Mbinu hii ikitumika, Dr SLAA anatoka gerezani siku mbili

Mbinu hii ikitumika, Dr SLAA anatoka gerezani siku mbili

Ingependeza zaidi ungeonyesha mfano wa kutoa tamko🤣🤣🤣🤣
 
Wewe umeongea kweli, mtu yupo kwenye key board anazungumza maswala ya njozi zake tu. Huwezi kupambana na serikali kirahisi rahisi kama unavyo dhania. Ona ANC walipambana miaka 30 Mandela akiwa ndani tena mapambano ya kigaidi. Maelfu ya watu walikufa kwenye mapambano yale. Ona Congo M23 na vikundi vingine vinazaidi ya miaka 20 vipo msituni vinapambana tu. Wewe umelala kitandani na kasimu kako unataka kuwaongopea watu.

Unaishi kwa kudhania. Waliopo madarakani wanajua nguvu ya uma, kuna mstari mwembamba sana kati ya ujeuri wanaoonyesha na jinsi tutakavyobembelezana.

Juzi tu hapo Ruto kdg awapigie magoti gen Z. Ila alipiga kwa Uhuru na Odinga ndo urais ukaendelea.

Waambie waliokutuma kuwa huku hatusamehe, tukishika channel tunakutoa white house, na tunakutoa mpaka kwako, ukajaribu kuishi huko uarabuni, wala hizo gunia za hela hazitasafiri nanyi.

Endeleeni.
 
Nilidhani una akili

Slaa balozi? Aliyesema chakadomoz mnatekana na kuuana, kwamba Lissu risasi ni normal tu, na akawauza pale Serena hotel?

Una akili fupi mno aisee…. Huyo mzee anatesingizia usalama wamemwambia wako tayari kwenda barabarani kuqndamana?
Acheni akome na ufitini wake

Chadomoz mnahangaika sana kihisia… and you don’t know where you stand

Ni bahati mbaya sana kila anayetetea haki anaonekana CHADEMA, mimi ni mwanachama wa CCM nisiyependa mambo mabaya ya CCM kwa ajili ya nchi yangu.

Sasa wewe unafanyia kazi buku 7 yako ndo tatizo
 
Kwani Kosa la Dr.Slaa ni lipi? Juzi niliona Clip Rais ana sema "Rais wa Tanzania haondolewi hivyo mnavyopanga huko mitaani, na uzuri mipango yenu yote na kila mlichoongea ninacho"

Nikahisi labda Dr.Slaa ni moja ya wahusika. Sifahamu kashitakiwa kwa kosa gani wana JF.

Na kama alihusika kupanga uhaini ni kosa, ama aombe asemehewe au atafia jela.
Alikuwa anazungumza lini na akiwa wapi? Pengine kijembe alikuwa anawatupia hao hao CCM wenzake.
 
Wanajukwaa heshima iwe kwenu.

Hivi kweli wenye mapenzi mema wanashindwa na walaghai na wafitini wenye kumshikilia Mzee Slaa na kumnyima dhamana kusiko haki?

La Hasha,
Mbinu hizi zitumike, huenda zikazalisha mengi zaidi mazuri ya neema kwa WaTz nchi ikapata mabadiliko muhimu sana kupitia sakata la Dr SLAA.

Moja,
Mawakili wooote wanaopambania ile kesi watangaze kujitoa na kuiachia mahakama na mawakili wa serikali waendelee nayo wenyewe. Kwanza Slaa mwenyewe alisomea canon law hivyo anaweza kujitetea mwenyewe.
Wakitaka wamfunge, wakitaka wamuue.
Hili suala litangazwe waziwazi mchana kweupe, kwamba watu hawawezi kupoteza muda wa kwenye mahakama zisizofuata kanuni, kuchezeana sarakasi zisizo na kichwa wala miguu.

Pili,
Hili suala la maCCM na wauza bandari la Tanganyika kutaka kumkomoa/kumuua Dr. Slaa (mtetezi wa kweli haki za Tanganyika ndani ya Tanzania) LIWEKWE WAZI, ifanye PRESS ya ukweli, na Itangazwe kuwa endapo ikitokea Dr SLAA akafanyiwa jambo baya kama kufungwa au kufa basi maandamano hayatokoma mpaka mkoloni mweusi atakapoiachia nchi yetu.

Tatu,
Tangazo la maandamano litolewe endapo Dr. Slaa hatoaachiwa ndani ya siku mbili. Kama wanashakia usalama wake basi hao wanaodhaniwa kutaka kumdhuru ndo wakamatwe.

Abdul na Mama yake hawawezi kufanya wapendavyo kwenye nchi ya wote hii.

HAKI LAZIMA ISIMAME, WALA SIYO YA KUBEMBELEZANA.
We umelewa pombe ikiisha uje kuandika tena
 
Amiri jeshi mkuu na msimamizi wa mhimili ule unaoimeza mahakama na kukosa kutenda haki, huyo wapili ndiye subject wa kesi aliyeshtakiwa nayo Dr. Slaa baada ya kusemekana kutaka kumwaga hela uchaguzi wa CHADEMA.

Hao ndo wahusika wakuu wa hiyo kesi, hata wewe unajua, majaji wanaorusha rusha mpira wanajua, polisi wanaojikosesha gari wanajua, na wewe unayejaribu kupindisha maneno hapa UNALIJUA HILO.
Hv unafikiri unawaandika mazuzu? Kafanye mambo yako umeandika utumbo
 
Inaniuma sana kuona mzee Dr. Slaa anateswa na mwanamama raia wa nchi nyingine (mzanzibari).
Na anatumia watanzania wenzake kumtesa mtanzania..li nchi Lina laana hili!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Inaniuma sana kuona mzee Dr. Slaa anateswa na mwanamama raia wa nchi nyingine (mzanzibari).
Mpuuzi wewe. Uzanzibari umehusu nini. Acha ubaguzi.
 
Back
Top Bottom