Mbeya: Mwalimu wa Shule ya Loleza Girls afunga Bweni na kuwalaza Darasani Wanafunzi


Wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza (Kombi ya HGL) usiku wa kuamkia Julai 11, 2023 walilazimika kulala darasani ikidaiwa kuwa ni baada ya mwalimu wa bwenini kuondoka na funguo za bwenini kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kupitia vyanzo vyake vya taarifa anasema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo.

Homera ameeleza kukerwa na tukio hilo kwenye shule ya Loleza anayosema ni ya mfano ikikusanya watoto kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini hivyo hata kama watoto walifanya kosa ilifaa kupewa adhabu walizojiwekea shuleni hapo na si kuwalaza darasani ikizingatiwa na musimu huu wa baridi.

Mwalimu anayedaiwa kuondoka na funguo za bweni ambaye ni msimamizi wa watoto hao bwenini Sabina Haule anasema chanzo ni ukorofi wa watoto hao lakini hakuwaamuru kwenda kulala darasani kwakuwa baada ya kufunga bweni alirudi baadaye majira ya saa nne usiku na kuwaelekeza kwenda kulala mabweni mengine ambayo hayana wanafunzi lakini watoto hao walikaidi na kwenda kulala darasani kimyakimya hivyo kuomba msamaha kwa mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Shule ya Loleza Mwal.mkuu Betiseba Nsemwa alipoulizwa juu ya suala hilo amesema.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa, alipata nafasi ya kutembelea hadi darasa ambalo wanafunzi wanadaiwa kulala usiku kisha kuzungumza na wanafunzi hao akiwaasa kuzingatia nidhamu wawapo masomoni na kumuagiza Afisa Elimu Mkoa Mwl. Ernest Hinjo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mwalimu husika.
 
Wewe ni mzazi bora sana
 
Mwanamke ni kiumbe dhaifu[emoji1787]
We are special Mkuu. Mungu alituumba baada ya kuwa amekamilisha kila kitu.,sisi ni malastborn wa Mungu.
Kutundika miguu juu watoto wa mjini hawawezi elewa.
Hii haina mbabe.
 
"Mwl wa mase hapa ni wapi..." huu msemo tu unatosha kuachana na wanafunzi kazuge shule saa nne nenda chini ya mti vuta fegi yako mwisho wa mwezi kapokee salary kale na familia yako
 
Ni kweli wanafunzi wengine ni wake za watu kwani walishaingia kwenye mahusiano ya kingono.
Hivyo kuwafuga hakuna tofauti na kufuga kunguru.
Kidato cha 6 ni watu wazima tena mikoani wanachelewa kuanza shule unakuta form 6 ana miaka hadi 24 kumfuga kama mfungwa ni upuuzi.
 
Kwa nini wanafunzi wa form 6 wanaitwa WATOTO!! watu wako above 18 years siyo watoto hata kidogo wanatakiwa waheshimiwe.
 
Homera nae hana dogo anaacha kuhangaika na mambo makubwa ya msingi anahangaika na mambo ya kipuuzi puuzi ambayo mengine yanaishia kumfedhehesha kama lile la PANDAHILL

matokeo yake ili kuficha aibu wanaamua kutengeneza kosa ili kosa liwepo mambo mengine ni yakumaliza tu wala hakuna haja ya kuhangaika na waandishi wa habari kila kukicha kufuatilia walimu na wanafunzi
 
Maadili yameporomoka sana. Hawa wanasiasa mara nyingi hawana ku balance changamoto wao huegemea upande wa wanafunzi hata kama wenyewe ndio wakorofi.
 
Maadili yameporomoka sana. Hawa wanasiasa mara nyingi hawana ku balance changamoto wao huegemea upande wa wanafunzi hata kama wenyewe ndio wakorofi.
Homera nimemdharau sana reasoning yake ndogo sana kwenye maswala ya kijamii
 
Huyo homela inaonekana ni mtu wa totoz sana jamaa kila siku misala yake ya mademu tu kama ana uchungu sana awasemee na wavulana hebu deal na mambo ya msingi braza hizi kiki nyngn muwe mnaziangalia kwa makini
 
Kwa hiyo wanafunzi kulala darasani nyie mnaona ni sawa?Siku nzima mtu yupo darasani,baadae jioni ale,kisha usiku preparation time,baada ya preparation time mtu kaondoka na funguo ili iweje?Kesho tena huyu huyu mwanafunzi aamke mapema kujiandaa,usafi nk.Adhabu zipo nyingi ila sio ya kuondoka na funguo,Wewe mtu mzima na akili zako upo nyumbani umerelax watoto wa watu umewafungia wasilale kama sio ujinga ni nini hiki.Mimi nimesoma shule za bweni nikisikia mtu anafanya hivyo nashangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…