Mbona kama tatizo la wateja katika benki kupata noti pungufu wanapotoa hela linaota mizizi?

Okay! Hapa nimekupata.
 
Ile kudondosha noti ni taaluma kama taaluma kama nyingine, mwenye hela huwezi kuona inapodondoka ila utashuhudia mashine imehesabu kiasi kamili ambacho wewe umeona, lakini ukicheki kiasi ulichopewa unakuta pungufu.
Ni sawa na kuchezea karata tu ukizoea kuishi nazo.
 

Mmh..kwamba hadi ATM ZINAIBA????
 
Huko bulk cash room kuna kaunta pia.
Nishatoa pesa huko.
Hakuwi kama sebuleni.
Usimfikirie mtu usiyemjua unavyofikiri binafsi yako.
Sasa point yako nini? Kwamba bulk cash room hawajesabu hela wanakupa tu? Tusipoteze muda. Bottom line mteja ana haki na anatakiwa kuhesabu hela zake kabla ya kuondoka. Ziwe 50,000 au 50,000,000.
Ukiamua kuchukua hela bila kuhesabu usilalamike ukiibiwa umetaka mwenyewe.
 
We
Wenye pesa huwa hawahesabu noti ndugu.
Wakisha andika cheki pesa inaletwa nyumbani.
Wanaohesabu pesa ni sisi wenye vipesa kichele.
Benki kuna mabanda ya pesa yamesha hesabiwa na kufungwa na rubber bend.
 
Wengi wanaokumbana na hali hii sio wazoefu wa mipesa mingi, hivyo kwao kuhesabu hata (mil 1 tu) baada ya kuidraw kbl ya kueguza kisogo anaona tabu
 
We

Wenye pesa huwa hawahesabu noti ndugu.
Wakisha andika cheki pesa inaletwa nyumbani.
Wanaohesabu pesa ni sisi wenye vipesa kichele.
Benki kuna mabanda ya pesa yamesha hesabiwa na kufungwa na rubber bend.
Still sijui point yako ni nini. Uzi huu watu wanalalamika kuibiwa hela zao benki. Ndio hao matajiri wasiohesabu pesa? Okay nilijua ni masikini wenzangu ambao tunatakiwa kuhesabu pesa.
 
Chai hii
 
Nilikuwa nimeihesabu 7,000,000/- mara mbilimbili. Nikaenda ku-deposit pale CRDB Tunduma kule chini Customs. Wakanipiga laki.

Nikaja tena kupigwa 15,000/- CRDB Tegeta. Nilitoa 5,000,000/-wakanipa notes za 5,000/- nimeenda kuziweka NMB zikapelea. Na zilikuwa zimefungwa ile mikanda ya plastic.

Huu mtindo upo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…