Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Mbingu ni kweli ipo na huu ni ushuhuda wangu binafsi

Wacha weeeeeeeeeeeeeweeewwww
Mkuu mm inanitokea mara nyingi sana hiyo kwenda huko ambapo mnaita mbinguni ila shida yangu wakati wa kurudi unajikuta unarudi kwa spidi kali hatari na mara nyingine njia siijui hapo huwa nalia 😂 😂
 
Hongera mkuu next time ukienda usisahau kumpiga Yesu picha
Aisee sijawahi kumuona huyo jamaa ila nikiona hata malaika nitawauliza maswali mengi ila target yangu nimuone mungu nimuulize maswali au hata yesu au muhamad huwa naenda mara kwa mara lkn wananikimbia 😁😁😁
 
Hahaaaaaaaa, Kiranga bwana. Una Blah blah nyingi na Kiingereeza cha ugoko eti utanibabisha na kuniyumbisha. Yaani ukiandika hizo theories unajiona msomiiiiiii. Inawezekana family back ground yako umetoka kijijini na familia duni sana na sasa kuwa Marekani yaani ni kama upo Peponi na ndio maana unakuja na hizo theories na kiingereza cha Ugoko humu kutisha na kupotosha vijana. Hizo theories nilisomaga advance pale Galanos Secondary kipindi hiko na nyingine nilisoma pale SUA wakati nachukua First degree mpaka tukawa Tunamuita Prof. Mrema wa Department ya Soil Science Schrodinger. Nakumbuka kuna jamaa mmoja hadi leo kwenye group la letu la Advance Galanos Combination ya CBA tunamuita Quantam. Kwangu mimi huna mpya kiranga. We sema jingine mkuu.
Hii ni inferiority complex inaongea, kama mlikuwa hamuijui, leo ndiyo mmeiona hapa.
 
Nimeona watu wengi humu JF wakimponda na kumkashfu Mwalimu Mwakasege baada ya kusema Mungu alimfunulia kuhusu mbingu na kwenda Mbinguni.

Binafsi nadeclare interest kuwa ninatumika Kanisa la TAG kama Mzee wa Kanisa huku Nyanda za juu kusini pia ni Mtumishi wa Serikali na huwa nahubiri mara moja moja. Siandiki hivi kwa kufurahisha watu au kujisifu wala kutaka kumsafisha Mwalimu Mwakasege ila naeleza kile nilichoshuhudia na kile ambacho Mungu amenitendea.

Kwa umri na muda niliomtumikia Mungu kama Mkristo nafahamu Mungu anajifunua kwa watu wengi yeye binafsi na pia kuwafunulia kuhusu wengi kuhusu mbingu.

Binafsi, nashuhudia leo na kikiwa na akili timamu na dhamira njema Moyoni mwangu kuwa nimemuona mwenye haki "Yesu Kristo" si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo na amenitokea kwa namna mbalimbali tofauti na watu wanavyokashfu kuwa tutatokewa na Mapepo yaliyovaa sura ya "Bryan Deacon" yule aliyeigiza "Filamu ya Yesu" Pia nashuhudia, Mungu kunifunulia na kuiona mbingu.

Mafunuo haya ya kutokewa na Yesu kwangu mimi hayakuwa kwa jinsi ya kimwili "yaani kunitokea physically" ila ni katika ndoto na Maono ya usiku pia wakati nasali nikajiona tu nimekutana naye.

Leo sitaelezea kuhusu kutokewa na Yesu ila nitaelezea kuhusu ushuhuda wangu wa kuiona Mbingu ila nasisitiza katika hilo, kila maono, ndoto au mafunuo ya Kimungu yanajengwa chini ya Neno la Mungu. Neno: Ayubu 33:14-16 hapa Mungu anasema kuhusu kusema na wanadamu kuhusu ndoto ns mqono ya usiku.

Neno: Yoel 2: 28-29 Anasema kuhusu "Ndoto na Maono".

Kuhusu Mungu kuwafunulia watumishi wake mbingu, tunaona Paulo anasema namna alivyochukuliwa na kuoneshwa kuhusu Mbingu katika 2 Korintho 12: 2-9 pia Stephano naye anafunuliwa katika Matendo ya Mitume 7:56 na pia Mtume Yohana anafunuliwa kuhusu Mbingu wakati anaandika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

Binafsi, Nakumbuka ilikuwa 2016. Mungu alinipa Neno toka Yeremia 33:3 inayosema "Niite nami nitakuitikia na nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua" pia kwa muda mrefu nilikuwa naimba moyoni mwangu wimbo mmoja wa zamani sijui uliimbwa na kwaya gani ila kuna kipande wanaimba " Nimpeleleza nani raha ya Mbingu×2, Yesu ndiye wa Kumpeleleza"

Nakumbuka Siku hiyo niliamka kama kawaida saa 9 alfajiri na kusali. Ilipofika saa 11:45 nikasema nilale kidogo ili nikiamka saa 1 hivi niende kazini. Nilipolala kama saa 12 alfajiri nikaona Malaika mmoja aliye kama mwanadamu amevaa mavazi meupe yenye kung'ara huku akiwa mwenye sura inayong'ara ananiambia "nimetumwa nikufuate". Akanishika mkono, nikaona natoka kwenye mwili upande wenye moyo.

