Mbezi Beach wamekosaje lami? Mbona Mbweni, Manzese na Yombo kuna lami?

Mara ya Mwisho kwenda Mbweni ni lini....

Hapa Dar hakuna mitaa yenye Barabara nzr na zenye quality kama Mbweni...

Hiyo Masaki yenye barabara zake zina viraka na madimbwi hatari

 
Magufuli alipanga Kuweka Lami mbezi yote na kuweka mfumo wa Maji Taka...Eneo lilikua kijengwe pale Kilomgawima la kupokea maji taka..Posta pia ilikua ifumuliwe yote...Sasa sujui nn kunaendelea...
 
Kazi za ovyo sana. Uchafu mtupu
Vilami ushenzi havitoboi hata miaka 2 nakwambia
 
Mwaka huu wataweka baadhi ya mitaa Chief nishauona mkeka.
 
Magufuli alipanga Kuweka Lami mbezi yote na kuweka mfumo wa Maji Taka...Eneo lilikua kijengwe pale Kilomgawima la kupokea maji taka..Posta pia ilikua ifumuliwe yote...Sasa sujui nn kunaendelea...
Mbezi beach hawana mfumo wa maji taka ,watu huko hufaulisha maji taka
Kwenye mifereji nje
Ukipita usiku mitaani ukisikia sauti ya pump ujue kuna shuuguli hapo

Ova
 
Hata mimi huwa sielewi mbezi beach pamoja na mikocheni ukiangalia barabara zilivyo na majumba ya kifahari yaliyopo maeneo hayo ni vitu viwili tofauti
 
Hii ndiyo Kijichi jimbo la Mbagala Wilaya ya Temeke Maisha yanaenda kasi sana
 
Sio haba hata sie wa G'mboto uswazi Mwendazake alitujengea lami mpaka mlangoni, bila kusahau maji ya Dawsco. Toka ameenda mradi wa maji umesimama.

I guess chuma kilijua kina muda mfupi wacha kituhangaikie watu wa hali ya chini, hawa matajiri wa mbezi na kwingineko wata jisort akiondoka.
Kifupi ilikua awamu ya wanyonge.
 
Huwa mnapenda kudandia vitu msivyovijuwa na kumpachika mtu sifa asizostahili.

Mradi wa DMDP ni kazi ya Jakaya Kikwete pamoja na daraja la Mfugale, ila utekelezaji umeangukia awamu ya tano.

Huu ujinga ndio mtasababisha watu wang'ang'anie Madaraka kwa kisingizio cha kumaliza kazi walizozianza, huu ujinga Magufuli na machawa wake walishauanza.

Mimi ni mjumbe wa project ya DMDP mtaani kwangu tulichaguliwa Kikwete akiwa Rais, hunidanganyi lolote kuhusu mradi wa DMDP.

Tena world bank wasingesimamia wenyewe hii miradi yao ungesikia imehamishiwa Chato.
 
Hata kuamia Dodoma alipanga Nyerere ila kafanya Magufuli hivyo huna chakutuambia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…