Mawaziri waliotemwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Mawaziri waliotemwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Agosti 30, 2023 amefanya mabadiliko Baraza la Mawaziri ambapo Waziri mmoja na Manaibu wawili wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wengine.

View attachment 2733703
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula

Miongoni mwa walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ambaye nafasi yake imechukuliwa na Jerry Silaha Mbunge wa Ukonga.

View attachment 2733704
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Pia, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja naye ameachwa huku nafasi hiyo ikichukuliwa na Dunstan Kitandula.

View attachment 2733705
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambapo kwa sasa wizara hiyo imegawanywa mara mbili; upande wa Ujenzi Rais Samia amemteua Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri na Uchukuzi amemteua David Kihenzile kuwa Naibu Waziri.

Mabadiliko haya yanatokea ikiwa ni siku 56 tangu afanye mabadiliko madogo katika baraza hilo kwa kuigawa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Ambapo alimteua Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.
Mwakibete ni mzigo hana jipya

Haaminiki tena na wapigakura
 
Kwa nini wale wenye vinasaba na Kanda ya ziwa wanaachwa? Je ni kwa sababu hua ni wazarendo ? Mashimba Ndaki mwenyewe alisha pigwa chini, ila sisi wananchi tunajua watu wa Kanda Ile ni wazarendo na wapiga kazi
Acha ukanda na ukabila wewe ndo aliyewaachia mjomba wenu yule Mwenda zake wewe unataka kuniambia watu wa kanda ya ziwa ndio perfect kuliko kanda nyingine? Na kwa taarifa yako tuko pale nchi hampewi tena hizo ni za ndani yani ile top 3 mtaisikia redioni
 
Mwandosya nilishukuru Mungu kupigwa chini

Alipigania uwanja wa ndege awe tu na nyodo zake apande ndege Dar hadi mbeya au akitoka nje

Uwanja wa ndege ule halikuwa hitaji la wanambeya mbeya kunalimwa sana ndizi, viazi mviringo,mpunga,chai,mbao nk na kuna gesi

Vyote hivyo hakuna kinahitaji ndege vinasafirishwa na magari

Mwandosya naye alikuwa mjinga fulani hivi na u Uproffesa wake

Alitakiwa kupigania kujenga barabara ya katumba hadi Mwakaleli akiwa mbunge

Uwanja wa ndege ule haukutakiwa kuwepo wanapanda tu wafanyabiashara wachache wakinga walioko Mbeya mjini na viofisa vya serikali vichache vya mahakama, bunge na serikali na taasisi Vienda kikazi mbeya kwa gharama za taasisi zao

Kule kinahitajika zaidi barabara sio hilo wanja la ndege la Mwandosya mpenda ndege
Mkuu umemchamba so poa[emoji16][emoji16]
 
Mkristo au muislamu mwenzako anakuletea ugali au bill ya watoto shuleni.

Kila mtu anahangaika familia yake. Uislam au ukristo hautakupa tija yyte kimaisha bila we kupambana na mazingira yako.

Wew Uko Namtumbo anateuliwa mkristo au muislamu wa Muleba mwenya baba na mama na familia yake. Wew kule Namtumbo unafaidika Nini?

Upuuzi upuuzi tu.
Maneno kuntu hayo

Na siku akiteua Muslims wengi uje na slogan hii tena...
 
Baaraza la mawaziri goigoia huwa linabadilishwa kila kila mara ile kufisha ugoigoi wake. Ukiwa rais halafu ukategema kufurahishwa atu fulani kwa kutoa vyeo kwa watoto wao au wao wenyewe, basi hao ndio watakaokuharibia. Spiderman alisema "with great power comes great responsibility".
Mcheza akichemsha unabadilisha namba au unamtoa unaweka mchezaji mwingine yeye kazi aliyojipa ni kubadilisha namba kipa anacheza namba sita mara namba 3 anenda namaba 10 hapo ni akil au matope
 
Mitaa ya dar inachangia pato la taifa kuliko hiyo mwakaleli yako mara mia kadhaa mbele. Kufananisha mwakaleli nakuita mitaa ya dar eti ya wauza maandazi ni ujinga wa kiwango cha juu saana. Mbeya yote kimaingizo haifikii halimashauri moja tu ya dar. Ukibisha tafuta ukweli
Yaani kabisa kuna mandizi pia kibao yanaenda mikoa yote bado barabara serikali haitaki kutengeneza sehemu yenye uchumi mkubwa kama hiyo wanatengenezea barabara mitaani za wauza maandazi na vitumbua wa dar es salaam
 
Atupele Mwakibete halali yake kutemwa hajafanya chochote jimboni kwake

Barabara ya kutoka Katumba hadi mwakaleli taabu tupu wakati hiyo barabara ndiko kunatoka gesi na chai inayoingizia Chi pesa za kigeni kwa wingi

Yaani serikali inavuna pesa kule lakini kutengeneza barabara hawataki na Mwakibete wao
Hiv pale mang'oma bado hawajaweka hata kakipande kadogo ka lami?
 
