Mbaroni kwa kusambaza uzushi Mtandaoni kwamba Rais Magufuli ni Mgonjwa. Kigogo wa Twitter naye anasakwa
Huyo jamaa nadhani hajielewi humu kishawasilianaa na watu wengi kuhusu business, lakini hapo naona anatukana matusi yote bila sababu zozote. Hakuna justification ya kutukana.
Ngoja tuone pengine anaweza kuonewa huruma akaachwa
Kwani mnaogopa nini? Hapa tutaenda sawa kama kuna mtu kinamuuma na akazikwe
 
Kigogo ni watu kama 72 na wapo katika nchi 8. Aanzie hapo
Ni kweli watumiaji wa utambulisho wa kigogo2014 ni wengi lakini IP address ya mtumaji ujumbe husika ni UNIQUE kwa maana ya kwamba mtumiaji mtandao kwa njia yoyote ya mfumo wa kitakirishi (kompyuta) IPv4 Protocol na atakayelengwa ni mmoja tu kati ya hao 72 uliowataja sijui ulifanya sensa yao lini na kubainisha ni nani na ni hata hivyo wewe ni shahidi mwongozaji mzuri utalindwa tu kwa taarifa zako za uhakika zinazopelekea mtuhumiwa kukamatwa ili ajibu tuhuma zake katika vyombo vya sheria.
 
Uonevu tu wa wazi wazi......kwan mtu kusema mtu anaumwa ni kosa siku hz....kwa kifungu kipi cha Sheria?
 
Unajua Leo nimeshangaa Sana watu ambao tumekuwa tukiwasiliana kuhusu biashara na maneno wanayoyatoa. Lakini pia nawaza Kama unataka kufanya hayo yote why unaji-engage kwenye business Tena na id ileile?
Anyway
Kama unataka kuwachomesha wamekurahisishia kazi boss taarifa zao unazo zipeleke kituo kilicho karibu na wewe kwanini unahangaika huku mtandaoni Kama inakukera.
 
Hii ni strategic move,kumtumia kama Chambo kuwatisha wanaomuongelea Magufuli....kama kukamata mbona hata humu kaongelewa sana kuumwa kwake?? watakamata wangapi?
 
Kuugua kwa Mwanadamu ni jambo la kawaida , na asilimia kubwa ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50 wanaugua jambo moja au mawili ......namna pekee ya kudhibitisha kuwa huyo magufuli sio mgonjwa ni yeye kutoka hadharani kuweka vipimo vya afya yake hadharani ili kudhibitisha kuwa huyo Majura ni muongo .....tofauti na hapo ni kupoteza muda kumshitaki
 
hongera kwa Jeshi la polisi Mkoa wa kinondoni,
tunaomba wazushi wote wakamatwe kwa kushirikiana na TCRA.

lkn pia wapo baadhi ya viongozi wa upinzani ambao wamejitokeza hadharani na kushadadia habari za uzushi pia wakamatwe ili iwe fundisho kushabikia na kucho chochea taharuki kwa wananchi wasio jua lolote.
Una uhakika ni uzushi mkuu, yawezekana kinyume chake ndio ukawa uzushi
 
Siku sio nyingi kulike, kukomenti au kufollow page ya kigogo litakua kosa kisheria na utakamatwa utupwe jela.
 
Back
Top Bottom