Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Mkuu Kama shule ilikupiga kusho huwezi elewa chochote. Hii ni lecture ya mwaka wa pili wanaodoma B.A economics au finance.

National debt= public debt + private companies' debts.

Hivyo alichosema mwigulu ndoshule yenyewe.

Na bado mtapiga hesabu hadi za pato ghafi kama Pole Pole enzi za shutuma ya ya upotevu wa 1.5 Trilioni. Yani Sekta binafsi inakopa nje fedha karibia ya serikali?
 
Taifa ni serikali pamoja na watu wake. Ikitokea hata wewe umeenda kukopa nje ya nchi na ukadhaminiwa na serikali ilo litakua deni la taifa maana umekopa na kuwekeza ndani ya taifa lako

Mwaka mmoja tu sekta binafsi imekopa trilioni 20, is it true. Yani spidi ya sekta binafsi kukopa inaizidi serikali?. Aisee
 
Serikali ikidhamini ni sawa tu kusema deni la Serikali
Point ambayo wengi hamtaki kuielewa ni kuwa, serikali ndio imedhamini hayo madeni.

Nadhani mnaelewa role ya mdhamini katika swala la mikopo, na mikopo mingi (private sectors) inaishia kwenye mifuko ya wa binafsi.

Tunatengeneza makampuni hewa, tunakopa na kuyadhamini kisha hela zinaingia mfukoni.

Deni litalipwa tu.
 
ni muhimu kusoma uchumi vitu vidogo vidogo ka hivi unavitambua (siyo lazima uchukue masomo ya uchumi)
 
Hapa kuna maswali ya kujiuliza.

Hayo makampuni ni yapi?

Na je, yamewekewa dhamana na serikalli?

Kama ndio, kwanini makampuni binafsi yakopeshwa kwa kudhaminiwa na serikali?

Kama CAG hakagui hesabu za mashirika binafsi, inakuwaje deni la makampuni binafsi kuingizwa kwenye deni la Taifa?

Je, huu ni utaratibu mpya au ulikuwepo tangu zamani?
hapana deni la taifa lina jumlisha serikali na sector binafsi hata uzalishaji unaangaliwa hivyo pia ni kanuni za uchumi na hii ni topic ndogo kwenye uchumi yuko sahihi mheshimiwa
 
Sasa wanaotubana wenyewe ni akina heche ambao wamesoma linauistics tu. Hawaelewi chochote

Na

Punguza dharau. Kama mnajua uchumi mbona deni la taifa limefika trilioni 91 sawa na asilimia 56 ya GDP. Kwa miaka miwili tukiendelea hivi deni la taifa litakuwa sawa na GDP 65%.
 
Kw
Taifa ni serikali pamoja na watu wake. Ikitokea hata wewe umeenda kukopa nje ya nchi na ukadhaminiwa na serikali ilo litakua deni la taifa maana umekopa na kuwekeza ndani ya taifa lako

Kwa hivyo deni la serikali ni Trilioni 46 tu?.
 
Kwa ufupi tumeambiwa Watanzania tukakope maana usipolipa basi Serikali italipa,

Bahresa akikopa China ,
1. Serikali ndio mdhamini? na

2. Deni linahesabika kuwa ni sehemu ya Deni la Taifa?

3.Mo akikopa China dhamana Serikali yetu,ukiogopa kukopa shauri yako.

4.Muda si mrefu tutasikia Richmond imekopa mdhamana Serikali,huku na huku kumbe Richmond kampuni ya mfukoni,basi ndugu zangu Serikali italipa tu.

Nimeshangaa sekta binafsi inakopa sana kuliko serikali. Sio kwamba serikali inajificha kwenye mgongo wa sekta binafsi?
 
