Mbinu za kumfukuza kwako kijana aliyefikia umri wa kujitegemea

Kijana anapambana kutoboa...changamoto ni nyingi...wewe unamuona mzembe...
Unamsimanga lakini anavumilia...
Ghafla anatoboa ana kupita kiuchumi..
Anaamua kukuchunia kutokana na masimango uliyompa...unaanza kulalamika kuwa hakumbuki fadhila.

Kataa wavivu...ila kama anapambana kujinasua kiuchumi mpe support.
 
Kwani aliomba umlete dunian km sio nyege zako...km vipi mpe mtaji akapambane mbele kwa mbele
Kuzaa ni asili
Haya wanyama, wadudu, ndege na mimea inazaliana
Hata wakimbizi wako vitani Bado wanazaa
Masikini nao laZima wazaliane, hakuna hoja ati kwakuwa ni masikini asizae.
Kikubwa ukifikisha umri wa ujana Toka nje pambana na umasikini wako na familia yako
Tusitafute excuse za ovyo
 
Haya mambo ni kuyaendea kwa akili kama wewe ni mzazi,..Kuna jamaa yangu alifukuzwa kwao na baba ake kwa kigezo hichohicho cha umri wa kukaa home umekwisha, manyanyaso kibao plus kunyimwa msosi ,mwamba akaona isiwe tabu akaondoka akaanza kupambana baada ya muda kweli mambo yakanyooka, ila sasa jamaa hataki kuwasaidia kwao kifupi mkubwa alijenga roho ya kisasi hataki kuzisikia habari za nyumbani kwao.
 
Kwa vijana wanajipambania na kukwama hao Sina shida nao
Shida yangu ni wale wapo wanabweteka hawajitumi kabisa
Hao laZima tuwakemee bila aibu
 
Kumfukuza kwao ndo kulimpa hasira na kupambana hatimaye ametoboa.
Hii ni kanuni laZima umri ukifika pisha nyumbani kapambane
Utajiri hauko nyumbani hapo Kuna comfort zone ambayo haitakuinua kiuchumi
 
Mtoto wa tajiri hawezi kuhama nyumbani, kwenu maskini mnaoshea chumba kimoja, afu matoto mengi kama tim ya Mpira, chakula Cha tabu, njaa tupu ndo mtahama

Watoto wa tajiri kama dewji na bakhresa kwao wapo wawili au mmoja afu nyumba yenyewe ghorofa apartment zaidi ya kumi, ahame au wahame waende wapi nani atasimamia mjengo, nani atasimamia Mali angali wazazi tyari ni wazee????
 
Wewe ni mtoto wa Bakhresa au Mo Dewji?
Kwanini ujilinganishe na mabwenyenye ikiwa unaijua hali ya familia yako ambayo inategemea labda wewe ndo utakuwa shujaa wao
 
Pumba tupu
 
Busara zinasema Mzazi una Jukumu la kumlea mtoto/watoto wako hadi Siku unaingia kaburini

Ila ni kosa kulea mtoto/watoto wa Watoto/Mtoto wako yaani Mjukuu/Wajukuu labda itokee huyo Mwanao/wanao walitangulia kufa kabla yako na kuwaacha watoto wadogo
 
Kumfukuza kwao ndo kulimpa hasira na kupambana hatimaye ametoboa.
Hii ni kanuni laZima umri ukifika pisha nyumbani kapambane
Utajiri hauko nyumbani hapo Kuna comfort zone ambayo haitakuinua kiuchumi
nakuunga mkono kwa hilo lakini unatakiwa uwe makini sana kwenye mbinu za kumuondoa bila kujenga chuki na hatimae visasi hapo baadae, hivi unashindwa nini kukaa mezani na kijana wako na kumuelezea uhalisia na maisha yanataka nini mpaka umnyime chakula, umuweke chumba kimoja na majogoo alfajiri yanamuwikia, kumuwekea mazao chumba anacholala afanyiwe vurugu na panya nk,....yani hata ingekuwa mimi nikiondoka nakata mawasiliano mazima iwe ntafanikiwa au lah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…