Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Hata dot zikiwa connected huwezi pata connection kati ya kuanika kufuli na kuhama... Kwani kuhama mchana hayo makufuli si yanawekwa kwenye mabegi au makabati..??!! AU ANAYEHAMA USIKU MAKUFULI YAKE ANAYAWEKA PALE PANAPOBANDIKWA ROAD LICENCE..??Kulinda "privacy".
Mama'ko anaanika kufuli zake uani?
Unakuta mtu unahama na mkokoteni mara masufuria yanaanguka kule huku jiko la mchina linamwaga mafutataa linaharibu vitu vingine kqdhalika vijiko vinaanguka kah!!
Ukicheki hapo ni baba na familia mko na mkokoteni mnaongozana nao pamoja na vitoto vingine vinalia chwiii chwiii ....!!!!!
Kuna sababu nyingi za kuhama usiku,mojawapo ni hizi:
1.Kuficha udhaifu wa mhamaji(kujistiri),ama kuepuka fedheha.
2.Sababu za kiusalama.
3.Hulka ya kutopenda kujulikana(kueji-expose
kwa watu)
Hakuna lolote.. Sawasawa na mkienda bar kupata vya bar, mwenye nokia tochi kuiweka mezani ni ngumu.. Labda aiweke juu ya S6 iliyoko juu ya meza, lakini kuiweka peke yake ni ngumu sana..Mchana ni macho ya watu na usumbufu wa foleni..na usiku stara zaidi wapangaji wenzako wakustukie asubuhi..!
Mkuu naomba kutokubalia na wewe kwenye maelezo yako....
1.Kuficha udhaifu wa mhamaji(kujistiri),ama kuepuka fedheha.
Udhaifu kama mtu anao, hauwezi kujulikana kwa siku moja tu, tena siku ya kuhama. Halafu kama unajikubali huweizi kuogopa udhaifu wako... ni sawa na kukimbia kivuli chako jua likiwaka tu unakiona.
2.Sababu za kiusalama.
Nilidhani kuhama mchana ndo salama zaidi... Unahama usiku kwa kuhofia usalama..??!! Ni nini hicho kinachopelekea kuhama usiku kuwe salama kuliko kuhama mchana..??!!
3.Hulka ya kutopenda kujulikana(kueji-expose kwa watu)
Hii inafanana na ya kwanza....
NB: Kwa nijuwa mimi
1. Kuhama usiku ni kuogopa makorokocho yako yanayofanana na dampo kuonekana... Kumbukeni wengine wananunua vitu kule mali mbovu
2. Kuhama usiku inawezekana unanunua vitu vya wizi tu kwenye mavitu yako. Hivyo usije ukaonwa na wenye vitu vyao
Hayo ni mawazo yako mkuu, na upo sahihi kwa mtazamo wako pia.
Jambo lingine la kufikiri, ni kwa nini pia vituo vya polisi/silaha za kivita mara nyingi huhamishwa usiku?
Mkuu, kwenye comparison huwa tunakompea ''epo'' na ''epo'' ....... Unapolinganisha kuhamisha silaha ya kivita na kuhamisha vifaa vya ndani kama sahani, bakuli vikombe , makabati pamoja na mende wake, vitanda pamoja na kunguni wake.... etc... sikuelewi
Kulinda "privacy".
Mama'ko anaanika kufuli zake uani?
Godoro jeusi tii utalihamisha vipi mchana mkuu
Panya akidondokaje wakati nipo kwenye foleni?
Bora kungekuwa hamna foleni unapitatuu vuuuuuuu.
weng wanaogopa kuni ( ferniture) kuonekana