Angela ni kiongozi msikivu sana tatizo hafikiki kirahisi, anautendaji mzuri mno, lakini kwa sehemu kama wizara ya ardhi yenye watumishi sugu, wezi, matapeli, uchu wa rushwa, bila kutengeneza dawati au muda wa kukutana na malalamiko sugu, ni lazima UONE KANE ZERO.
-DAWATI OVU LA KINONDONI.

Wenyewe wanaita kupiga mbata, yaani "ukizubaa unapigwa tu"
Ndo maana unatakiwa uwe na akili kama za mchwa kukaa hapo ardhi,au uwe untouchable kama January Makamba. Yule mama alivyokuwa waziri kamili ,nikajua hapa hatoweza.
 
Huyu Samia anadanganywa sana na mkwere na ndiye anayempeleka shimoni! Leo ameteua wajumbe wa baraza la mipango, kati ya wanne walioteuliwa wawili walikuwa ndio madalali wakubwa kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya umma!! Ami Mpungwe ndiye dalali makubwa wa makampuni ya makaburu kuja kununua rasilimali zetu kwa bei ya kutupa ikiwemo benki ya NBC, Kilombero Sugar, TBL pamoja na TANZANITE ONE! Mwenzie Omar ISSA ndiye aliyekuwa dalali wa kuwauziua wahindi TTCL ambayo baadae Magufuli alikuja kuinunua upya na kuirudisha serikalini!! Huyu huyu Omar Issa ndio alimletea Mkwere mradi wa mkopo toka World Bank ukiitwa BEST RESULTS NOW ambao alipoingia Ikulu, Magufuli aliufutilia mbali akiuita mradi wa UPIGAJI!!

Sasa hawa madalali ndio Samia ameshauriwa na mkwere awateuwe kwenye tume ya mipango unategemea nini? Ni muendelezo wa upigaji wao wa kifisadi basi.
Mbona unatafuta "scapegoat " mwenye madaraka ni mmoja ambaye amekabidhiwa Jamhuri kwa muujibu wa Katiba yetu. Huyo Mkwere anatoka wapi - au wewe ndio wale wanaamini kwamba Mwanamke hawezi kuwa Mkuu wa nchi lazima kuwa na mwanamume anaye mwongoza kwa "remote control". Hii ni Karne ya 21 - Achana na Mkwere lete hoja zako tuzielewe siyo kuturudisha nyuma kifahamu kama watoto wa chekechea - Mkwere alimaliza kazi yake salama na alikuwa mwanademokrasia kweli kweli, apewe Sifa zake.
 
Barabara ya muhimu sana hii kiuchumi lakini hakuna anayejali. Hata ile ya kwenda Lwangwa. Unakuta gari zimebeba maparachichi zimekwama maparachichi yanaoza. Na hakuna anayejali. Wanachojali kukusanya kodi tu. Naibu waziri mzima angekomalia kupata fungu la kutengeneza hii barabara hasa ukizingatia umuhimu wake kiuchumi asingeshindwa. Mwakibete ni mbunge wangu lakini ni hopeless kabisa huyu jamaa. CCM wakimrudisha tena nitashangaa!
Kama kuna Jimbo ambalo halijatendewa haki kwa nchi nzima ni Jimbo hili la Busokelo kutokana mchango wake kiuchumi.kwa wasilolijua Busokelo ilitoa mchango mkubwa kwa Zao la kahawa tangu uhuru.Baada ya Zao kupotea kwa magonjwa mazao mengine kama chai,parachichi,gas,mbao za stima,viazi, vyote vikitumia barabara ya vumbi hata baada ya Rais magufuli kuahidi kuijenga kwa kiwango Cha lami.Kinachoshangaza baadhi ya majimbo yaliyoanzishwa hivi karibuni yameunganishwa na lami.Unahitaji kuwa malaika kuona ni jambo la kawaida
 
