THE BIG SHOW ,
..Natofautiana na wewe unapohusisha harakati za Chadema kudai Katiba mpa na suala la IMANI ya Rais Samia Suluhu pamoja na JINSIA yake.
..Kilichotokea kati ya Rais Samia Suluhu na uongozi wa Chadema ni kupishana kwa mitizamo yao kuhusu muda gani ni sahihi kwa suala la Katiba mpya kushughulikiwa.
..sisi tunaowafuatilia viongozi hawa, tunapaswa kupima kauli na misimamo iliyotolewa na kila upande, na kuangali upande upi umejenga hoja iliyo sahihi.
..Binafsi sijakubaliana na hoja ya Rais Samia Suluhu ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Zuio hilo linakwenda kinyume cha katiba na sheria zetu.
..Pia sijashawishika na hoja ya Rais Samia Suluhu kwamba wabunge peke yao ndio wanaoruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Uamuzi huo ukitekelezwa utakipendelea chama cha Raisi, CCM, na kuvikandamiza vyama vingine vya siasa.
..Vyama vya upinzani huku Tanganyika vina mbunge ktk jimbo moja tu, hivyo CCM watafanya mikutano ktk majimbo zaidi ya 200++ nchi nzima, huku Chadema wakifanya mikutano katika jimbo moja tu.
..Kwa upande mwingine nadhani Mh.Mbowe anakosea anapolalamika, au kulazimisha, Rais akutane na Chadema. Kama Rais anaamini muda haujafika wa kuonana na Chadema basi wamuache aendelee na ratiba na majukumu yake aliyojipangia.
..Kila upande hapa uendelee na shughuli, ratiba, na mipango yake. Raisi Samia Suluhu aendelee kurekebisha uchumi kama alivyoahidi. Chadema nao waendelee na operation yao ya kuelimisha kuhusu Katiba mpya, na wasibugudhiwe na mtu au chombo chochote.
..Rais Samia Suluhu akirekebisha uchumi Watz wote tutafaidika. Chadema nao wakihamasisha kuhusu Katiba bora umma mzima utafaidika.