DOKEZO Mbowe anakwenda kupewa nafasi nyeti ili kuyalinda maridhiano

DOKEZO Mbowe anakwenda kupewa nafasi nyeti ili kuyalinda maridhiano

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari zenu wana JF wenzangu, natumai kila mtu ana afya tele.

Kwa dokezo lililonifikia kutoka kwa mtu ambae siwezi kumtaja, ni kwamba mama anamuandalia kamanda Mbowe nafasi nyeti na muhimu ndani ya serikali yake ili kujenga serikali yenye sura na mtazamo wa kitaifa.

Ikumbukwe kwamba raisi Samia aliwahi kunukuliwa akitamka mwenyewe kwamba serikali yake anayoiunda angependa kuona anashirikiana na wanasiasa wa vyama vingine vya siasa, ili kutengeneza serikali ya kitaifa ambayo haiegemei upande wowote wa chama.

Na katika hili raisi ameanza kuonesha njia kwa kujiweka mbali na siasa za majitaka, ambazo zimekuwa zikiwafaidisha wapuuzi wachache waliopo ndani na nje ya chama chake.

Mungu ilinde Tanzania yetu
Mungu mlinde raisi wetu
Mungu ilinde amani yetu
na kila aliepo ndani ya nchi yetu
Ameen [emoji2969][emoji2969][emoji2969]
Ungemalizia pia na
Mungu mlinde kiongozi shupavu
Mbowe.
Ingeleta ukweli wa andiko Laki.

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
 
Ungemalizia pia na
Mungu mlinde kiongozi shupavu
Mbowe.
Ingeleta ukweli wa andiko Laki.

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
Nimeandika Mungu ailinde nchi yetu na kila mwananchi aliepo ndani ya mipaka ya nchi yetu. Sasa wewe unafikiri kuwa Mbowe hayupo ndani ya mipaka ya nchi yetu?
 
Mbowe ameshakuwa SEFU new model. Hapa ni mwendo wa kutuigizia mapambano ya kudai haki huku yeye anaingiziwa mabilioni kila mwaka.

Sufuri kabisa.
Hahaha mbona jitihada zake zimesaidia kuleta maridhiano ya kisiasa mkuu.
 
Kwani upinzani ni minyukano au ugomvi? nyie watu vipi? Basimkama Tanzania hakuna upinzani anzisha wewe chama chako tuone ni vipi utakuwa mpinzani bora kuliko Mbowe au Zitto Kabwe
Umemwambia kweli kabisa. Siasa za vurugu siku hizi hazina nafasi ndani ya nchi yetu.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, natumai kila mtu ana afya tele.

Kwa dokezo lililonifikia kutoka kwa mtu ambae siwezi kumtaja, ni kwamba mama anamuandalia kamanda Mbowe nafasi nyeti na muhimu ndani ya serikali yake ili kujenga serikali yenye sura na mtazamo wa kitaifa.

Ikumbukwe kwamba raisi Samia aliwahi kunukuliwa akitamka mwenyewe kwamba serikali yake anayoiunda angependa kuona anashirikiana na wanasiasa wa vyama vingine vya siasa, ili kutengeneza serikali ya kitaifa ambayo haiegemei upande wowote wa chama.

Na katika hili raisi ameanza kuonesha njia kwa kujiweka mbali na siasa za majitaka, ambazo zimekuwa zikiwafaidisha wapuuzi wachache waliopo ndani na nje ya chama chake.

Mungu ilinde Tanzania yetu
Mungu mlinde raisi wetu
Mungu ilinde amani yetu
na kila aliepo ndani ya nchi yetu
Ameen 🤲🤲🤲
Hili tulishalidokeza siku nyingi; labda tu ni kwa vile haikuanzishwa kama mada.

Dalili zote zinaonyesha kwamba siasa za Kenya ndizo zinazokuja kujaribiwa Tanzania.
Ni kama Tanzania siku hizi inaiga kila kitu kinachofanyika Kenya; iwe ukulima wa parachichi, nasi tunakimbilia kuiga; kuzungumza kiingereza, nasi tunataka tuwe kama wao. Wakisema wao wanawatambua 'diaspora' wao kwa kiwango fulani, nasi tunatafuta kuhimiza watu wetu watoke kwenda nje;, kana kwamba hapa kwetu hakuna fursavtele ambazo vijana wetu hawa wanaweza kuzitumia kujenga taifa lao kwa ufanisi.

Tumekuwa watu wa kuiga tu kila kitu, hatuna ubunifu wowote tunaoweza kujivunia...; la hasha; nisisahau Kiswahili chetu na taasisi yetu iliyofanya kazi nzuri sana BAKITA.

Nje ya hapo, ninaomba kukumbushwa eneo jingine tunaloweza kujivunia katika kulifanya vizuri.

Lakini naomba usinitajie udumu wa CCM kwenye madaraka, kama mfano.
 
Ndo maana mie mwenzenu haya mambo ya siasa siyatoleagi macho kivile,, mpinzani wa kweli bongo hayupo, narudia tena hayupo, wote wanatafuta vyeo(ulaji) kwa ajili ya wao na familia zao, rejea kwa Edward lowasa, tambwe hiza, dokta mashinji, etc.
Kwahiyo kwa hizo akili zako kabisa umekubaliana na huyu kenge alieleta huu uzi?
 
