Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Mbinu za kuchukua namba ya Simu katika Mazingira Magumu

Wazee wa kupambania Kombe..
Huwa mnatumia Njia gani kuomba/kuchukua namba za simu katika Mazingira MAGUMU na HATARISHI?

Umafia:

Part 1>
Nilikuwa nipo katika Daladala watu wengi vibaya mno, nikatupia jicho pembeni nikaona KIFAA kimetulia kinachezea simu. Nikajiuliza hapa namba nabebaje? Kuangalia nje bado vituo viwili nishuke.

Kuchek katika wallet business card binafsi zimeisha zimebaki za Ofisini (Michoresho) nikaona hii hapana kuitoa.

Nikajipapasa huku na kule bahati nzuri nilibahatisha kipande cha TICKET ya Bus la mkoani, na katika ile ticket kuna namba yangu ya SIMU, sikujiuliza mara mbili wakati nashuka nikamshtua yule mrembo kwa kumgusa begani then ile ticket nikaipitisha kwa chini kama vile alikuwa kaiangusha then nikamkazia machoni huku nikimuonyesha ishara ya NIPIGIE. Mie nikashuka zangu huyo Home nikatulia.

Zikapita kama siku 5 kimya, nikaona hapa Mkeka umechanika.. siku ya 6 jioni nipo viti virefu nashangaa namba ngeni kupokea ni yule Manzi.. akajitambulisha pale.. then the rest is history..😋

Kuna wengine wanatumia mpaka Hela kuandika namba (Karatasi hakuna).. mtu anachukua noti ya elf 10 anachora namba yake anamkabidhi mrembo..
Siku uje na uzi wa kupeana mbinu za kupambana na ccm ili Taifa lipone
 
Ndio maana wameseme inabidi watu wasome kwanza elimu ya katiba kwa miaka mitatu. Hafu ndio wadai katiba maana hawajui wanachodai.
Vichwa vinawaza ngono, mpira na kubet tu.
FB_IMG_16852199375666242.jpg

Siku uje na uzi wa kupeana mbinu za kupambana na ccm ili Taifa lipone
 
Part 2 aisee ni kisa kirefu kidogo..

Ila huyo Manzi baada ya kuwasiliana siku mbili tatu niligundua kuwa ni Mke wa Mtu na ametoka kufunga ndoa recently na aliyemuoa sio yule aliekuwa nae pale.

Yaan story ni ndefu ila ile Ndoa sina hakika kama ipo au La.. ila mie ndio nikawa Suspect namba moja, nilibadiri kuanzia namba yangu ya simu, Mpaka Makazi niliyokuwa naishi.

Kwanini ikawa hivyo mkuu ?
 
Part 3.

Kuazima PENI mara moja na Kuingiza Karatasi uliyoandika namba ndani ya Bomba la Peni na kumrudishia mwenye Peni..


Hii nilipiga huko Mkoa wa Morogoro kwenye Semina elekezi, wakuu wamejipanga hapo na kikao ndio kinakaribia kuisha sina jinsi zaidi ya kufanya ubunifu tajwa hapo juu..

Baadae nilipigiwa simu tukafahamiana zaidi.
 
Back
Top Bottom