Nikapita kwenye bati la nyumba bila kizuizi. Safari ya kupanda juu ikaanza kwa speed ya ajabu huku akiwa amenishika Mkono. Nikaangalia chini na kuona mwili wangu, mke na mtoto wangu wamelala kitandani. Unaona nyumba na miti ya duniani. Tukapaa juu kwa spidi nikaangalia chini tena na kuona kadunia kalivyo kadogo then tukafika katika nchi ile ambayo "watu" wanaimba na kumuabudu Mungu. Nikaungana nao tuliimba "Bwana Mungu nashangaa kabisa"

Sijui nielezeje muonekano wake nchi ile ila ni nzuri na ya meta meta. Hali ya hewa na mazingira ni tofauti na huku duniani. Nchi ile ni kweli na mji ule ni kweli. Jitahidi usikose kuingia mji ule.

Baadaye nikaambiwa turudi na kwa speed ya ajabu, najikuta naingia mwilini mwangu upande wa kushoto kwenye moyo, mwili ukawa kama umepigwa "shot" nikashtuka.

Binafsi, nimewasikia na kuwaona watumishi wengi wa Mungu wanaoshuhudia kuhusu Mbingu huku kwetu na sehemu myingine. Ukiacha hao maarufu, japo "Zumaridi hapana kwani inaonekana ana shida ya akili" Ukiacha Mwakasege, hata Marehemu Kulola alishashuhudia siku moja kufunuliwa kuhusu Mbingu.

Nami nimeona nishare uzoefu wangu kuhusu Mafunuo ya Mbingu. Siku nyingine nitaeleza kuhusu kutokewa na Yesu ana tutokeaje, yupoje na tunajuaje kama ni Yesu.

Asanteni.
Asante umetufariji Sana
 
Bro kutoka moyoni, leo nimekudharau sana. Lengo lako ni nini kuniwekea hiyo theories?
Hujanidharau vya kutosha, jaribu tena.

Bora hata ungeuliza hili swali kabla ya kujishebedua unajua sana umesoma SUA, this and that.

Sasa kumbe ulikuwa unajishebedua kote huko bila hata kujua mimi nimeandika kwa lengo gani?
 
Kila mtu kashaota Yuko mbinguni...na kila mtu kashaota anaongea na Mungu.....sioni cha ajabu kabisa ..since ndoto ni mkusanyiko WA mawazo yako...ukiipenda Sana Range Rover kuna siku utaota unaendesha Range Rover
 
Hajawahi kunibabaisha kwani najua ana shida gani? Waliopinga uwepo wa Mungu walikuwepo na watakuwepo hadi mwisho wa dahari. Hana mpya na Biblia inawaita "Wapumbavu" kwa umri wangu, hanipati, hanibabaishi, haniyumbishi wala hanipotezei muda wangu kujibizana naye kuhusu uwepo wa Mungu kwani macho yangu yameshuhudia mengi yanayothibitisha pasi na shaka uwepo wa Mungu na wala sina mashaka naye. Najua alikuwepo, yupo na atakuwepo milele na milele. Poleni kwa huo "Upumbavu" uliowajaa ila samahani kwa hilo mkuu.
Mungu yupo ila nyinyi mnafanya mzaa sana, upelekwe mbinguni? acheni utani na Mungu wetu.
 
Hujanidharau vya kutosha, jaribu tena.

Bora hata ungeuliza hili swali kabla ya kujishebedua unajua sana umesoma SUA, this and that.

Sasa kumbe ulikuwa unajishebedua kote huko bila hata kujua mimi nimeandika kwa lengo gani?
Bro, mi nimeshamaliza. Leo nimekudharau sana, tena sana. Yaani ungekuwa karibu yangu ningekutema mate. Lengo la kuweka hizo theories ni nini? Yaani unitishe na hayo majina ili uonekane msomiiiiiiiiiiiii na unajua vituuuuu😃😄😃😀😆😅🤣 ngoja nikuignore maana sio level yangu. Wewe ni "empty kabisa upstairs". Ngoja nijibu reply za wenzio ila sio wewe nimekuignore kuanzoa leo.
 
Bro, mi nimeshamaliza. Leo nimekudharau sana, tena sana. Yaani ungekuwa karibu yangu ningekutema mate. Lengo la kuweka hizo theories ni nini? Yaani unitishe na hayo majina ili uonekane msomiiiiiiiiiiiii na unajua vituuuuu😃😄😃😀😆😅🤣 ngoja nikuignore maana sio level yangu. Wewe ni "empty kabisa upstairs". Ngoja nijibu reply za wenzio ila sio wewe nimekuignore kuanzoa leo.
Wewe una inferiority complex.

Hata nikikusaliia "Hello" utanijibu kwa ghadhabu zako za maisha "Who are you calling a hoe?"

Una frustrations gani za maisha?
 
Back
Top Bottom