Mbona Peter Kibatala anahangaika kujua jina la mbwa badala ya mbwa mwenyewe aliyewàuma watu?

Mbona Peter Kibatala anahangaika kujua jina la mbwa badala ya mbwa mwenyewe aliyewàuma watu?

Kanisa limefunguliwa?
Jamaa nilikua napitia huu uzi wako na namna unavojibu watu, mkuu kiukweli hujui kujenga hoja na inaonesha una mihemko sana..
Pengine unaweza kua upo sahihi kwa baadhi ya mambo lakini jifunze kujenga hoja utaonekana smart sana...
 
Jamaa nilikua napitia huu uzi wako na namna unavojibu watu, mkuu kiukweli hujui kujenga hoja na inaonesha una mihemko sana..
Pengine unaweza kua upo sahihi kwa baadhi ya mambo lakini jifunze kujenga hoja utaonekana smart sana...
Kaka lazima watanzania wote tuujue ukweli ili tutafute njia za pamoja za kuijenga nchi yetu katikati ya dunia ambayo imejaa matatizo na vikwazo vingi sana. Wakati mwingine nchi haziendelei sio kwa ubovu wa Katiba na uzembe wa viongozi wake bali mifumo ya dunia ilivyosukwa na nchi zilizoendelea. Nchi hizí zinapanga bei za mazao yetu na bei za mazao yao pia wakati wa kuuza na kununua. Nchi hizi zimelazimisha Dunia yooote iuze na kununua kwa kutumia sarafu zao za Dola, Euro na Pound baasi.

Tanzania tumeachiwa Katiba mbaya au nzuri na Mwl Nyerere ambayo imetumiwa na Marais wote mpaka sasa. Katiba hii imetupatia Rais mwanamke kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi yetu na ukanda mzima wa East Africa na Sadc. Kuwa na Rais mwanamke hakujazoeleka hata Marekani wameyakataa mazoea hayo mpaka Sasa.

Baada ya Katiba hii kutupatia Rais mwanamke tulipaswa sote tumsaidie atuvushe salama kwenye kipindi chake maana inafahamika kuwa wanawake wakoje katika nyakati tofautitofauti za furaha, huzuni, wanaposifiwa, wanapokaumiwa, wanapotukanwa na kubezwa, wanapoweza na wanaposhindwa.

Kuna watu wenzetu ambao wanataka Rais huyu wa majaribio Africa awe uchochoro wao wa kupata Yale yooote ambayo walishindwa kuayapata wakati wa Nyerere, Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli hata ikibidi kwa nguvu.

Sisi watanzania wegine akiwemo mm ndiyo tunajiuliza kwanini hivi? Kwanini Sasa?. Je, ni expiry date ya Katiba ya Nyerere imefika wakati wa Samia? Je , ni kwasababu Rais ni mwanamke? Je, Rais huyu mwanamke ameharibu sana kuliko wale wengine 5 waliomtangulia, ameharibu nini?
 
Afrika Ina rasilimali nyingi lakini haina technology ya kuivuna na masoko ya haki ya kuiuzia. Ina viongozi wengi vibaraka wa mataifa mengine wanaoingizwa kwa njia kuu nne; demokrasia, mapinduzi, vita ya wenyewe kwa wenyewe na kupandikizwa baada ya kiongozi wa wananchi kuondolewa na mataifa ya nne. Njia zao kuu ni kuwachonganisha wananchi na kiongozi wao mzalendo kwa kutumia vikwazo, propaganda kupitia radio zao za BBC, DW, VOA na France 24, vyama vya upinzani na makanisa/Misikitii.

