Mazishi ya Queen yamewageuza viongozi wetu Afrika kuwa watoto wa shule

Mazishi ya Queen yamewageuza viongozi wetu Afrika kuwa watoto wa shule

SAsa kwa akili ya kawaida tu nani ana shida na raisi yeyeto wa kiafrica, ana impact gani duniani. Tofauti na raisi wa USA Wana maadui wengi na hatari yeyeto mda wowote.
 
Bideni akiuwa itapelekea vita vya tatu vya duniani tofauti na raisi wa kiafrica ataombolezwa na wananchi wake tu.
 
Ishu kuu ni usalama na wala Hakuna kingine. Kati ya Bideni na maraisi wa kiafrica nani yupo kwenye risk zaidi
 
  • Wakija kwao nao wawe wanapanda mabasi.
  • Kwenye basi, situ ya kwanza ni ya Raisi, viongozi wafuate kadiri ya protokali.
  • Wamezidi kujikweza mno mbele wananchi wao walio dhoofu mbaya kiafya na kiuchumi.
 
SAsa kwa akili ya kawaida tu nani ana shida na raisi yeyeto wa kiafrica, ana impact gani duniani. Tofauti na raisi wa USA Wana maadui wengi na hatari yeyeto mda wowote.
Sasa kama marais wetu hawana uadui wowote hii misururu mirefu ya magari na walinzi kwetu na kufunga barabara ni ya nini? inayokula kodi na tozo zetu? Kwanini kule ulaya unasema hakuna maadui wao lakini nyumbani wana maadui hivyo wana hitaji ulinzi mkali? eleza kidogo tukuelewe
 
Ishu kuu ni usalama na wala Hakuna kingine. Kati ya Bideni na maraisi wa kiafrica nani yupo kwenye risk zaidi
kwahiyo huko kwao Afrika ndio wana maadui wengi kuliko ulaya? wanawafanya nini wananchi wao kiasi cha kuhitaji misululu ya walinzi na kufunga barabara?
 
Kweli bongo kazi zimeadimika.......maana ukiangalia utakataka wa hoja zilizong'ang'aniwa na watu wazima, tena maGT!!! Vile wanafuraaahi wenyewe kwa hoja zao hizo, unapata jibu la wazi kuwa kuna tatizo mahali.
Serikali ifanye jambo kuhusu ajira maana hali hii ikiendelea haki ya nani tutawakuta watu wazima humu wanacheza mdako au kuruka mkuta (kamba) au kidali po! Mark my words......maana vihoja hivi vya kuokoteza mwishowe vitaisha au kuwachosha hata hao wazushaji.
 
kwahiyo huko kwao Afrika ndio wana maadui wengi kuliko ulaya? wanawafanya nini wananchi wao kiasi cha kuhitaji misululu ya walinzi na kufunga barabara?
Hao ndio wababe wa duniani,usakwa na magaidi na KILA aina ya maadui
 
Sasa kama marais wetu hawana uadui wowote hii misururu mirefu ya magari na walinzi kwetu na kufunga barabara ni ya nini? inayokula kodi na tozo zetu? Kwanini kule ulaya unasema hakuna maadui wao lakini nyumbani wana maadui hivyo wana hitaji ulinzi mkali? eleza kidogo tukuelewe
Kwetu huku misururu ni swaga SAwa na harmonize au diamond kutembea na lundo la walinzi ni swaga tu na sio uhatarishi wowote.
Pia misururu ndio sehemu pia ya kupigia pesa zetu misururu ni biashara unaweza kuta Waziri anaenda kutazama ufisadi wa milioni 10 lakini anatumia gharama ya mafuta,posho na taka taka zingine kwa 30.
Wao uongozi ni wito wa kuwatumikia walipa kodi thus Wana msamiati wa kujiuzuru, kwetu uongozi ni ajira binafsi kwa maslai binafsi na sio wito wa kuwatumikia walipa kodi thus Hakuna msamiati wa kujiuzuru.
 
Hadhi waliopewa viongozi wetu wa Afrika kwenye mazishi ya Queen sikuyapenda hata mimi, kama watoto wa shule vilee!! wamefuata nini cha mno? ona usafiri walipewa tofauti kabisa na wengine. Nani katuroga? njaa au nini? usipokwenda watakufanya nini?

View attachment 2362652

View attachment 2362653
Wamefunzwa matumizi bora ya pesa ya umma. Itashangaza wakirudi waendeleze ujinga wa safari zenye misafara ya magari 70 na helicopter 2 angani.
 
Wamefunzwa matumizi bora ya pesa ya umma. Itashangaza wakirudi waendeleze ujinga wa safari zenye misafara ya magari 70 na helicopter 2 angani.
Wamekomeshwa, mtu kaiba kura halafu anajiapisha kuwa Rais sawa na Macron, Biden na wengine waliochaguliwa kidemokrasia. Rais anashindwa hata kuwalisha watu wake, wanashindwa hata kupanga na kusafisha miji Yao.
 
Ukisikiliza hotuba za viongozi wetu wa Afrika kwenye mkuto wa Umoja wa mataifa, UNGA kule New York, wanalalama badala ya ya kuwasilisha hoja konki kutoka Africa. Wanalia njaa wana ardhi kubwa za kilimo na maji mengi ya mito na, maziwa yanayotiririsha maji yote baharini. Wanashindwa kuwapatia watu wao hata maji ya kunywa, Wanalalamikia chakula kutoka Ukraine, shame on them.
 
Back
Top Bottom