Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Kitongoji cha kibumbe, kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya mke, mume na watoto wawili wakutwa wamefariki ndani ya nyumba na miili yao ikiwa imeharibika.
Mdogo wa marehemu (mke) kutoka Mbeya Mjini alisema zaidi ya wiki moja alikosa mawasiliano na familia hiyo ambao wote ni walimu, hivyo ikawalazimu kwenda kujua kuna nini sababu haikuwa kawaida kukaa bila kuwasiliana na dada yake.
Walivyofika walikuta milango yote imefungwa ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji. Anasema walifanikiwa kuingia ndani na kukuta miili hiyo ikiwa imeharibika, ikiwa pamoja na mapanga, nyundo na sumu (madawa ya kumwagilia kwenye mboga).
Kijana huyo anasema walivyofika walipata harufu kutoka ndani ya nyumba hiyo, walipoenda polisi walipewa ruhusa ya kuvunja mlango na kukutana na jambo hilo la kutisha.
Anasema kabla ya mauaji kulikua na mgogoro wa familia kati ya wanandoa hao.