Duh aisee yako mengi siyajui kumbe...sasa nauliza wenyewe wakikopa wanaweka nini bondi au ndo vitu walivyowekeza?ebu wataalam wa masuala ya uchumi tutoeni tongotongo
Mkuu 'Ndege JOHN', naomba hii elimu mpya kwako usiisahau. Binafsi nimejifunza pia, na ndio mwanzo wangu wa kuhoji mengi ninayoyaona kila siku yakifanyika na serikali yetu.
Itumie kutanua akili yako kujua mengi zaidi yanayofanyika huko ndani ya serikali yetu kwa manufaa ya watu wachache sana miongoni mwetu.

Hao hao wanaonufaika, mara nyingi hutugeuka na kulaani kwamba serikali haifanyi biashara, kumbe walishavimbiwa na fadhira walizofanyiwa na serikali hiyo hiyo.
Wengi wao kodi stahiki hawalipi, na ndio walio mbele kuchochea rushwa kila mahali.

Tumia elimu hiyo hiyo, kumkumbuka mkulima anayejipinda mgongo kila mwaka huko vijijini bila ya msaada wowote toka kwenye serikali yake. Ni hawa hawa wachuuzi wanaonufaika na hii mikopo wanaokwenda kumnyonga mkulima asifaidike na hicho kidogo alichokitolea jasho lake.

Lakini pia ngoja nikupe swali la kuhoji hiyo hiyo serikali: Hivi "sekta Binafsi" ni nani?
Huyu mkulima wa korosho hatambuliki kuwa mmoja wa sekta binafsi, kwa nini?
 
Hoja mbili hapa; hoja ya kwanza ni hii: deni la taifa = deni la umma + deni la makampuni binafsi. Deni la makampuni binafsi linatokana na makampuni hayo kukopa nje ya nchi sio ndani... Hapo imeeleweka. Hoja ya pili ni hii; ni makampuni gani yamekopa nje na kufanya deni hilo kuwa kubwa kiasi hicho? Hapa kuna wasiwasi kwamba kuna makampuni hewa yameingizwa na wahuni ili deni lihesabike kama deni la umma! Ufafanuzi hapa unahitajika
 
Mikopo binafsi nayo iko kama nilivyoeleza juu. Kuna wakati, serkali inaweza kupata mikopo kutekeleza miradi fulani katika nchi. Hii miradi mara nyingi inatekelezwa na sekta binafsi (na mashirika ya umma). Mwisho wa siku sekata binafsi hutakiwa kuilipa serkali na serkali kulipa huko ilikokopa. Nakumbuka katika miaka ya 80/90 serkali ilipata pesa nyingi toka (nadhani) benki ya dunia kufufua zao la mkonge. Hiyo pesa ilipewa sekta binafsi ili kufufua kilimo cha mkonge. Hiyo mikopo ilichukuliwa, wakapewa mashamba mkonge, lakini badala ya kufufua hicho kilimo hiyo fedha yote iliingizwa kwenye shughuli nyingine. Tena hiyo pesa walipewa kama foreignm currency credit facility. Wahindi wengi waliipokea hii pesa na wengine walikimbilia Cana/Uingereza na wengine hadi leo wako TZ na ni mabillionea na hiyo pesa hawakulipa.

Pesa kama hiyo hapo juu ni mkopo wa serkali hata kama mtumiaji ni mtu binafsi na huwezi ukajumlisha hela waliopewa sekata binafsi kama mkpo unaojitegemea.
Toa shule mkuu, wanafunzi tupo tayari kujifunza.
 
Mbona mimi nimemuelewa!...Yaani mfano mzuri ni huu let say deni la nyumba x=Sh 15 mpangaji namba 1 sh 5,mpangaji namba 2 ni sh 10,kila mpangaji atalipa deni linalomuhusu mwenyewe bila ya kujumlisha deni la mwenzie yaani ndio kama hivyo Serikali italipa deni lake na sekta binafsi italipa deni lake kwahiyo jumla ndio deni la taifa(deni la nchi ya Tz )
Uchumi wa nchi gani huo ,kwanza ulisoma uchumi kwwli au ndio nyie hkl mnakuwa wachambuz wa maswal ya uchumi na fedha
 
Back
Top Bottom