Kama wewe hujatekwa, kuuawa, Wala kutekwa maana yake waliotekwa, kuawa na kubakwa walikuwa na tabia zilizowasababishia watekwe, kuawa na kubakwa. Acha kutembea na wake za watu utabakwa na mwenye mke, acha kudhulumu watu watakuteka, acha kufuga fisi Wala watu utauawa na wananchi wenye hasira Kali.
Hata hivyo, mauaji na utekaji mwingine unafanywa na watu waliotumwa kuichafua nchi ili ionekane haifai kwa wawekezaji, watalii, kupewa misaada na kufanya biashara. Haya yote tunayafahamu.
Tunafahamu pia watekaji na wauaji ni watu wanaotaka kuonyesha kuwa Tanzania sio salama na maisha yao Yako hatarini ili waendelee kupatiwa hadhi ya ukimbizi na kupata faida ya ukimbizi kwenye nchi hizo.
Wengine ni watu wanaotafuta uhalali wa kupewa misaada ya kwenda Ikulu kuonyesha utawala haufai, na hii tunafahamu.