Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

View attachment 2356124

Kitongoji cha kibumbe, kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya mke, mume na watoto wawili wakutwa wamefariki ndani ya nyumba na miili yao ikiwa imeharibika.

Mdogo wa marehemu (mke) kutoka Mbeya Mjini alisema zaidi ya wiki moja alikosa mawasiliano na familia hiyo ambao wote ni walimu, hivyo ikawalazimu kwenda kujua kuna nini sababu haikuwa kawaida kukaa bila kuwasiliana na dada yake.

Walivyofika walikuta milango yote imefungwa ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji. Anasema walifanikiwa kuingia ndani na kukuta miili hiyo ikiwa imeharibika, ikiwa pamoja na mapanga, nyundo na sumu (madawa ya kumwagilia kwenye mboga).

Kijana huyo anasema walivyofika walipata harufu kutoka ndani ya nyumba hiyo, walipoenda polisi walipewa ruhusa ya kuvunja mlango na kukutana na jambo hilo la kutisha.

Anasema kabla ya mauaji kulikua na mgogoro wa familia kati ya wanandoa hao.
Shida ya ndoa za mwanaume na mwanamke wote waajiriwa hua zina migogoro sana. Nilishasema na nitasema tena mke apaswa kukaa nyumbani wakiwa na vijiajira hua wanakua natdharau, na dhihaka za mwendo kasi.

Kufikia kuua mke na watoto huyo mwanaume yalimfika hapa. NIONYESHE MWANAMKE MWENYE AJIRA ALIE MNYENYEKEVU KWA MUME WAKE NA MIMI NITAKUONYESHA MBUZI ANAETAGA MAYAI.
 
Back
Top Bottom