Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Kwa ufupi tumeambiwa Watanzania tukakope maana usipolipa basi Serikali italipa,

Bahresa akikopa China ,
1. Serikali ndio mdhamini? na

2. Deni linahesabika kuwa ni sehemu ya Deni la Taifa?

3.Mo akikopa China dhamana Serikali yetu,ukiogopa kukopa shauri yako.

4.Muda si mrefu tutasikia Richmond imekopa mdhamana Serikali,huku na huku kumbe Richmond kampuni ya mfukoni,basi ndugu zangu Serikali italipa tu.
 
Kwa hiyo kama kampuni yangu inadaiwa na Bank, loans yangu itakuwa sehemu ya deni la Taifa? muongo mkubwa sana huyu na sijui kasoma wapi, aende akawadanganye wajinga wenzake sio sisi
 
No, if you owe money to a bank, it is not included in the national debt. The national debt is the total amount of money that the government owes to its creditors. This includes both public sector and private sector loans, but does not include personal debts owed by individuals to banks or other financial institutions.
 
Hapa kuna maswali ya kujiuliza.

Hayo makampuni ni yapi?

Na je, yamewekewa dhamana na serikalli?

Kama ndio, kwanini makampuni binafsi yakopeshwa kwa kudhaminiwa na serikali?

Kama CAG hakagui hesabu za mashirika binafsi, inakuwaje deni la makampuni binafsi kuingizwa kwenye deni la Taifa?

Je, huu ni utaratibu mpya au ulikuwepo tangu zamani?
Kasome uchumi, ujinga wako usiwe mzigo kwa wengine. Shule mkimbie halahu msumbue wenzenu? Shwani
 
Msamiati katika hiki tukiri wazi ni mgumu kuuelewa. Hinafsi huwa napata abc baada ya kupitia komenti kadhaa za wangwana wenye utulivu wa akili na wenye uelewa wa mambo haya. Utasikia
-deni himilivu
-tunakopesheka
 
Madeni ya makampuni binafsi sisi yanatuhusu nini? Au huwa wanawadhamini? waache uhuni wa kitoto.
 
Duh aisee yako mengi siyajui kumbe...sasa nauliza wenyewe wakikopa wanaweka nini bondi au ndo vitu walivyowekeza?ebu wataalam wa masuala ya uchumi tutoeni tongotongo
Mimi nijuavyo, mfano deni la taifa la marekani liko trilion 15 usd, unaweza kuta mifuko ya jamii inadai 30% ya deni hilo,,
Deni la taifa haina maana kuwa deni lote ni la nje
 
Kuna report huwa zinatolewa kila mwenzi na Bank kuu ukiwa unazipitia pitia utaelewa. Hizo habari za twitter na jf zimekaa ki propaganda sana
Deni hulipwa continuously, na mikopo vilevile huchukuliwa kwa mwendelezo pia
 
Mimi mfano wako siukubali. Twende taratibu. Mr. & Mrs. X wamekopa millioni mia nane benki kujenga nyumba za kupangisha. Wamewapangisha watu 20, na katika hao tuseme wote hawajalipa kodi ya miezi miwili na wanadaiwa millioni 6. Deni la millioni 6 ni la wapangaji wanaodaiwa na mwenye nyumba. Hili deni haliwezi kuongezwa katika deni la mwenye nyumba alilokopa benki. Ila linaweza kuongeza deni kama mwenye nyumba atashindwa kulipa pesa aliyotakiwa kulipa benki mwezi huo, na benki ikampiga faini ya 0.9% ya pesa aliyotakiwa kulipa.

Mikopo binafsi nayo iko kama nilivyoeleza juu. Kuna wakati, serkali inaweza kupata mikopo kutekeleza miradi fulani katika nchi. Hii miradi mara nyingi inatekelezwa na sekta binafsi (na mashirika ya umma). Mwisho wa siku sekata binafsi hutakiwa kuilipa serkali na serkali kulipa huko ilikokopa. Nakumbuka katika miaka ya 80/90 serkali ilipata pesa nyingi toka (nadhani) benki ya dunia kufufua zao la mkonge. Hiyo pesa ilipewa sekta binafsi ili kufufua kilimo cha mkonge. Hiyo mikopo ilichukuliwa, wakapewa mashamba mkonge, lakini badala ya kufufua hicho kilimo hiyo fedha yote iliingizwa kwenye shughuli nyingine. Tena hiyo pesa walipewa kama foreignm currency credit facility. Wahindi wengi waliipokea hii pesa na wengine walikimbilia Cana/Uingereza na wengine hadi leo wako TZ na ni mabillionea na hiyo pesa hawakulipa.

Pesa kama hiyo hapo juu ni mkopo wa serkali hata kama mtumiaji ni mtu binafsi na huwezi ukajumlisha hela waliopewa sekata binafsi kama mkpo unaojitegemea.
Umefunguka sana mengi..no dewji baadhi waliobeba..honestly speaking maraia wameamua kutunyonyoa na tutalia na kusaga meno maana mapanya yalifungiwa kwa mda mrefu..tutamkumbuka mwendazake
C3E1A8C7-862A-4AF4-83D8-527123065CD0.jpeg
 
Mkuu Kama shule ilikupiga kusho huwezi elewa chochote. Hii ni lecture ya mwaka wa pili wanaodoma B.A economics au finance.

National debt= public debt + private companies' debts.

Hivyo alichosema mwigulu ndoshule yenyewe.
Sisi tunataka hicho? Deni la serikali ni sh ngapi?
 
Back
Top Bottom