Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Mbowe hakwamishi jitihada za watanzania kujikomboa. Watanzania wenyewe ndio wanajichelewesha.
Mnataka ajipeleke kichwa kichwa ili aliwe kichwa huku nyie mkichekelea nyuma ya keyboard sio? Mlikuwa wapi wakati anasota rumande? Mlikuwa wapi wakati biashara zake zikifungiwa? Mlikuwa wapi wakati mashamba yake yakifyekwa? Mlikuwa wapi wakati majengo yake yakivunjwa? Mlikuwa wapi wakati accounts zake zikiwa freezed kwa amri ya Magufuli?
 
Huu uzi umeletwa kwa hisani ya Lumumba FC na kufadhiliwa na chawa ambao wamejipanga kuleta mashambulizi hatari kweli kweli
 

..Kinachoendelea ni juhudi za kuidhoofisha Chadema.

..Kuna watu hawajafurahishwa na taarifa kwamba Chadema inaelekea kanda ya Nyasa kufanya mikutano na wananchi.
 
..Kinachoendelea ni juhudi za kuidhoofisha Chadema.

..Kuna watu hawajafurahishwa na taarifa kwamba Chadema inaelekea kanda ya Nyasa kufanya mikutano na wananchi.

Chadema imepinga hadharani jitihada za wananchi zilizokuwa zinashika kasi kupinga biashara ya bandari na kudai katiba mpya.

Tatizo ni hilo tu.

Mbaya zaidi ni kuwa kwa kujua au kutokujua, imefanya hivyo kwa niaba ya CCM.
 
Huu uzi umeletwa kwa hisani ya Lumumba FC na kufadhiliwa na chawa ambao wamejipanga kuleta mashambulizi hatari kweli kweli

Mtaitana majina hadi mmalize misamiati yote.

"Mwingine naye akisema huu uzi unapingwa kwa hisani ya Lumumba FC na kufadhiliwa na chawa ambao wamejipanga kuleta mashambulizi hatari kweli kweli."

Hapo napo utasema je?
 
Chadema imepinga hadharani jitihada za wananchi zilizokuwa zinashika kasi kupinga biashara ya bandari na kudai katiba mpya.

Tatizo ni hilo tu.

Mbaya zaidi ni kuwa kwa kujua au kutokujua, imefanya hivyo kwa niaba ya CCM.

..Hapana.

..Hakuna kiongozi wa Chadema aliyeunga mkono bandari kuuzwa, au mchakato wa katiba kusitishwa au kucheleweshwa.

..Na kwa uelewa wangu Chadema wamefanya mikutano mingi na maeneo mengi kuzungumza na wananchi kuhusu hoja hizo.

..Kwanini tunawakatisha tamaa? Kwanini tunawalaumu? Kwanini tunawazodoa? Tunafanya hivyo kwa faida ya nani?
 
Mbowe is just talking, talking, talking. Na kuongea anajua sana, kipaji cha kupiga tantalalia anajua.

Sasa tunataka kwenda beyond sweet talk. Tunataka action. Na ufortunately Mbowe kasukuma kete ya utengano , ambayo inakwaza azma ya wananchi eventually kuraise up na kulisongesha kitaa.

Mbowe anataka siasa za kishostishisti, na CCM hizo ndo siasa wanazozitaka!
 
Mkuu Missile of the Nation , hili nililizungumza hapa Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu? nilisema
Kisha nikashauri
Kwa sisi waelewa hakuna ajabu yoyote!, huwezi kuukata mkono unaokulisha au kulikata tawi la mti ulioukalia!.
Huu ni ushauri mzuri, akina sisi tumeisha ishauri Chadema, ushauri na ushauri. Kwenye CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! niliishauri Chadema ijipange vipi, wapi na nilitoa ushauri kumhusu Mwenyekiti Mbowe
Nikaja kutoa ushauri muhimu sana kwa Chadema Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

Ndipo nikagundua CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe! na kujiridhisha CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! hivyo 2015 ilikula za uso!.

Tulipokuja 2020 hapa naomba nisizungumze kuepuka kitu kinachoitwa stigmata!.

Kuelekea 2025 pia nimeshauri Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Nimeshauri Wapinzani to concentrate on serikali za mitaa, udiwani na ubunge, urais wa 2025 bado ni CCM!, Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!

P
 
..Hapana.
Tuwe tunapiga hatua basi ndugu, bila kusahau Chadema si mtu na huko hamko peke yenu?

Kwamba hujui kuwa Chadema ilipinga hadharani jitihada za kina Mwabukusi kuhusiana na katiba mpya na mauzo ya bandari? Ni mwanzo kuyasikia haya hapa leo?

