Mh, sasa kumbuka kuwa Pwani ni sababu ya kizamani ya mji kukua, biashara siku hizi iko bara kuliko Pwani, Iringa kumbuka ndio njia kuu ya biashara kwenda Congo na Zambia, pia ni njia panda ya kwenda Mbeya, Morogoro na Dodoma, Lindi sasa yenyewe iko Pwani ndio, ila ukitoka hapo Lindi unaenda wapi tena kwenye mzunguko wa biashara.
Halafu pwani ishatwaliwa na miji kama Dar, kidogo na Tanga na Mtwara inakujakuja siku hizi, kumbuka Mtwara sio tu wana bandari kubwa pia wana njia kuu ya kwenda Songea na Mbeya na Malawi hivyo Mtwara ni kituo kikubwa cha biashara kuliko Lindi.
Hapo kwasababu za kushindani Lindi inapoteza taji kwa Mtwara