Mwanamke TAJIRI akupende mwenyewe kaka,ila ukitaka mwanamke Tajiri lazima na wewe uwe stable
huwezi kwenda kula chipsi SINZA useme utakutana na mwanamke TAJIRI kuna sehemu ambazo zinatakiwa
ziwe katika circle yako ya maisha,mwanamke Tajiri hupatikana sehemu za matajiri ishu ni kuweza afford ingia
hizo mahala,maana kununua soda/juice/soft drink (ya kawaida) kwa 50k mkuu yakupasa ujitoe sadaka haswa
ila Yote kwa Yote Mapenzi ya kutafuta SIO mapenzi,ukiweza Afford ingia 5 star hotel kila siku kwa lengo eti upate
mwanamke TAJIRI nadhani si sawa,Mapenzi ni zaidi ya status zenu Financialy,Sawa una pesa Utapata Mke ana Pesa
haya sasa mko kwenye NDOA mna watoto, mke hajui malezi,mke hajui kitu,Yani huelewi hata ni imekuaje akawa MKE wako.
Fungua akili yako Omba Mungu akupe mke mwenye Hekima zake asie Mbinafsi mtakae ongea Lugha 1,Kaka amini nakwambia
Unaweza kuwa na mwanamke Kapuku Masikini na asikuombe hata senti yako na daily anapendeza kwa pesa za wazazi/kaka/ndugu zake,nk ni pure Maskini ambae si mzigo.
Tabia ya kuomba omba,ipo ndani ya Mtu na si katika uhalisia wa kipato chake,Nimeshawahi date mwanamke hana shida kabisa kuanzia familia yake mpka pale alipo sasa Lakini ni omba omba yule mwanamke Matonya akasome.
Uzungu mwingiiii kumbe ni ili tu atumie zangu zake zitulie bank so ishu sio Mtu mwenye PESA ishu ni MOYO brother, Ukipata mwanamke mwenye Moyo/utu/upendo,nk umemaliza
Hii ya kutafuta Mahusiano na stable woman kipesa au stable Man Kipesa itatokea watu puani na wapo ambao wanakula matunda ya walichokipanda.
Omba Mungua akukutanishe na Ubavu wako,Kwisha.