Mbona unatafuta "scapegoat " mwenye madaraka ni mmoja ambaye amekabidhiwa Jamhuri kwa muujibu wa Katiba yetu. Huyo Mkwere anatoka wapi - au wewe ndio wale wanaamini kwamba Mwanamke hawezi kuwa Mkuu wa nchi lazima kuwa na mwanamume anaye mwongoza kwa "remote control". Hii ni Karne ya 21 - Achana na Mkwere lete hoja zako tuzielewe siyo kuturudisha nyuma kifahamu kama watoto wa chekechea - Mkwere alimaliza kazi yake salama na alikuwa mwanademokrasia kweli kweli, apewe Sifa zake.
Mkwere angemaliza kazi yake angejichimbia kwao ""MSOGA" akicheza na wajukuu zake kama alivyochimbia enzi za Magufuli!!! Leo hii Msoga hakukaliki kila leo yupo kisogoni kwa huyu bibi ndio maana anachanganyikiwa!! Ndio maana amemchagulia Samia TISS kachero Mkuu ili aweze kufanya vitu vyake!! He is a devil incarnate.
Mwanademocrasia kwa kuua waandishi wa habari? Mikono yake ina damu ya marehemu Mwangosi ; halafu wewe bwege unamsifia mwanademokrasia!
 
Kabisa

Sijui serikali inawaonaje watu wa kule wajinga,mbwa au kenge au nini? Kwa nini hawapeleki lami ? Pesa zivunwe kule watengeneze barabara kwao au Dar au kusiko na chochote kisa kiongozi mkubwa a

Gesture Mongela aliongea ka clip.fulani akihutubia kuwa Samia amskie aachane na washauri wanaume wanapotosha hadi dunia

Huyo mwanaume aliyeongea Getrude Mongela mpotosha Samia nani? Kikwete au nani?

Gertrude Mwongela hiyo mada I'mo humu jamii forums wiki iliyopita akisisitiza Samia Asikie aachane na wanaume waponaompotosha ila hakutaja hao wanaume wanaompotosha Samia na uzee wake ni akina nani?

Umri wa Raisi Samia ni.wa kupotoshwa na wanaume? Swali aulizwe getrude Mongela
SAMIA ni mwanamke kama Wanawake wengine, kupotoshwa na wanaume ni rahisi sana!! Mtaani tunawaona wanawake wa umri kuzidi yeye na wanadanganywa na watoto wadogo kuliko wao itakuwa hao wa umri wa mkwere?
 
Atupele Mwakibete halali yake kutemwa hajafanya chochote jimboni kwake

Barabara ya kutoka Katumba hadi mwakaleli taabu tupu wakati hiyo barabara ndiko kunatoka gesi na chai inayoingizia Chi pesa za kigeni kwa wingi

Yaani serikali inavuna pesa kule lakini kutengeneza barabara hawataki na Mwakibete wao
Ila ni ka-handsome..laabda amewaongezea nguvu kazi wanyambala??!!!
 
Mwandosya nilishukuru Mungu kupigwa chini

Alipigania uwanja wa ndege awe tu na nyodo zake apande ndege Dar hadi mbeya au akitoka nje

Uwanja wa ndege ule halikuwa hitaji la wanambeya mbeya kunalimwa sana ndizi, viazi mviringo,mpunga,chai,mbao nk na kuna gesi

Vyote hivyo hakuna kinahitaji ndege vinasafirishwa na magari

Mwandosya naye alikuwa mjinga fulani hivi na u Uproffesa wake

Alitakiwa kupigania kujenga barabara ya katumba hadi Mwakaleli akiwa mbunge

Uwanja wa ndege ule haukutakiwa kuwepo wanapanda tu wafanyabiashara wachache wakinga walioko Mbeya mjini na viofisa vya serikali vichache vya mahakama, bunge na serikali na taasisi Vienda kikazi mbeya kwa gharama za taasisi zao

Kule kinahitajika zaidi barabara sio hilo wanja la ndege la Mwandosya mpenda ndege
Na utalii utakuzwa na barabara?
 
SAMIA ni mwanamke kama Wanawake wengine, kupotoshwa na wanaume ni rahisi sana!! Mtaani tunawaona wanawake wa umri kuzidi yeye na wanadanganywa na watoto wadogo kuliko wao itakuwa hao wa umri wa mkwere?
Mkuu Bulesi Hivi ni kweli wanawake ni rahisi kudanganywa hata akiwa ni mwanamke mtu mzima?
 
Back
Top Bottom