..Hakuna kiongozi wa Chadema aliyeunga mkono bandari kuuzwa, au mchakato wa katiba kusitishwa au kucheleweshwa.

Sasa Chadema si ingechagua hata kunyamaza tu badala ya kutokea hadharani kupinga harakati za wengine wale? Kulikoni kujitokeza hadharani kufanya ambacho angefanya CCM?

..Na kwa uelewa wangu Chadema wamefanya mikutano mingi na maeneo mengi kuzungumza na wananchi kuhusu hoja hizo.

Tatizo si kuwa Chadema Imefanya mikutano au kuzungumzia haya mambo.

Labda kama unasema mikutano ilikuwa imeshatosha na mwingine iikuwa asifanye tena?

..Kwanini tunawakatisha tamaa? Kwanini tunawalaumu? Kwanini tunawazodoa? Tunafanya hivyo kwa faida ya nani?

Huoni kuwa tunaitisha reconciliation? Tumemtaja hata mediator tokea Chadema. Au labda nyie mnataka nini?

Kwanini suluhu kwenu ni kuwakatisha tamaa, kuzodoa au kulaumu.
 
Ngombe wewe Mbowe anafungwa magereza miezi 8 kuna kima aliandamana ili Mbowe achiwe?
 

..Ndugu Chadema hawajawapinga kina Mwabukusi.

..Nionyeshe ni wapi Chadema wamesema Mwabukusi asidai Katiba, au asipinge bandari kuuzwa.

..Naona kama mnaibua ugomvi ambao haupo, halafu mnapendekeza msuluhishi.

..Sasa huo usuluhishi sio kupoteza muda wa kwenda kwa wananchi na kuwatia hamasa?

..Kwanini unataka Mwabukusi na wanaharakati wapoteze muda kuzungumza na Chadema, badala ya kukutana na wananchi na kupanga nao mikakati ya ku'deal na Ccm?
 
Kuwategemea Wanasiasa kuleta mabadiliko, ni kupoteza wakati tu, wanapigana vijembe majukwaani, jioni wanakuwa wote wakigonga cheers!
 
Mbowe kwenye mkutano wa Juzi na wazee alishindwa kujenga HOJA zenye mashiko.

Akumbushwe CDM inapata support na wananchi pia wasio na vyama vya siasa.
Njia halali ya kisheria ya kuwania madaraka ya uongozi wa nchi, ni kuanzisha na kuendesha chama cha siasa! Hiyo ya akina Mbambukusi ni uhuni na vurugu! Kama kweli wanania ya kuikomboa nchi, hakuna short cut, wajiunge na vyama vya siasa!
 

Nililazimika kukwambia tuwe tunapiga hatua. Andiko lako ni kama umefika duniani sasa tokea sayari nyingine.

Kwa andiko lako hujui kuna mtafaruku, kuwa hakuna hata usuluhishi unaohitajika.

"Kwamba unadhani kumbe wanaoandika hawa ni wendawazimu."

Sawa endeleeni kukaza shingo ila hoja haipigwi rungu.

Wapi umeona Mwabukusi na wanaharakati wanataka kuongea na chadema ambayo hata tumekubaliana si mtu, ya mtu na hayupo mwenye hati miliki peke yake humo?

Haya si ni maajabu yenyewe ya Mussa?
 
Njia halali ya kisheria ya kuwania madaraka ya uongozi wa nchi, ni kuanzisha na kuendesha chama cha siasa! Hiyo ya akina Mbambukusi ni uhuni na vurugu! Kama kweli wanania ya kuikomboa nchi, hakuna short cut, wajiunge na vyama vya siasa!

Ushauri kama wako unatolewa na CCM, kina bi tozo na kina Tulia huko.

Wewe ni mwenzao?
 
Opportunity....

Fursa....

Dunia ya fursa....

Tutadanganyana hadi lini ?!!![emoji1787][emoji1787]

Komredi Mbowe ni yuleyule....

Dr.Slaa ni yuleyule....

Uchizi wa Mdude ni uleule [emoji23][emoji23]

#Siempre SSH[emoji7][emoji7][emoji2956]
 
Mleta mada ungekuwa mkweli kwako mwenyewe (honest to yourself) usingeandika bandiko hili. Umeibua mambo kadhaa kuthibitisha kuwa Mbowe na CHADEMA “yake” hawana nia ya dhati ya kupambania katiba na ajenda zingine muhimu za wananchi; kwamba hawataki kumuudhi Rais na serikali yake kwa matarajio ya kutobanwa uchaguzi mkuu wa 2025 na hivyo kuambulia viti kadhaa vya ubunge. Kwamba wanapuuza vyama vingine vya upinzani na wanaharakati. Kwamba wanakwamisha juhudi za wananchi kuibana CCM; n.k.