Kama mm mtu dhaifu najua hili unadhani serikali husika hazijui? Ndio maana Afrika kusikia mtu katekwa, kapigwa, kuawa au kafunguliwa mashitaka yasiyokuwa na kichwa Wala miguu ni jambo la kawaida sana. Ni kweli kabisa Kuna watu waafrika wenzetu wanaotumiwa na nchi za kigeni kutuibia na kuhatarisha usalama wa viongozi waliko madarakani.
Kama waliopo ni wazarendo mbona hawafanyii kazi report ya CAG mbona document za ufisadi zinavuja na waliotajwa hakuna hatua na walio vujisha ni watanzania,mbona hataki kukosolewa na watanzania,mbona hao wazungu ndo anaongoza kuwakopa?,
 
Kama waliopo ni wazarendo mbona hawafanyii kazi report ya CAG mbona document za ufisadi zinavuja na waliotajwa hakuna hatua na walio vujisha ni watanzania,mbona hataki kukosolewa na watanzania,mbona hao wazungu ndo anaongoza kuwakopa?,
Hueleweki. Kwani report za CAG ni mara ya kwanza kuzisikia kwenye awamu ya mama Samia? Magufuli alidiriki kumfukuza na CAG mwenyewe, Prof. Assad mbona ripoti ya CAG iwe ni sababu wakati wa Samia tu. Shida hapo ni Samia au wabunge wenu wanaogonga meza kwa Kila jambo.

Mimi nilifurahia sana wagombea wa upinzani kuenguliwa mapema kabla hawajatusababishia gharama za kuendesha chaguzi ndogo baada ya wao kuhamia CCM kuunga juhudi. Wote tumeshuhudia wabunge wa upinzani wakirudi CCM na kulazimika kuchagua tena kwa gharama mpya. Kama hata Peter msingwa, Nasari, mtulia, tumbili, mkumbo nk wameenda CCM huwezi kujua nani hatarudi CCM. Bora waenguliwe tu mapema.
 
Hoja ya Wakili msomi Peter Kibatala kuwa jina la kanisa kwenye barua liyotumika kulifunga kanisa la Gwajima ni tofauti na jina la kanisa la Gwajima lililopo kwenye usajili, hivyo kulifunga kanisa la Gwajima ni makosa, Hoja kama hii ni nyepesi sana kwa mtu ambae anafahamika (raia, mbunge na askofu) ameonekana kwa macho na kusikika kwa masikio akimtweza Rais wa Tanzania na Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote Tanzania. Yaani mbwa kichaa anaeuma watu watu wanajua , wamemuona na kumsikia akibweka wakati anauma watu lakini eti Kibatala anasema watu wasimuue mbwa huyo kichaa kwakuwa hawalijui jina lake kamili kwa usahihi.

Hoja nyepesi sana hii kwa mtu anaemdhihaki Mkuu wa nchi na Amirijeshi Mkuu, maana barua iliandikwa na kupelekwa kwa mtu anaefahamika sana na kanisa linalofahamika sana, na polisi waliokwenda kulifunga walienda sehemu wanayoifamu sana. Sidhani kama hoja hii ya Wakili ina mashiko ya kuzuia kanisa la Gwajima lisifungiwe kwasababu ya utofauti wa majina kamili kwenye barua.
Tz Ina ma-jinga mengi sana. wewe uko top ten
 
Mara vuuuuupuuuu!!!! Gwajima mungu kamjalia kawa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Baada ya miezi 7 tu ya kuwepo madarakani anapata khabari kuwa kuna mtu kanya mavi kwenye madhabahu ya kanisa la ufufuo na uzima, huku akitamba kuwa ametumia demokrasia yake katika kujisaidia, huku wenzake wanaomuunga mkono wakidai atoke kwanza sio mkatoliki, Anglican wala Mluteri, ni mfupi mno kama stuli hafai kuwa Rais. Kwenye barabarani anasikia kuna maandamano ya wanajeshi wanataka mishahara ya 5m kima cha chini na malupulupu yao, na walimu wamegoma kufundisha nchi nzima wanataka 2M mishahara yao kima cha chini. Rais Gwajima angefanya nini?

Je, angefanya tofauti na ambavyo angefanya Rais mwingine?
 
Back
Top Bottom