Mbeya: Wanandoa Mbaroni Baada ya Kumshushia Kipigo Hadi Kifo Mtoto Wao wa Miaka Minne

Mbeya: Wanandoa Mbaroni Baada ya Kumshushia Kipigo Hadi Kifo Mtoto Wao wa Miaka Minne

Ufala huu... Nakumbuka kuna dogo wa miaka mitano jirani na nilipopanga alijiendeshea kitandani ucku akiwa kalala... Wazazi walipoamka asubuhi na jazba wakaanza kumpa kichapo cha mbwa koko!

Ikabidi niende kuingilia ugomvi na kuwazuia wasiendelee kumpga. Uzuri nilikuwa nawamudu, Nikawaambia km shida ni kufua kinyesi chake km walivyokuwa wanalalama mi nitafua ila wamwache dogo.

Ikabidi nimuulze dogo ilikuwaje akaharisha kitandani? Akanambia usiku tumbo lilikuwa linamuuma, alipomwamsha mama yake ampeleke chooni akakataa. Akamwambia km huwezi kuamka kunya hapohapo kitandani... Dogo kutokana na kushindwa kuichambua ile kauli ukilinganisha na umri wake pamoja na break kufeli akakuta tayari ashaharibu hali ya hewa kitandani

Sisi wazazi muda mwingine ndo visababishi vya watoto kufanya mambo ya ajabu!
 
Baba unaanzaje kutoa kichapo kwa mtoto under 5 years? Mental health is real.. CCM must go now
hizo akili za ki CHADEMA kabisa maana ccm hakuna mtu mwenye akili finyu kama huyu chizi unapiga mtoto 4 yrs kweli kisa mbunye imeshawishi apige ? sasa jela maisha inamuhusu na mbunye atakuwa anazisikia tu
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Ramadhan Tembo Mwakilasa [28] maarufu kama Rama Love ambaye pia ni Mwandishi na Mtangazaji na Mariamu Charles Mwashambwa [28] wote wakazi wa TEKU viwandani Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Chloy Ramadhan [04] kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Ni kwamba Novemba 25, 2024 saa 2:00 usiku huko Mtaa wa TEKU viwandani Jijini Mbeya, mtoto Chloy Ramadhan [04] alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Ramadhan Tembo Mwakilasa [28] akishirikiana na mama yake wa kambo aitwaye Mariamu Charles Mwashambwa [28] wote wakazi wa TEKU viwandani.

Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukatili na unyanyasaji kwa kumuadhibu mtoto baada ya kujisaidia kwenye nguo alizokuwa amezivaa.

Jeshi la Polisi linawataka wazazi/walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watoto pindi wanapokosea na badala yake watumie njia sahihi na salama kuwafundisha au kuwaelekeza bila kusababisha madhara.

View attachment 3162069View attachment 3162070

Hawa waandishi wa aina gani?
 
Shida kuu ni mwanamke,

Sisi tunaozurura mitaani tunayaona saana
Mwanamke kama bado unajiweza usikubali mwanao akalelewe na mwanamke mwingine,

Wanaume huwa tunaingizwa mkenge Kwa kuambiwa makosa feki ya mtoto wetu hapo tunajua moja Kwa moja mwanangu hamskiliz mke wangu kumbe maskin hujui tu akina hawa,

Hapa jirani kuna jamaa alikuwa akirudi job anakata bakora na kuingia nayo ndani huku akituuliza hivi huku watu hawajui kuadhibu? Dogo ana mialama kibao mgongoni,
Walifika hatua kakitoka kuoga wanakaimbia kakae nje Kwanza kakauke haijalishi kiangazi, masika,usiku wala
mchana
Kuna mwingine kapewa na dada yake kaanzie chekechea kwake basi kamerudi shule sasa sijui nywele zlichomoka kwenye kibanio, weee Ile kanafika Tu hakajaulizwa habari yoyote Kofi nani kachomoa nywele hakajajibu vzuri kakaongezwa
Inauma saana
 
Back
Top Bottom