Mawaziri waliotemwa katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Agosti 30, 2023 amefanya mabadiliko Baraza la Mawaziri ambapo Waziri mmoja na Manaibu wawili wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wengine.

View attachment 2733703
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula

Miongoni mwa walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ambaye nafasi yake imechukuliwa na Jerry Silaha Mbunge wa Ukonga.

View attachment 2733704
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Pia, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja naye ameachwa huku nafasi hiyo ikichukuliwa na Dunstan Kitandula.

View attachment 2733705
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambapo kwa sasa wizara hiyo imegawanywa mara mbili; upande wa Ujenzi Rais Samia amemteua Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri na Uchukuzi amemteua David Kihenzile kuwa Naibu Waziri.

Mabadiliko haya yanatokea ikiwa ni siku 56 tangu afanye mabadiliko madogo katika baraza hilo kwa kuigawa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Ambapo alimteua Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.
Kwa mwakibete nimefurahi sana kiachwa. ..
 
Baaraza la mawaziri goigoia huwa linabadilishwa kila kila mara ile kufisha ugoigoi wake. Ukiwa rais halafu ukategema kufurahishwa atu fulani kwa kutoa vyeo kwa watoto wao au wao wenyewe, basi hao ndio watakaokuharibia. Spiderman alisema "with great power comes great responsibility".
 
Yule naibu wa Maliasili kwa kweli ni zero kabisa.Kama January tu.Sema Mary na Ms Mabula wana damu ya kunguni.Maana January kabadilishiwq wizara pamoja na kuvurunda.
Angela ni kiongozi msikivu sana tatizo hafikiki kirahisi, anautendaji mzuri mno, lakini kwa sehemu kama wizara ya ardhi yenye watumishi sugu, wezi, matapeli, uchu wa rushwa, bila kutengeneza dawati au muda wa kukutana na malalamiko sugu, ni lazima UONE KANE ZERO.
-DAWATI OVU LA KINONDONI.

Wenyewe wanaita kupiga mbata, yaani "ukizubaa unapigwa tu"
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Agosti 30, 2023 amefanya mabadiliko Baraza la Mawaziri ambapo Waziri mmoja na Manaibu wawili wameachwa na nafasi zao zimechukuliwa na wengine.

View attachment 2733703
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula

Miongoni mwa walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ambaye nafasi yake imechukuliwa na Jerry Silaha Mbunge wa Ukonga.

View attachment 2733704
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Pia, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja naye ameachwa huku nafasi hiyo ikichukuliwa na Dunstan Kitandula.

View attachment 2733705
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ambapo kwa sasa wizara hiyo imegawanywa mara mbili; upande wa Ujenzi Rais Samia amemteua Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri na Uchukuzi amemteua David Kihenzile kuwa Naibu Waziri.

Mabadiliko haya yanatokea ikiwa ni siku 56 tangu afanye mabadiliko madogo katika baraza hilo kwa kuigawa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuunda Wizara tatu; Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Ambapo alimteua Mbunge wa Ubungo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji.

Pia alimteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha.
Yule jamaa aliyepata ajali Dom akiwa na demu kapona kweli?
 
Yaani kabisa kuna mandizi pia kibao yanaenda mikoa yote bado barabara serikali haitaki kutengeneza sehemu yenye uchumi mkubwa kama hiyo wanatengenezea barabara mitaani za wauza maandazi na vitumbua wa dar es salaam
Tatizo Dar ndo kwenye uchumi mkubwa hata hizo ndizi mnazolima ndoto zenu ni kuja Kuuza Dar
 
Sasa
Yaani kabisa kuna mandizi pia kibao yanaenda mikoa yote bado barabara serikali haitaki kutengeneza sehemu yenye uchumi mkubwa kama hiyo wanatengenezea barabara mitaani za wauza maandazi na vitumbua wa dar es salaam
Hapo shida ni Mbunge?!
 
Tatizo sio mawaziri, tatizo ni Watanzania wote wenye kuhitajika kuzalisha serikalini kufanya kazi kwa mazoea pasipo na tija yeyote...

Watu hufurahia tu kupata kazi na wala sio kazi kupata watu...
 
Back
Top Bottom