Mbinu za kumfukuza kwako kijana aliyefikia umri wa kujitegemea

Nenda kakodishe chatu na simba wa sabasaba uwaweke humo chumbani mwake
 
Umasikini ni mbaya sana,hizi mentality ni za kimasikini sana..kwani ukiishi na kijana wako akiwa anajitafuta Kuna dhambi Gani? Mpe full support huku ukimtia moyo..huo uhuru unaotaka aupate una gharama...
Kumbuka hata kazi Hana,ataenda kuishi geto na wahuni halafu abebe tabia zote za ajabu ushangae na roho Yako .
 
...Hivi ungejaaliwa kuwa na fedha nyingi ? Ungewaza kumfukuza home mwanao wa kumzaa?
Humfukuzi kwasababu una hela ama la. Unamjenga ili aweze kukabiliana na maisha na atakapo hama siyo kwamba utamuacha lazima umfuatilie na ujue maendeleo yake na akikwama huna budi kumsaidia
 
Jenga nyumba za kutosha uwagawie watoto wako
Kama ukifanya hivyo naye atakuwa anaweza kujenga za kutosha na kuwapa wanae? Hell No, aliyezoea kutafutiwa hataweza kujitafutia. Mkiwafanyia watoto hivi mtawaharibu. Wazungu wenyewe na akili zao hawafanyi huu ujinga wa waafrika matajiri wa kuwatafunia watoto kwa kuwajengea na kuwatafutia kila kitu na hivyo kuwafanya waishi kwenye comfort zone.
 
Hizi ni mbinu za vikabila vile vichovu. Sisi Usukumani hata akioa kijana anaolea akiwa hapo home na wanaruhusiwa kukaa mpaka miaka mitano wakijitafuta. Kama kijana hajaoa lazima awe na kajumba kake pembeni (tunaita m'aji) siyo kulala kwenye nyumba ya wazazi, ni huku mjini tu ndiyo tumekengeuka. Ukifanya yote hayo uliyotaja utakuwa na roho mbaya tu!
 
Awe anafungia mbuzi kwenye nyasi anafungulia warudi nyumbani.
 
Kwa wazungu na huku ni tofauti. Huku Africa ajira hakuna ni bora kumuandaa mwanao kutokuwa masikini baadae kwa hiyo si kila kitu wanachofanya Waafrika ni ujinga eti kwa sababu tu wazungu hawafanyi
 
Kwa hiyo na wewe watoto wako utawapa nyumba na mtaji wa biashara? Na wao wakizaa wa kwao wataendelea kufanya hivyo hivyo? Kwamba hawa vijana wanaozaliwa wanapaswa kukuta kila kitu kimeandaliwa? Maisha ndio yanapaswa kuwa hivyo?

Mimi nimemuelewa mtoa mada tofauti na wengi walivyomwelewa. Kijana kutoka kwenda kujitegemea hafanyi kwa kuwa baba ni maskini ama ni tajiri bali kwa kuwa amefika umri ambao anapaswa kujitegemea.

Mimi nina ushuhuda wa marafiki zangu wengi walioachiwa nyumba za kuishi na baba zao, wengi wao pamoja na kwamba wana kazi na wengine biashara hawajaweza tena kununua hata kiwanja ama kujenga nyumba zao. They are living on comfort zones na sidhani kama wanaona tena umuhimu wa kuwa na cha kwao. Mimi ninajenga nyumba ya tatu sasa na nilianza maisha mwenyewe from the scratch.

Wazazi wenye mentality za kufikiri kutafutiwa na kutafuniwa na wazazi kama wewe (ambao hapa JF ni wengi) mtaendelea kuwa spoil watoto huku mkifikiria mnawapenda na kuwajali sana watoto kumbe mnashindwa kuwapa fursa ya kujifunza kujitafutia wenyewe.

Wazungu wengi (labda ni kutokana na kuendelea na kuwa na mifumo imara) hawawajengei watoto wao nyumba na kijana akisha fika umri wa kujitegemea anaondoka mwenyewe kwenda kutafuta hata bila kuambiwa au kutimuliwa.
 
Kwa wazungu na huku ni tofauti. Huku Africa ajira hakuna ni bora kumuandaa mwanao kutokuwa masikini baadae kwa hiyo si kila kitu wanachofanya Waafrika ni ujinga eti kwa sababu tu wazungu hawafanyi
So kila mtu amtafutie mwanae kwa kuwa sisi ni maskini? Hivyo utafutaji ubaki kwa wazazi na mtoto akikuwa atumie tu na aendelee kuishi hapo kwako. Akishazeeka naye amtafutie mwanae, mwanae naye ale tu kisha amtafutie mwanae.

Ajira zimepatikanaje huko Ulaya? Sio kwamba huku Afrika tufanye kama walivyofanya wazungu ili ajira ziwepo? Ili kila mtu aliyefika umri wa kujitegemea afanye kazi kuliko akina baba kuwa na mentality za kuwatafutia watoto wakubwa chakula na hifadhi?? Kwa hiyo tuwasomeshe vyuo na wakihitimu tuendelee kuwalisha na kuwajengea majumba sio? Basi sawa.
 
Unamfukuza ili akawe mwizi?,ombaomba,danga? Au ni raha kuona damu yako ikihangaika mtaani?
 
Shida ya wa Africa ni ubinafsi uliopindukia hivi unawezaje kuwaza ujinga huu na kumfanyia mtu aliekuja duniani kwa starehe zako za nyege??? ni jukumu la waliofanya mapenzi kupambana kuhakikisha waliemleta duniani hajutii kuletwa, ndio maana race ya ki Africa ndio race yenye umaskini uliopindukia, tofauti na jamii ya watu wengine hivi kweli mafanikio ni kama mche wa mgomba ukifa mkubwa unaacha miche midogo ichukue nafasi ktk shina hilo hilo moja, ni aibu kuona jitu zima kama wewe huelewi namna bora ya kuruthisha mambo yanayofaa kwa uzao wako zaidi ya kuendekeza ubinafsi, huna maana kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…