DOKEZO Mbowe anakwenda kupewa nafasi nyeti ili kuyalinda maridhiano

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ungemalizia pia na
Mungu mlinde kiongozi shupavu
Mbowe.
Ingeleta ukweli wa andiko Laki.

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
 
Ungemalizia pia na
Mungu mlinde kiongozi shupavu
Mbowe.
Ingeleta ukweli wa andiko Laki.

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
Nimeandika Mungu ailinde nchi yetu na kila mwananchi aliepo ndani ya mipaka ya nchi yetu. Sasa wewe unafikiri kuwa Mbowe hayupo ndani ya mipaka ya nchi yetu?
 
Mbowe ameshakuwa SEFU new model. Hapa ni mwendo wa kutuigizia mapambano ya kudai haki huku yeye anaingiziwa mabilioni kila mwaka.

Sufuri kabisa.
Hahaha mbona jitihada zake zimesaidia kuleta maridhiano ya kisiasa mkuu.
 
Kwani upinzani ni minyukano au ugomvi? nyie watu vipi? Basimkama Tanzania hakuna upinzani anzisha wewe chama chako tuone ni vipi utakuwa mpinzani bora kuliko Mbowe au Zitto Kabwe
Umemwambia kweli kabisa. Siasa za vurugu siku hizi hazina nafasi ndani ya nchi yetu.
 
Hili tulishalidokeza siku nyingi; labda tu ni kwa vile haikuanzishwa kama mada.

Dalili zote zinaonyesha kwamba siasa za Kenya ndizo zinazokuja kujaribiwa Tanzania.
Ni kama Tanzania siku hizi inaiga kila kitu kinachofanyika Kenya; iwe ukulima wa parachichi, nasi tunakimbilia kuiga; kuzungumza kiingereza, nasi tunataka tuwe kama wao. Wakisema wao wanawatambua 'diaspora' wao kwa kiwango fulani, nasi tunatafuta kuhimiza watu wetu watoke kwenda nje;, kana kwamba hapa kwetu hakuna fursavtele ambazo vijana wetu hawa wanaweza kuzitumia kujenga taifa lao kwa ufanisi.

Tumekuwa watu wa kuiga tu kila kitu, hatuna ubunifu wowote tunaoweza kujivunia...; la hasha; nisisahau Kiswahili chetu na taasisi yetu iliyofanya kazi nzuri sana BAKITA.

Nje ya hapo, ninaomba kukumbushwa eneo jingine tunaloweza kujivunia katika kulifanya vizuri.

Lakini naomba usinitajie udumu wa CCM kwenye madaraka, kama mfano.
 
Ndo maana mie mwenzenu haya mambo ya siasa siyatoleagi macho kivile,, mpinzani wa kweli bongo hayupo, narudia tena hayupo, wote wanatafuta vyeo(ulaji) kwa ajili ya wao na familia zao, rejea kwa Edward lowasa, tambwe hiza, dokta mashinji, etc.
Kwahiyo kwa hizo akili zako kabisa umekubaliana na huyu kenge alieleta huu uzi?
 
Duh!

Umeandika mkuu 'The Palm Beach', nami kwa kiasi kikubwa ningekubaliana nawe kumhusu Mbowe, hadi alipoingia Samia!

Mbowe, mbele ya Samia ameyeyuka!

Hebu nieleze kiuhakika: Kisiasa Mbowe na Samia wanatofautiana vipi?

Mbowe na chama chake wanatofautiana kwa lipi, ambalo Samia hakubaliani nao?
Kazi kubwa iliyobakia sasa ni kwa Samia kulizima kundi lililoko CCM linalotofautiana naye. Akimaliza kazi hiyo, CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe hawatakuwa na tofauti yoyote.

Ni kazi rahisi tu, baada ya hapo, kueleza watu kwamba wamekubaliana kuwa pamoja, na stori ndefu ndefu sana za kulaza usingizi watu.

Huko CHADEMA ninayeweza kuona shida juu yake kukubaliana na msimamo huo ni Lissu, na pengine Heche.

Wengine wote watapiga vigelegele kuelekea kwenye umoja wao wa CCM ya Samia, na CHADEMA ya Mbowe.

Akina Kabwe wao tayari wapo huko CCM ya Samia.
 
Huwezi kunikalisha kimya wewe kama nani,, au imekuuma kusema hakuna mpinzani wa kweli,, ndio wote janja janja wanatufuta vyeo na wale na familia zao,, mfano dokta mashinji, nusrat hanje, Edward lowasa, tambwe hiza, etc.
Sasa hao unataka kuwafananisha na Mh Mbowe?
 
Hahaha Slaa alikwepa kumpigia deki Lowasa kwenye barabara ili apite kama walivyofanya viongozi wengine.
Hapo ndio ninapoona huu uzi wako umeuleta kama umbea tuu[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Pumba tupu umeandika hapa[emoji706][emoji706][emoji706],sijui hata nilitaka nin?,ila hii hoja yako ni mfu
 
Umejenga hoja vizur ila hiyo aya hapo mwisho umeharibu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…