Mawaziri wapokea taarifa ya wataalam kuhusu mgogoro wa mipaka ya kiutawala na msitu wa Kazimzumbwi

Mawaziri wapokea taarifa ya wataalam kuhusu mgogoro wa mipaka ya kiutawala na msitu wa Kazimzumbwi

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
IMG-20261003-WA0018.jpg
Timu ya Wataalam iliyoundwa kwa ajili ya kuchambua hoja za wananchi kuhusu mgogoro wa muda mrefu wa mipaka ya kiutawala na mpaka wa Msitu wa Kazimzumbwi, imewasilisha taarifa ya uchambuzi wa hoja zaidi ya 60 zilizowasilishwa na wananchi 22 kwa Mawaziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Timu hiyo inaundwa na Mkurugenzi anayeshughulikia Mipango Miji na Vijiji wa OWM–TAMISEMI, Kamishna wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara hiyo pamoja na Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
photo_2026-10-03_20-04-51.jpg
photo_2026-10-03_20-04-36.jpg
Taarifa hiyo imewasilishwa Oktoba 2, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa Septemba 23, 2026 na Waziri wa Nchi, OWM–TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, wakati wa mkutano wa Mawaziri hao watatu na wananchi uliofanyika katika Viwanja vya Chanika Zingiziwa kwa lengo la kusikiliza na kuchambua hoja zao.
photo_2026-10-03_20-04-33.jpg
Mkutano huo ulikuwa sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, aliyoyatoa Septemba 18, 2026 akiwa Dampo la Pugu, akiwataka Mawaziri hao watatu kukutana na wananchi ndani ya siku saba kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa mipaka ya kiutawala.

Na: OWM–TAMISEMI, Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom