Mazishi ya Queen yamewageuza viongozi wetu Afrika kuwa watoto wa shule

Mazishi ya Queen yamewageuza viongozi wetu Afrika kuwa watoto wa shule

Mimi naona sababu iliyowafanya wasafirishwe kwa basi ni kuwa baadhi yao hawakuchaguliwa na wananchi.
 
si ndio watoto wa shule wanavyolindwa bwenini hivyo? mbona akina Biden, Macron, etc haikuwa vile?
Hadhi ya mataifa yao imewabeba hivyo lazima wapewe 'special privilege'...hakuna tatizo hapo.
 
Kwani kuna shida gani? Huwa wanjikweza tu wakiwa hapa lakini ni wa kawaida sana! Mimi nawaangalia wale mabodigadi wao kuna mbinti mmoja yule kipepeo huwa anatembea kwa kutanua mikono hatari lakini huko mbona amenywea? Kumbe inawezekana kabisa marais kutembea bila walinzi!!😁😁😂😂😂
wakoloni sio mchezo, hawana utani.
 
Waafrika tujifunze hiyo ndiyo namna ya kuishi!
Wewe ulitaka kila mmoja aandaliwe Landcuizer V8?
Màisha hayo ndiyo yanayoendelea kutuumiza hapa kwetu
Mbunge umpe V8 la mkopo bila kodi
Mamilioni ya shilingi kila siku,kila mwezi,
Matibabu bima
Pesa ya mafuta nk
Saa ngapi atakutetea wewe mwananchi?
Huo waliopanda ni usafiri tu si walifika?kuna video clip ilimuonyesha waziri mkuu wa Sweden akienda ofisini na baiskeli je ungeiona hii si ungezimia wewe?
Huku kwetu nani kiongozi ataweza angalau siku moja aende ofisini na mwendo kasi au bodaboda?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Sijaona umuhimu wa kwenda huko, salamu za rambirambi zingetosha kabisa, sio kwasabau ya kupanda hilo basi ila kwa sababu ya kutoonekana umuhimu wao huko.
wakoloni wamewakomesha! kupata mwaliko sio kwamba umeambiwa lazima uje. Ni kawaida unapomkuta mtu anakula chakula kukaribisha kwa kukwambia karibu chakula hata kama hamaanishi ule na share yako haikuwepo pale maana haukuwepo wakati chakula kinapikwa. Hivyo sio kila karibu chakula lazima uende kula huku ukijua share yako haipo pale. Waingereza walialika watu wote kama formality tu lakini hawakumaanisha kuwa watu waote waende kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuhudumia watu wote kwa hadhi zao. Wengine tungebaki kwenye runginga tu,
 
Waafrika tujifunze hiyo ndiyo namna ya kuishi!
Wewe ulitaka kila mmoja aandaliwe Landcuizer V8?
Màisha hayo ndiyo yanayoendelea kutuumiza hapa kwetu
Mbunge umpe V8 la mkopo bila kodi
Mamilioni ya shilingi kila siku,kila mwezi,
Matibabu bima
Pesa ya mafuta nk
Saa ngapi atakutetea wewe mwananchi?
Huo waliopanda ni usafiri tu si walifika?kuna video clip ilimuonyesha waziri mkuu wa Sweden akienda ofisini na baiskeli je ungeiona hii si ungezimia wewe?
Huku kwetu nani kiongozi ataweza angalau siku moja aende ofisini na mwendo kasi au bodaboda?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa, viongozi wetu wanatakiwa wa "think globally and act locally" walipaswa kulichukua hili somo la kubana matumizi walilopewa na wazungu warudi nalo nyumbani na ku practice. Wanatakiwa wajue kwamba kumbe mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kutumia bus au kuwekwa wote kwenye coaster/mini bus moja kusafiri kutoka dar es salaam kwenda Dodoma kwenye mkutano na kurudi. Siku moja nilikuwa pale Kigurunyembe Morogoro kulikuwa kuna mkutano unaowataka wakurugenzi wotewa wila kuhudhuria, chaajabu kila Mkurugenzi wa wilaya kwenye mkoa mmoja amekwenda pale kwenye mkutano na Landcruiser yake na dereva, nikajiuliza ni kwanini Mkurugenzi wa handeni, Korogwe, Lushoto, pangani, tanga mjini, Kilindi, handeni vijijini, Muheza wasingekutana wote pale Mkata na kusafiri kwenye coaster moja kuelekea Morogoro na kuaacha magari yao pale mkata ili kubana matumizi?
 
Sasa watu wanatoa mikopo kwetu kila siku, madeni kibaooo wanatudai, sisi umuhimu wetu nn kwao ? Zaidi labda tuwaibie tu
Wanatoa mikopo na misaada kwetu, lakini wanashangaa kuwaona viongozi wetu wanajenga majumba makubwa ya kifahari, wana magari makubwa ya kifahari, wanapeana mabenz kwenye birthday za wastaafu wao, wanasomesha watoto na ndugu zao shule ghali za ulaya na marekani na wana pesa nyingi kwenye mabenki ya ndani na nje ya nchi. Sasa wajiuliza na kujilaumu kwanini wanalia njaa kwetu na kwanini tuwape? Wanaona kuwa hela zao ndizo wanazotumia kujenga majumba hayo na maisha mengine ya juu ambayo wao hawana.
 
Hadhi waliopewa viongozi wetu wa Afrika kwenye mazishi ya Queen sikuyapenda hata mimi, kama watoto wa shule vilee!! wamefuata nini cha mno? ona usafiri walipewa tofauti kabisa na wengine. Nani katuroga? njaa au nini? usipokwenda watakufanya nini?

View attachment 2362652

View attachment 2362653
Wewe hapo ukienda kwenye msiba hadi chini unakaa na kwako una sofa na msosi ukitengewa unakula kwa sinia sometimes bila hata kunawa alafu unataka Viongozi wetu ndio wapeleke tambo hadi msibani?
 
Wewe hapo ukienda kwenye msiba hadi chini unakaa na kwako una sofa na msosi ukitengewa unakula kwa sinia sometimes bila hata kunawa alafu unataka Viongozi wetu ndio wapeleke tambo hadi msibani?
weee acha izo, hata pale kwenye msimba wa rais wetu JPM hakukua na kiongozi mkuu wa nchi fulani aliyekaa kwenye jamvi eti kwasababu ni msibani. Tofautisha kati ya mtu binafsi na Rais wa nchi, wee veepe!! tembo hata akonde vipi hawi sugura.
 
Waafrica mna shida wangeenda na misafara mngesema kodi zetu sasa hivi wameharauliwa
Sisi tusingeshangaa kama kwenye ule usafiri tungewaona na marais wazungu wamo, shida yetu ni kuwaona viongozi wetu wakipumuliana wenyewe kwa wenyewe tu kwenye basi na wazungu akina Biden twawaoga wakiwa kwenye bullet proof zao na misafara yao.
 
Maraisi wetu wa mchongo
Hebu muone Ruto anakenua tu, kaapishwa juzi tu hata serikali hajaunda, lakini ona huyoooo UK na rundo la Per dieum (posho). Juzi juzi tu aliwaambia serikali haina fedha anataka kubana matumizi, kumbe anazuga tu, huyooo UK na akitoka UK huyooooo USA kwenye mkutano. Afadhali hata Rais wetu katuma mwakilishi huko New York
 
Kilichowafanya wafanywe vile kule ni vitu vifuatavyo:

1. Demokrasia: Wazungu wanafahamu kuwa viongozi wa Afrika wameiba kura kupata urais, hakuna demokrasia

2. Mahakama: Wanafahamu kuwa Afrika hakuna utawala wa sheria na mahakama haziko huru.
3. Wizi: Wanafahamu kuwa viongozi wa kiafrika ni wezi tu kama wezi wengine, wanaibia watu wao wenyewe na kwenda kuficha ulaya na marekani, wanajisikia kichefuchevu kuwatazama.
4. Msimano: Hawaeleweki, hawana msimamo kwenye maswala ya kimataifa, eti hawafungamani na upande wowote. Duniani hakuna kitu kama hiko, hata bibilia inakataa watu kuwa vuguvugu.
5. Ombaomba: Wanaomba mno, hapo wanafahamu kuwa kuja kwao kwenye msiba ni kisingizio tu, lakini wamekuja kuomba hiki na kile, hili na lile kutoka kwa viongozi wakizungu waliochaguliwa kidemokrasia kwelikweli na watu wao watakaokwenda kuhudhuria mazishi. Yaani wameficha mabakuli yao kwenye vilemba na kanzu zao. Hawakusanyi kodi huko kwao wanataka kupewa tu za walipakodi wa kizungu,
Ati walipanda school bus? Jaman wabongo hawafai huko mitandaoni
 
Back
Top Bottom