Mawazo yanahitajika kuhusu Uncle kulala na mtoto chumba kimoja

Kinyume na alivyofanya yeye kumchana mgeni eti dunia imechange,dah kazingua ssna

Kumwambia mgeni Dunia imebadilika amefeli sana,,,, hakuna Busara ya namna hio.. unamfanya mgeni ni mtuhumiwa tayari.
Ujue dunia ya sasa imekuwa ngumu sana,, Zamani watu walikuwa wanafurahia wageni lakini leo ugeni imekuwa kero kwa wengi...

Option ya kulala sebuleni ilikuwa the best na familia zetu wengi, watoto tumeshawai kulala sebuleni ili wageni walale vyumbani.. (ni kawaida sana kwa jamii yetu).

Kizazi cha sasa hata ukienda kwa mtu ghafla utaonekana unamaliza Ugali hehehehehe.. Sijui ni kizazi cha hovyo au ndio wakati umetaka mabo yaende hvyo.

Niishie hapo...
 
Angelilala ukumbini mwenye nyumba huwenda huyu mgeni angeona haya kwamba anawabana angeondoka mwenyewe.
 
Mkuu kwanza huo ujasiri wa kumruhusu alale chumba cha watoto uliutoa wapi????
Aiseeee watu hampo serious kiasi hiki!!!
 
Ww endelea kumlea mpka akamilishe anachokitaka alafu uje uandike uzi mwingine.

Ila sisi watanzania muda mwingine sijui tupoje!! Unaona kabsa mtu anapoishi panatosha yeye na familiar yake tu na hapaitaji wageni wa kulala ila bado unaenda! Hizi tabia za kipumbavu sana
 
Mfukuze haraka Sana huyo
 
Uko sahihi.
Mtu mzima tena wa kiume kulala na watoto iwe wa kike au wa kiume,,sio jambo zuri,,

Lakin pia njia iliotumika kutatua tatizo kama ulivoeleza sio njia ya busara,,

Wangelala na mtoto chumbani ,,mgenini akalala peke yake kwenye chumba cha watoto_ a very simple solution

Mtoa maada ametumia nguvu kubwa saana kutatua tatizo dogo

Mtoa maada anaweza kua kweli ameshinda lakini hebu ajalibu kuvaa viatu vya mgeni wake,,kama angekuwa yeye angehisije tena unaambiwa kabisa kuwa "uenaenda kulala gest kwa sababu sikuamini kulala na watoto wangu,,"

Lazima kama mtu mzima ujisikie vibaya.
 
Mkuu uko sahihi,,

Uamuzi alioufanya haukuwa wa busara
 
Wow hongera mkuu uamuzi mzuri Sana yaani suala la mtu mzimakulala chumba kimoja na mtoto usirudie kabisa kesi za unyanyasaji wa watoto zimekua nyingi Sana na takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya watoto wanaofanyiwa ukatili wa kingono wanaofanyiwa na watu wao wa karibu(wanafamilia).Malezi ya watoto kipindi hiki ni magumu Sana Mungu awasaidie wazazi wote.
 
Walimwengu roho zimetugeuka, heri nusu shari!
Akija tena mkaribishe, usiku apate dinner baada ya hapo nyumba ya kulala wageni...baaasi!
 
Huna akili wewe!! Umevunja mahusiano mazuri na anko wako kwa akili za kuambiwa. Hujui kesho kama utakuwa umelala mauti ni nani atakulelea watoto wako. Labda huyo ulie mnyapaa kwa kumpeleka gest ya kunguni ndo anaweza kuwa msaada kwa wanao.

Hivi unawezaje na unaanzaje kumpeleka ndugu yako gest ili hali una pa kumlaza. Huo ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana.

Umeshindwa nn kulala na mwanao mgeni ajihifadhi kwa hiyo siku moja au hata ingekuwa wiki kuna ubaya gani. Naweza kusema pia ww ni mchoyo umemfukuza kijanja.

Kingine nyie watu wa mjini acheni uzungu majitaka. Mbona mkija huku vijijini kwetu tunawakarim vizuri tu na nyumba hizi hizi za vyumba na sebule na wakati mwingine tunawapa hata magodoro yetu na wake zetu sisi tunabaki tumelalia mbavu za umbwa!?
 
Katu sitoruhusu mtu yeyote kulala na wanangu, hao wageni wakalale lodge huko, dunia imebadilika sana.
 
Jamaa ametumia hisia badala ya akili,,,anasahau kuwa kuna kesho.

Tena kibaya sana amemwambia wazi kabisa hamuamini kulala na watoto wake,

Yes,it is good usimuamini mtu,,lakini kulikuwa na ulazima gani wa kumwambia hili,,

Kama ingeshindikana kabisa kulala kwake basi angetafta excuse ya busara alafu angempeleka mgeni wake guest,,
Hii ya kumuhukumu Mtu kwa hisia ni mbaya sana,,sio kila mtu ni mbaya,

Kitachomuumiza mgeni wake sana sio kulala gyest,,ila ni sababu iliyofanya apelekwe guest,
 

πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½
Copy na paste mrejesho post yako #1 chini ya uliyoandika..
Butua edit..
 
Upo sahihi kabisa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…