Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Wakazi wa Lindi siyo consumer wazuri wa bidhaa lakini pia mkoa huu una watu wachache sana. Hivyo hauwezi kuwa kuvutia kibiashara kwa mtu yeyote anayetaka kuwekeza.
Lakini pia mkoa huu hauna mwingiliano wa wageni kutoka sehemu zingine hivyo population yake ni kama homogenous hivi haina kichocheo cha mabadiliko.
Kwa experience yangu mkoa wowote ukikuta hauna wachaga, wasukuma, wakinga, na waha ujue hauna fursa za kiuchumi.
Hayo makabila yanajua Kunusa fursa za uchumi kuliko panya Magawa Lindi haina hii sifa.
Hili ni kweli mkuu na ukitaka kujua umahiri wa mji, pita Tu mtaani uwaulize watafutaji ni mikoa ipi wanatamani kufika. Nina uhakika ni ngumu kuipata Lindi
Hata Mimi Lindi ni mkoa ambao hata kichwani haupo labda maisha yanipeleke. Ila kwa plan za kawaida Tu haipo.