Mbowe akiri kuukubali "mziki" wa Rais Samia, agomea wana-Chadema kuingia barabarani, asema ni mihemko

Mama anakuza siasa za kistaarabu, kuingia barabarani kipindi hiki cha neema kwa taifa ni upuuzi.
 
Mkuu ukiwa kiongozi lazima uwe flexible, huwezi expect kutumia mbinu zile zile ushinde. Tumekuwa radical tokea 2000 ila Serikali haikuwahi tenda haki Sasa tumeamua kuwa diplomatic na Serikali inakubali mazungumzo naona ni njia nzuri.

Kwanini tuingie barabarani ilihali mezani tunaweza pata suluhu? Umeona Kenya, Odinga kaamua kutumia meza kuupata urais na imezaa matunda atapelekwa Ikulu Hata kwa wizi wa kura!! so nadhani path tuliyochukua sio mbaya tusubiri matokeo tukiona hayazai matunda obviously tutarudi Ground kujipanga upya
 
Mkuu kwani haiba ya chadema ni kuingia barabarani? Mbona vijana wa chadema mnaonekana ni watu wenye hasira hasira na mmekaa kishari sana? Akitokea mtu akataka siasa za kistaarabu kwenu nyie ni msaliti au kanunuliwa embu jifunzeni kwa wenzenu Ghana.
 
Mama hana uadui na Watanzania, tunaunga mkono jitihada zake kutuanganisha. Madui wa mama wamo ndani ya ccm .
 
Njia sahihi ya kupambana kisiasa baad ya minyukano na majeraha ni Dialogue
 
Chairman ameongea UKWELI Mama ameleta maelewano na mshikamano.
 
It may be, narudia; it may be, kulikuwa na mazungumzo ya background na ya siri kati yake na rais Samia, na kuna mambo walipanga na kukubaliana na hawataki baadhi ya watu wayajue kwa sasa, kwa sababu maalum! Hii sababu maalum inaweza kuwa inahusiana na ''traces'' alizoacha mwendazake ambazo zinahitaji muda na ''ujasusi'' maalum kuzi-overcome!
 
Samia mjanja si amempa hela Tundu Lissu! CDM kwisha
 
Acha uzwazwa Lissu alipoitisha maandamano mlijitokeza? Alipokuwa gerezani mlijitokeza kuandamana, ameona njia ya shali mnamuangusha Bora atumie dialogue

Alipoitisha maandamano watu hawakuandamana sio kwa sababu hawakuona umuhimu bali uoga ulitawala. Alipokuwa gerezani hakuna aliyejitokeza kuandamana kwani kesi ilikuwa inaendelea. Kuandamana huwa inatokea automatically baada ya watu kufukia hatua ya mwisho ya uvumilivu, na sio lazima itokee siku Lisu au Mbowe ametangaza. Labda useme kuwa yeye alikamatwa akiwa tayari mstari wa mbele kwenye maandamano, na watu hawakutokea, sio yeye kaaigiza kisha anasubiri watu watokee.
 
Wewe unapinga msimamo wao lakini wakiitisha maandamano hujitokez,wakipigwa risasi, kufilisiwa, fungwa jera, we unakuw keyboard worriors tu, acha wafate njia nyingine maaana nyie Ni mangombe tu

Kwani walivyokuwa wakienda bungeni nilikuwa naenda nao, mpaka useme walipoitisha maandamano sikutokea? Kwa taarifa yako hapa nilipo nina kovu la jeraha kwa ajili ya maandamano hayo ya CDM. Sasa ufahamu kila jambo lina timing yake. Huko kwenye maandamano tulikuwa tunaelekea, ilihitajika uvumilivu fulani.
 
Kipindi hicho Asali ilikua haipo upande wake
 

Sipingi maelezo yako mazuri, Odinga aliingia kwenye mazungumzo kwa kuombwa na Kenyatta na sio kinyume chake. Hapa kwetu viongozi wa CDM ndio wanajinyenyekeza kwa serikali. Matokeo yake watapoteza imani yetu kwao sisi wafuasi wao, siku wakirudi baada ya kukwama, watakuta hatuna imani nao. Haya mazungumzo ni utashi wa Samia kama yeye, akitoka mchezo unarudi hapo hapo.

Tazama Samia bado yuko madarakani lakini wapinzani hawapewi mazingira mazuri ya kufanya siasa. Samia anawatumia viongozi wa CDM kuhakikisha hakutani na ugumu kwenye utawala wake, lakini sioni kama anaweza kuleta mabadiliko yoyote ya maana. Kwenye meza ya mazungumzo inabidi muende wote mkiona umuhimu huo, na sio kinyume chake.
 
Mkuu kwani haiba ya chadema ni kuingia barabarani? Mbona vijana wa chadema mnaonekana ni watu wenye hasira hasira na mmekaa kishari sana? Akitokea mtu akataka siasa za kistaarabu kwenu nyie ni msaliti au kanunuliwa embu jifunzeni kwa wenzenu Ghana.

Usichanganye siasa za kistaarabu na ukondoo boss.
 
Nimekupata
 
Kwa hiyo nyie mnasubiri huruma ya CCM mmuingie madarakani?
 
Acha uzwazwa Lissu alipoitisha maandamano mlijitokeza? Alipokuwa gerezani mlijitokeza kuandamana, ameona njia ya shali mnamuangusha Bora atumie dialogue
Ile ni kazi yake
 
Wewe unapinga msimamo wao lakini wakiitisha maandamano hujitokez,wakipigwa risasi, kufilisiwa, fungwa jera, we unakuw keyboard worriors tu, acha wafate njia nyingine maaana nyie Ni mangombe tu
Kwani kunamtu kamuajili kuwapigania wa Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…