengi hapa wanashangalia kabla ya hukumu lakini ndio ile hali ya watanzania kusahau mambo ya msingi ndani ya muda mfupi. Watu wameshasahau jinsi mapingamizi ya wazi yalivyokuwa yanatupwa na jinsi maamuzi tata yalivyokuwa yanaamuliwa tokea jaji wa kwanza, wa pili na hata huyu watatu. Kama sheria na taratibu zingefuatwa tokea mwanzo hii kesi ilikuwa ni mfu tokea mapingamizi ya awali lakini ilitumika namna kuiendeleza mpaka Mungu alipoamua kuudhihirisha ukuu wake kupitia mashahidi wa mchongo kujichanganya sana kizimbani.

Kwangu mimi kama kuna makubaliano ya kuimaliza kesi bila masharti yoyote ni jambo la kupongezwa na ninaombea iwe hivyo. Sisi watanzania ni wamoja na hasa sisi tuliokulia enzi za Nyerere pamoja na shida zote za miaka ile lakini kuheshimu utu wa mtu na usawa ilikuwa ndio nguzo kubwa ya umoja wa taifa letu. Hakukuwa na matabaka ya aina yoyote lakini sasa hivi kuna watu eti wanataka kujiona wao ni bora na wanahaki zaidi kuliko wengine katika nchi hii kwa sababu tu wapo chama fulani. Hivi kuna raha gani ya maisha kumsingizia binadamu mwenzio mwenye familia na wategemezi kama wewe eti gaidi akaozee jela ili tu upate cheo? Hivi ni lini watanzania tulianza rasmi kuwa roho za kikatili kiasi hiki?
Kwa kweli inatia uchungu sana hasa nikikumbuka upendo wa watanzania tuliokuwa nao sio tu kati yetu watanzania kwa watanzania bali ulivuka mipaka mpaka Afrika nzima kiasi kwamba Tanzania ilisaidia nchi nyingine kupata uhuru wao.
Matatizo Makubwa yalianzia October 2015 Mpaka March 2021.
 
Kesi nzima hapo ndo unaona kukosea kuuliza 1000 ilienda wapi? Ilikuwa ni lazima iulizwe labda shahidi angeweza kusema hiyo 1000 sasa ndo ilikuwa inunue vilipuzi, mabomu, ikate magogo,n.k
Tusiongee mengi - tuongee Jumamosi asubuhi
 
Mama leo akihojiwa na mtangazaji wa DW ameshangaza Sana kwamba hakuna mtuhumiwa wa ugaidi aliyefungwa kesi iko mahakamani tuache Jambo kesi iamuliwe na mahakama hiyo kesho ,bbc akihojiwa alisema washafungwa au alishindwa kutofautisha mahabausu na kufungwa gerezani
 
Nachojua hata kama ameombwa kumwachia hawezi mwachia sasa hivi ataprove failure.kwahiyo watazungushwa weee siku zitapita.

Mpaka aachiwe lazima kuwe na ushahidi kuwa sio gaid. Sasa nani ataleta ushahidi huo kama sio kuacha kesi iendelee?

Tutaona huko mbele unless kuna makubaliano nje ya pazia

Mpaka aachiwe lazima kuwe na ushahidi kuwa sio gaid. Sasa nani ataleta ushahidi huo kama sio kuacha kesi iendelee?
Mkuu Upande wa mashtaka, umeshamaliza ushahidi wao hivyo. Ushahidi uliotoka, ndiyo huo uliousikia wa hao mashahidi 13.
Kulichobaki, ni mahakama kuona kwa ushahidi uliotolewa, ni kweli kuna UGAIDI uliofanyika, au kutaka kufanyika? Kama ni ulikuwepo, akina Mbowe nao, wataanza kujitetea kuwa sio kweli au kweli!
Sasa, hapa JF kama wewe ni kweli mmojawapo wa ma -G.T, na huna mihemko ya ITIKADI za kisiasa, unaweza kujua, kama kuna ukweli wa TUHUMA hizo, au laaah!
 
Mkuu Upande wa mashtaka, umeshamaliza ushahidi wao hivyo. Ushahidi uliotoka, ndiyo huo uliousikia wa hao mashahidi 13.
Kulichobaki, ni mahakama kuona kwa ushahidi uliotolewa, ni kweli kuna UGAIDI uliofanyika, au kutaka kufanyika? Kama ni ulikuwepo, akina Mbowe nao, wataanza kujitetea kuwa sio kweli au kweli!
Sasa, hapa JF kama wewe ni kweli mmojawapo wa ma -G.T, na huna mihemko ya ITIKADI za kisiasa, unaweza kujua, kama kuna ukweli wa TUHUMA hizo, au laaah!
Kesi ya mbowe ni ya kupika,ni vijambo vya kisiasa hili wawaweke upinzani busy wakikamilisha mambo yao mengine.

Upinzani hawako bungeni, wakiwacha mbowe uraian atawasumbua na katiba mpya ,sijui haki sijui nini.

Cha kufanya ni kumuweka ndani , kiwaka kazi ya kwenda mahakamani pia kuwaweka busy wananchi wakifatilia kesi hiyo.
 
Ila walishindwa kupangua ukweli kuwa Mbowe alimtumia pesa Urio
Kwani kuna dhambi gani Mbowe kumtumia Urio pesa? Lakini pia upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa hizo pesa zimetumika kufadhili vitendo vya kigaidi.
 
Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali kumpa mtu sampuli ya Sirro kuwa IGP wakati hakuna anachojua tofauti na kubambikia watu vyesi feki ili mradi tu siku moja wamruhusu agombee ubunge kwa tiketi ya ccm.

Sirro is very useless and a poor excuse for an IGP.

Asubiri kesi itupiliwe mbali ndio tuje tumkandie humu vizuri. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom