Mkuu naomba kutokubalia na wewe kwenye maelezo yako....
1.Kuficha udhaifu wa mhamaji(kujistiri),ama kuepuka fedheha.
Udhaifu kama mtu anao, hauwezi kujulikana kwa siku moja tu, tena siku ya kuhama. Halafu kama unajikubali huweizi kuogopa udhaifu wako... ni sawa na kukimbia kivuli chako jua likiwaka tu unakiona.
2.Sababu za kiusalama.
Nilidhani kuhama mchana ndo salama zaidi... Unahama usiku kwa kuhofia usalama..??!! Ni nini hicho kinachopelekea kuhama usiku kuwe salama kuliko kuhama mchana..??!!
3.Hulka ya kutopenda kujulikana(kueji-expose kwa watu)
Hii inafanana na ya kwanza....
NB: Kwa nijuwa mimi
1. Kuhama usiku ni kuogopa makorokocho yako yanayofanana na dampo kuonekana... Kumbukeni wengine wananunua vitu kule mali mbovu
2. Kuhama usiku inawezekana unanunua vitu vya wizi tu kwenye mavitu yako. Hivyo usije ukaonwa na wenye vitu vyao