Hujui kuota wewe...!

Humjui Freeman Mbowe wewe...!

Huyo hawezi kuuza utu wake Kwa shekeli otherwise angeshavutaga hela nyingi miaka mingi iliyopita...

Labda hujui tu. Kwa taarifa yako Iko hivi;

✓ John P. Magufuli alikuwa tayari kumpa Freeman Mbowe hata Uwaziri Mkuu (u - PM) ili mradi aiue CHADEMA lakini FM hakuweza kuuza utu wake...

✓ John P. Magufuli alikuwa hata tayari ampe hazina yote ya nchi hii ili mradi aiue CHADEMA, lakini FM hakuweza kuuza utu wake...

✓ Ndiyo maana jamaa (JPM) alipoona amemshindwa kumnasa kwenye hayo, akaamua kujaribu kuivuruga CHADEMA kwa nunua nunua ya wabunge na madiwani nchi nzima, lakini hata hiyo, Mwamba hakutikisika wala Kununa...

✓ Na mwisho wa siku akamsukia Zengwe la kumbambikia likesi la kijinga la ugaidi ambalo nalo lili-backfire hatari kwa kishindo na kwa aibu kubwa kwa waliosuka uhuni huo...

NOTE: Tanzania hii wapo viongozi wawili tu wa vyama vya siasa (vya upinzani) WASIONUNULIKA lakini wakati huohuo hawa ndo sumu ya CCM na serikali yao...

Hawa ni FREEMAN MBOWE (FM) na TUNDU LISSU (TL). Hawa kuwadhibiti ni aidha uwaue tu au watafutie uraia wa Burundi kwa Mwigulu Nchemba...!!!
Duh!

Umeandika mkuu 'The Palm Beach', nami kwa kiasi kikubwa ningekubaliana nawe kumhusu Mbowe, hadi alipoingia Samia!

Mbowe, mbele ya Samia ameyeyuka!

Hebu nieleze kiuhakika: Kisiasa Mbowe na Samia wanatofautiana vipi?

Mbowe na chama chake wanatofautiana kwa lipi, ambalo Samia hakubaliani nao?
Kazi kubwa iliyobakia sasa ni kwa Samia kulizima kundi lililoko CCM linalotofautiana naye. Akimaliza kazi hiyo, CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe hawatakuwa na tofauti yoyote.

Ni kazi rahisi tu, baada ya hapo, kueleza watu kwamba wamekubaliana kuwa pamoja, na stori ndefu ndefu sana za kulaza usingizi watu.

Huko CHADEMA ninayeweza kuona shida juu yake kukubaliana na msimamo huo ni Lissu, na pengine Heche.

Wengine wote watapiga vigelegele kuelekea kwenye umoja wao wa CCM ya Samia, na CHADEMA ya Mbowe.

Akina Kabwe wao tayari wapo huko CCM ya Samia.
 
Huwezi kunikalisha kimya wewe kama nani,, au imekuuma kusema hakuna mpinzani wa kweli,, ndio wote janja janja wanatufuta vyeo na wale na familia zao,, mfano dokta mashinji, nusrat hanje, Edward lowasa, tambwe hiza, etc.
Sasa hao unataka kuwafananisha na Mh Mbowe?
 
Hahaha Slaa alikwepa kumpigia deki Lowasa kwenye barabara ili apite kama walivyofanya viongozi wengine.
Hapo ndio ninapoona huu uzi wako umeuleta kama umbea tuu[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Mkuu hakuna anaetosheka na hela(vyeo) we ujiulizi, kwani museveni kaguta ana njaa gani lkn mbona hataki kuachia madaraka!! Na je kagame? We ujiulizi siku hizi huyo mbowe misele ya kwa bi mdashi haiishi pale jengo jeupe,, kifupi hawa wanasiasa sio watu wakuendekeza sana kiasi kwamba mpaka umchukie mwingine,, muhimu kukaza kwenye shughuli zetu zinazotupatia riziki kama mi mwenzio nilivyoboresha kazi yangu ya udalali.
Pumba tupu umeandika hapa[emoji706][emoji706][emoji706],sijui hata nilitaka nin?,ila hii hoja yako ni mfu
 
Mbowe hana mkakati wa kugombea urais yeye kama yeye; ana mkakati wa kutoa Rais kutoka kwenye chama chake, yeye akiwa pembeni. Alishasema kuwa 2025 hatasimamisha mgombea, maana yake ni kwamba atajikita zaidi katika kutafuta wabunge. CCM wasipojiandaa vizuri 2025, idadi ya wabunge kati yao na CHADEMA itakuwa 50 by 50; na bado kuna ACT wazalendo nayo imeshakuja juu.
Njia wanayoweza kutumia CCM kumdhoofisha Mbowe, ni kuhakikisha kuwa wananzisha chama kingine kwa kivuli cha upinzani ambacho hata ikitokea mambo yakawa magumu 2030, wanahamia huko kisirisiri. CCM wao ndiyo wanatakiwa kuandaa chama ambacho watakuja kuwa tayari kukiachia madaraka. Mpaka muda huu, bado hatujawa na chama pinzani chenye uwezo wa kushika dola kwa usahihi kama wao
Umejenga hoja vizur ila hiyo aya hapo mwisho umeharibu kabisa
 
Back
Top Bottom