Mbaroni kwa kusambaza uzushi Mtandaoni kwamba Rais Magufuli ni Mgonjwa. Kigogo wa Twitter naye anasakwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgonjwa.

Pia , Kingai amesema wanamsaka mwanaharakati anayejiita Kigogo katika mtandao wa Twitter, kwa tuhuma za kuzusha hofu na uongo kwamba Rais John Magufuli anaumwa.
Wanatisha watu tu. Huyo Charles majura ukute wamepanga naye njama. Ili mradi tu kuogopesha watu.
 
Japo sio kitu kizuri kufurahia kifo au matatizo ya mwengine.Lakini kinachonishangaza sana hili jambo kufichwa kama kwamba kuumwa ni dhambi sijui ni sababu za kiusalama au ni nini
Tatizo mnachukulia tittle ya u rais,Kama ujumbe wa nyumba kumi kumi.
 
Tusishabikie Uovu. Hii kitu inaweza kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kiongozi mkuu wa chama unapofurahia mabaya kwa Rais wa nchi siyo jambo jema hata kidogo. Kumbuka kuwa huyo unayemtabiria mabaya ana washabiki na wapenzi wa chama chake hata wasiyokuwa na chama. Angalia Burundi na Rwanda, Somalia, Iraq, Libya etc.
 
hongera kwa Jeshi la polisi Mkoa wa kinondoni,
tunaomba wazushi wote wakamatwe kwa kushirikiana na TCRA.

lkn pia wapo baadhi ya viongozi wa upinzani ambao wamejitokeza hadharani na kushadadia habari za uzushi pia wakamatwe ili iwe fundisho kushabikia na kucho chochea taharuki kwa wananchi wasio jua lolote.
 
Back
Top Bottom