Umeunga mkono wanaodai CHADEMA ni mali binafsi ya Mbowe na kwamba yeye na chama chake si wapinzani wa kweli bali wasaka fursa, vyeo na ruzuku; n.k.!

Honestly speaking, kwa fikra za aina hiyo, unapomlalamikia Mbowe kwa kutounganisha nguvu na wengine kuibana serikali kwenye suala katiba, bandari, n.k. inakuwa vigumu sana ukaeleweka. Huwezi kumtoa thamani mtu na chama chake kiasi hicho halafu ukategemea afanye mambo ya maana kama hayo unayolalamikia. HALAFU, si Mbowe wala CHADEMA wenye MONOPOLY ya upinzani Tanzania. Ni nani basi huyo anayewazuia nyinyi wapinzani na wanaharakati makini kuongoza hayo mapambano dhidi ya CCM na serikali yake? Ni Mbowe? Ni CHADEMA?

Hili bandiko haliko honest kabisa. Neither is it just and fair to Mbowe and CHADEMA.
 
Njia halali ya kisheria ya kuwania madaraka ya uongozi wa nchi, ni kuanzisha na kuendesha chama cha siasa! Hiyo ya akina Mbambukusi ni uhuni na vurugu! Kama kweli wanania ya kuikomboa nchi, hakuna short cut, wajiunge na vyama vya siasa!
Usichokijua ni kuwa watu hao wanaomsaport Mdude, Mwabukusi na Slaa ndo wanaisapot CDM.

Suluhu ni kuungana, Si kuanzisha chama kipya.

Chama kipya kitapunguza nguvu ya UMOJA wa watz na nguvu ya CDM kama main opposition party.

Kila kundi likianziaha chama chake Bado adui hatowezekanika ndo sababu ya Slaa kuomba support ya CDM.

Narudia HOJA za Mbowe hazikuwa na mashiko.
 

Wakikuelewa usiache kutuletea mrejesho. Haijulikani wanataka au hawataki nini na wala kuwa wanamsemea nani.
 
Ni maoni na mawazo yako, binafsi nayaheshimu...

Lakini bado, hii siyo hoja ya kuitumia kuilaumu CHADEMA na Freeman Mbowe kama ndiyo kikwazo cha wengine kuliamsha kwa namna yao na kwa njia zozote zile halali...

Mtu kama Dr Wlbroad Slaa anatoa wapi political moral authority ya kutoa maagizo kwa taasisi kubwa kama CHADEMA huku historia ya siasa za usaliti dhidi ya wenzake haohao ikimsuta?

Na wakati huohuo ukumbuke kuwa, siasa za ki - Afrika zikiwemo za kwetu Tanzania ni za utata sana na kubebwa na watu watata sana kama huyu Dr Wlbroad Slaa..

Anaweza kujitokeza mtu na kujifanya ni mwanaharakati na mpambanaji mpigania haki mwenzenu na akaonekana hivyo kwa macho ya damu na nyama, lakini kumbe ni kibaraka na ni mkono wa walewale mnaopambana ulingoni...!

Nina maana kuwa, ktk kila hatua ya maamuzi ya kisiasa ndani ya taasisi makini kama CHADEMA, umakini ni wa lazima sana kuepuka kujikuta mmejitia kitanzi wenyewe kwa uamuzi wa kipupa...

Ilisemwa zamani kuwa si vyote ving'aavyo ni dhahabu na wahenga wengine walisema; it's better late than never..."

Freeman Mbowe na CHADEMA wako sahihi na kwa kweli ni mjinga pekee anayeweza kuwalaumu CHADEMA kwa kukataa kupewa maagizo na amri na watu kama kina Dr Slaa ambaye moral authority yake kisiasa ina mashaka makubwa..!

However, bado hakuna kilichoharibika. Muda bado upo. Warudi kwenye drawing board na waweke mikakati ya pamoja...

By the way, mtu kama Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyangali mbona ni wanachama active wa CHADEMA!
..!!

Inakuwaje wanatumia jukwaa jingine kusukuma ajenda zao hizo nje ya utaratibu wa kichama na mwisho wa siku wanarudi tena chamani na kuanza kukilaumu kuwa hawaungi mkono mambo yao? Mbona kama haiingii akilini vile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…