Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Mawaziri Selemani Jafo na Dotto Biteko watunukiwa PhD ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

Kuna kautamaduni kameibuka ka kuchukia watu wanaofanya bidii na kufanikiwa katika kazi, biashara, masomo au hata maisha kwa ujumla.

Ukipata cheo watasema umependelewa, ukifanikiwa kibiashara watasema ni freemason una misukule dukani, ukifanikiwa kielimu utasikia mara hii si lolote si chochote amefoji tu! Acheni hizo. Acheni wivu.

Kama na nyie mnataka kuwa 'doctor' kasomeni. Mwenzenu Jafo amebukua pale UDOM huku akiendelea na majukumu yake ya uwaziri, na leo anatunukiwa PhD yake.

Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.

Hongera sana Selemani Jafo, PhD.
Pamoja na maneno mengi sana..hujandika Selemani amepata PhD ya nini. Na ameisotea miaka mingapi. PhD nyingi vio vya bongo ni usanii mtupu..kifupi PhD nzuri unapata ukiwa scratched. PhD gani unamicheo kibao,? nani atakunyima huku ukienda na Bahasha bhana? If you want to Prove my point "Check how those so called Professors in the government wanadeliver nini.angalia jinsi wanavotushangaza..Mwingine jana tu anadai hajui kupanda kwa gharama ya vifaa vya ujenzi.
 
Publication siyo lazima katika kupata PhD, inategemea chuo na chuo. Kuna PhD za coursework na dissertation (fanya google search utaona nyingi tu), hata UDSM pale IDS kulikuwa na mpango wa kuanzisha a taught PhD (PhD by coursework), yaani unaingia darasani unaimbiwa lectures weeee, halafu unapigwa U.E ukifaulu unavaa gamba la PhD sawa na wengine waliokuwa wanalala maabara.
Vyuo "serious" lazima hiyo Dissertation yako itoe paper kwenye reputable journal hata kama una A zote kwenye coursework, bila kutimiza hicho kigezo huwezi kuruhusiwa kudefend dissertation (research) yako, Sasa kama hicho chuo ulichokitaja nacho ni serious then its Ok.
 
Basi huyu alikuwa anajua chemistry, CH114 and 220. Ukivuka hapo umemaliza UDSM from dept of science! Alimaliza form six, akenda Canada for BSc, MSc, and PhD from the same University! He was good upstairs!
Lakini alikuwa kicheche! Kicheche kabisa kwa maana halisi. Kicheche ni mnyama fulani huwa anasubiri ufuge kuku halafu aje kuwawinda bandani.
 
Kwani Jaffo ndiye mzaramo wakwanza kupata PhD ? Mbona kelele sana?
 
Publication siyo lazima katika kupata PhD, inategemea chuo na chuo. Kuna PhD za coursework na dissertation (fanya google search utaona nyingi tu), hata UDSM pale IDS kulikuwa na mpango wa kuanzisha a taught PhD (PhD by coursework), yaani unaingia darasani unaimbiwa lectures weeee, halafu unapigwa U.E ukifaulu unavaa gamba la PhD sawa na wengine waliokuwa wanalala maabara.
si rahisi kihivyo. Lazima hiyo kazi iwe publishable! Uko sahihi lkn lazima katika coursework kuwe na kitu kipya unakielezea, a new theory at least...... and something of that nature.......
 
Wewe tu ni mwanaume kama mabinti. Sisi hatuna mpango na hayo ma-PHD ya kuokoteza. Sisi tunachotaka uwajibikaji na utendaji bora. Tunataka watu kama Sokoine. Wasio na tamaa. Hizo PhD za siku hizi hata hazijulikani zina maana gani?.
 
Lakini alikuwa kicheche! Kicheche kabisa kwa maana halisi. Kicheche ni mnyama fulani huwa anasubiri ufuge kuku halafu aje kuwawinda bandani.
Niwe mkweli, amenifundisha miaka 4, sikusikia kitu hicho..... Prof Gaspar Ndaalio...alikuwa Mchaga. RIP my Prof!
 
Kuna jitu nimeona huko limeshaenda kufukua huko mitandaoni linadai hiyo thesis ya Jafo inafanana na ya nani sijui wa huko Kenya! Hivi, kati yako wewe wa madongo kuinama na maprofesa wa UDOM, ni nani mwenye uwezo wa kutambua kuwa thesis iko sahihi au la?

Unaamini kabisa kuwa unaweza kuwakosoa maprofesa waliomsimamia Jafo hadi leo anapomalizia defense?

Narudia: acheni wivu. Kama jambo huliwezi sema "siwezi", usiseme "haiwezekani". Jafo ameweza, wengine igeni, jifunzeni.
Ungeandika tu kuwa Jafo anapata PhD leo ingetosha!
Mihemko yako ya kike ndio imeharibu kila kitu, ona unaogelea maneno sasa!
 
Back
Top Bottom