Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgonjwa.
Pia , Kingai amesema wanamsaka mwanaharakati anayejiita Kigogo katika mtandao wa Twitter, kwa tuhuma za kuzusha hofu na uongo kwamba Rais John Magufuli anaumwa.
Mimi ninamwomba Rais Magufuli na serikali yake kuwa wasitafute makosa kwa watu wengine bali ingekuwa busara kama yeye Rais na wasaidizi au watendaji wake wangejiuliza au kujitathmin wao wenyewe kuwa wamefanya makosa gani, mpaka hao watu au huyo kigogo akapata nafasi ya kujitutumua hivyo kwa kuleta uongo mitandaoni?
Nashangaa kwanini toka tusikie hizi tetesi za
kupotea kwake kutoka kwa hao waropokaji wa dunia wasioitakia mema Tanzania na watanzania kwa ujumla mpaka hii leo Rais Magufuli, kama bado yuko salama huko aliko, ameshindwa kupost hata clip moja, akawasalimia watanzania na kuwahakikishia kuwa yeye yu mzima na salama wa salmin?
Yeye na serikali yake wanavyo endelea kukaa kimya namna hiyo ina malengo gani kwetu sisi wapenzi wake?
Nachopenda kusisitiza kwa Rais wetu na watendaji wako wa serikali ni kwamba naomba utambue kuwa wewe sio tu Rais na kipenzi cha watanzania peke yetu, bali ni Rais na kipenzi cha wananchi wengi wa ulimwengu pia utake usitake. Matendo yako na ujasiri wako katika kipindi hiki kifupi cha muhula wako wa kwanza yametokea kuyapendeza wananchi wengi ulimwenguni hasa waafrika popote pale walipo duniani. Zaidi ya hayo wewe umekuwa matumaini yao na msemaji wao katika mapambano dhidi ya mabeberu.
Kwa hali hiyo nipende tu kukueleza kuwa usifikiri kukaa kwako kimya ni sifa. Kwa watu wengi ambao wewe ni matumaini yao kama nilivyo dokeza hapo juu ni kwamba kuto kujitokeza kwako kunatufanya sisi wazalendo wa nchi yetu Tanzanaia na wafuasi wako tuwe na mashaka na wasiwasi mkubwa. Usiku hatulali vizuri tuna kuwa na msongo wa mawazo kuhusu maisha yako na hali ya maisha ya watanzania na maendeleo yetu bila wewe itakuwaje?
Rais Magufuli naomba utambue kuwa wewe katika karne hii ya 21 mpaka sasa, sijui huko baadae, ni Star wa waafrika and you are more than akina Nyerere na akina Lumumba, kwa mtazamo wangu. Chochote kitakacho semwa kuhusu wewe basi ujue kuwa ulimwengu mzima utapata habari. Wewe kwenye ulimwengu uko kwenye Level ya akina Trump kiumaushuhuri.
Nitoe mfano kuhusu hii nchi ambayo ninanishi, kuna Magazine moja kwa jina la "SPIEGEL", hii Magazine ni kama TIMES na NEWS WEEK au SUN ya nchi tunazo zijua. Ni jarida ambalo linaheshimika sana Ujerumani na lina wasomi wengi ambao ni prominent kama akina Angela Merkel na wengineo. Sasa jarida kama hili likiandika mambo yoyote yale kuhusu wewe, yawe mabaya au mazuri, basi elewa kuwa you must be somebody to fear or to love.
Kwa bahati nzuri wewe kwa wazalendo wengi kama mimi nakupa BIG UP kutoka moyoni, lakini kwa wasaliti wachache wakiwemo wa-caucasian ni tishio kwao.
Kwa hali hiyo nakuomba chonde chonde Rais wetu tuondoe mashaka kwa kujitokeza kwa chochote kile. Kukaa kwako kimya hakutupi sisi wafusi wako faraja na amani, kunatufanya sisi tunyong'onyee sana na hivyo pia katika hili janga la COVID-19, tuweze kupungukiwa na immunity yetu na kuwa vulnerabe kwa CORONAVIRUS.
Wewe mwenyewe kila wakati unaimba wimbo wa kutaka sisi tusiwe na hofu, lakini hofu ya maisha yako ambayo wewe mwenyewe unasababisha kwa ukimya wako, hiyo huioni, isipokuwa hofu ambayo inasababishwa na CORONAVIRUS ndiyo unayoiona.
Hiyo ni double standard Rais wangu, huwezi ukatufanyia ubaya hivyo. Sisi tukiiona sura yako tu ni amani tosha.
Wewe ni ICON yetu sisi wanyonge na wazalendo wa nchi yetu na Race yetu. Wewe ni mpambanaji wa rasilimali zetu kwa maslahi yetu na ya waafrika wote kwa ujumla na pia uafrika wetu kwa hivi sasa kuliko Rais mwingine yeyote yule Afrika. Wewe ni mtetezi wa Race yetu dhidi ya Caucasians. Kwa hali hii tafadhali usifanye utani na maisha na afya yako!
Nakuombea maisha mema marefu na baraka nyingi zenye upendo kwa Mungu wetu wa Mbinguni!