Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Mbeya: Mdude Nyagali aachiwa huru na Mahakama baada kutotiwa hatiani katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya

Sasa mahakama za ccm si ndio hizo zimeona ziachane nae baada ya kuona hana ishu tena?

Wapi ww, dhalimu ndio alikuwa anaendesha siasa za kidhalimu, na sasa hayupo haki imerejea nchini.
 
Bila katiba mpya ipo siku atakuja jiwe mwingine na atadumu muda mrefu sana.
Itakuwa kilio mara mbili.
Exactly, maana i wazi kuwa mtu (rais) ana nguvu kuliko vyombo vyote vinavyoifanya nchi iitwe taifa hivyo kama atakuwa na akili kama za jiwe au Kim Jong ill raia ndio wanaomia.
Suluhisho ni katiba mpya yenye kwendana na uhalisia wa mazingira ya sasa, yenye kumwajibisha kiongozi kwa wananchi na si mamlaka za juu kama wao wanavyotuambia sasa kuwa baya lililotokea ilikuwa ni kutii mamlaka za juu.
 
Wapi ww, dhalimu ndio alikuwa anaendesha siasa za kidhalimu, na sasa hayupo haki imerejea nchini.
Si ndio maana huwa nakwambia sasa tuko vizuri? Mambo ni super.

Haki kila kona,! Hata 2025 mnaenda ikulu kama kimbunga maana aliekuwa anawanyima haki hiyo kafariki!

Makofi kwa mama tafadhaliiiii
 
Natoa wito huu kwa Serikali ya awamu ya 6, kwamba wote walioshiriki kumtesa Mdude ambao bila shaka wanafahamika , wakamatwe haraka sana na kushitakiwa Mahakamani

Ni muhimu sana kwa Chalamila na kundi lake akiwemo RPC wa Songwe na RPC wa Mbeya , Biswalo Mganga (mnyororo ni mrefu) wakamatwe na kushitakiwa ili kuimarisha utawala wa sheria nchini Tanzania, ni muhimu watu hawa kukamatwa ili kuepusha wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa lengo la kulipa kisasi.
Ni wakati wa kusamehe, kusahau na kusonga mbele ndugu yangu.
 
Si ndio maana huwa nakwambia sasa tuko vizuri? Mambo ni super.

Haki kila kona,! Hata 2025 mnaenda ikulu kama kimbunga maana aliekuwa anawanyima haki hiyo kafariki!

Makofi kwa mama tafadhaliiiii

Kwenda ikulu sio lazima, bali tunaongelea mazingira sahihi na ya haki ya kwenda ikulu. Somo ndio hilo dogo.
 
Kwenda ikulu sio lazima, bali tunaongelea mazingira sahihi na ya haki ya kwenda ikulu. Somo ndio hilo dogo.
Sasa si ndio yapo sasa hivi baada ya aliekuwa anayazuia kufariki?
 
Kwa hali hii hivi Magufuli huko aliko ana waongoza malaika kweli au anawaongoza mashetani wenzake?.
 
Back
Top Bottom