Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

View attachment 2356124

Kitongoji cha kibumbe, kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya mke, mume na watoto wawili wakutwa wamefariki ndani ya nyumba na miili yao ikiwa imeharibika.

Mdogo wa marehemu (mke) kutoka Mbeya Mjini alisema zaidi ya wiki moja alikosa mawasiliano na familia hiyo ambao wote ni walimu, hivyo ikawalazimu kwenda kujua kuna nini sababu haikuwa kawaida kukaa bila kuwasiliana na dada yake.

Walivyofika walikuta milango yote imefungwa ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji. Anasema walifanikiwa kuingia ndani na kukuta miili hiyo ikiwa imeharibika, ikiwa pamoja na mapanga, nyundo na sumu (madawa ya kumwagilia kwenye mboga).

Kijana huyo anasema walivyofika walipata harufu kutoka ndani ya nyumba hiyo, walipoenda polisi walipewa ruhusa ya kuvunja mlango na kukutana na jambo hilo la kutisha.

Anasema kabla ya mauaji kulikua na mgogoro wa familia kati ya wanandoa hao.
Hao ndo wanaume kama mabinti, cheki na lisura lake kama kenge, mwanaume gani un akuwa mpumbavu kiasi hicho.
 
Haya maamuzi mengine huwa mabaya sana, sasa hao watoto amewanywesha sumu kwa kosa gani?

Unamkata mtoto panga la kwanza analia, na mwenzie anakutazama, bado unamkata la pili, la tatu, mpaka anakata roho, then unamgeukia mtoto mwingine, this is insanity.

Huwa siamini kam kuna ugomvi usio na solution hapa duniani, sawa hasira hupanda, lakini pia ukijipa muda zitashuka, na ukishazoea majaribu ya mwenzio, sioni sababu kwanini yawe yanakupandisha hasira kila wakati.
 
Kuoa / kuolewa ni zaidi ya kurusha dege la kivita. Kwa mtu ambaye amelelewa mayai mayai ni vigumu sana kudumu kwenye ndoa. Ndoa ni zaidi ya majukumu. Vijana wengi (sio wote) wanaingia kwenye ndoa kichwa kichwa. Malezi mazuri ni jambo muhimu sana kwa wanafamilia vinginevyo vifo vya aina hii vitazidi kuongezeka siku hadi siku.

Wajibu wa baba na wajibu wa mama uchukue nafasi yake katika familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom