Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea

Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea

Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freemani Mbowe na wenzake 3 wataanza kujitetea Machi 4, 2022 katika kesi ya ugaidi inayowakabili baada ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuwakuta na kesi ya kujibu.
Tujiandae kisaikolojia. FAM leo hawezi kuwa huru. Watesi wake bado hawajapata wanachokitaka toka kwake. Wanataka FAM awaombe msamaha kama mbinu ya kumuua kisiasa. Jaji tayari ana hukumu yake mfukoni na maelekezo mezani kwake.
Tujiandae kwa utetezi.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freemani Mbowe na wenzake 3 wataanza kujitetea Machi 4, 2022 katika kesi ya ugaidi inayowakabili baada ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuwakuta na kesi ya kujibu.
Asanteni sana wakuu mliojitoa kutuhabarisha toka kesi hii imeanza Nyendo , The Sheriff , Suley2019 na wengine.

Hii kesi ikiisha leo tutamshukuru sana Mungu, Mheshimiwa Mbowe na Makomandoo waungane na Familia zao, mapambana ya kudai katiba Mpya yaendelee
 
Niko kama wewe nimejiuliza sana kuhusu huyu mtu, speed yake katika typing ni hatari.
Alikuwa na simu ya kurekodi kinachozungumzwa na hii nyingine ametumia kuchapa maneno kwa ku-play ile aliyerekodi. Ndivyo inavyokuwa, kwa hiyo hakuna muujiza hapo, hata darasa la saba angeweza kuchapa bila kukosea!
 
Nolle proseque maana yake jamhuri haina nia ya kuendelea na mashtaka (kwa sasa)?

Baadae Jamhuri ikipenda inayarejesha mashtaka hayo mahakamani kivingine.

Anachofanyiwa Mbowe ni kuchimbiwa kaburi la kisiasa
 
Watu wengi wamepanic ila kwa kesi hii ambayo ni ya ugaidi na uhujumu uchumi ,ukizingatia na uzito wake isingekua rahisi kwa jaji kuitupilia mbali.
Japokua itakost maisha ya watu gerezani lakini mwaka huu kila kitu kitafunuliwa .
Tutegemee kuona maajabu na uozo wa huu mchongo ulivyo.
Kuna baadhi ya viongoz watawajibishwa kwa hili ,kichama na kiserikali
IGP jiandaye ni shaid mmojawapo 'sabaya naye ajiandaye na kingai naye ngoma ngumu kwenu
Wengi mmemcheka kibatala kwa baadhi ya maswali aliyoyauliza kwamba mengi yalikua hayahusiani na hii kesi ila mtashuhudia majibu yake kipindi cha pili.
Kipindi cha kwanza serikali imeogea mvua ya magoli 'sasa hivi kipindi cha pili wanataka majina ya mashahidi 'hahaaaa watanzania tuwe na subra mema yanaijia tanzania
Yeah mkuu
 
Mahakama iko sahihi kuna kesi ya kujibu kama hao makomandoo waliajiriwa kama walinzi wa mbowe au Lisu je taratibu za ajira zikizingatiwa? Wakkatwa Kofi ya mapato ya TRA na NSSF kipindi chote cha hiyo ajira yao iwe ya siku moja au wiki au nk sababu ukiajiri kibarua hata kwa Siku moja lazima ukate TRA na NSSF

Hao makomandoo waliajiriwa kwa mkataba UPI? It appears waliitwa kwa ajira IPI hiyo isiyotambuliwa sheria za ajira,NSSF na TRA? Kama siio ugaidi
Serikali enyewe haikatagi PAYE au NSSF kwa casuals leo Mbowe ndo alazimike kulipa PAYE casuals wake? Wewe mbona hujawahi kupeleka PAYE au NSSF ya housegirl wako?
 
Justice was not served. Huyo jaji ni pussy ass. Hope he gets to meet an early death for such a plain and gross injustice.
 
Once a soldier u die a soldier! Wale wana viapo na wengi bado wanatumika na dola. Hapo Mbowe alijichanganya. Wengi wastaafu wanakua kama wapelelezi. Kupata wataoside na wewe in 100% ni ngumu mno.

Binafsi huwa sijawahi kuwaamini maaskari au wastaafu...wote wanoko tu!
Tuna solder huku mtaani wastaafu wapo kwenye kazi za ulinzi hata kwenye sheria za kuanzisha kampuni ya ulinzi moja ya sharti la kugungua lazima one of director awe ameshapitia vyombo vya ulinzi na usalama
 
Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba anayesikiliza hii kesi anaitwa jaji lakini siyo jaji. Huyu ni miongoni mwa maafisa qa TISS walioingizwa na marehemu kwenye mahakama.

Hakuna chochote atakachoamua kilicho kinyume na maelekezo ya ikulu. Anachofanya, tujue ndicho walichokubaliana kufanya.

Ikulu imeshtaki, ikulu inatoa ushahidi, ikulu ndiyo inayoamua. Mawakili wa utetezi endeleeni kufanya kazi ili kudhihirisha uovu wa ikulu, lakini siyo kutarajia huyu jaji eti atoe hukumu kwa kutegemea hoja zenu.
 
Heshimuni madalaka ya dunia.Mbowe sio gaidi ila hakueshimu mamlaka ya dunia apo tu ndo alialibu na itamtesa sana
 
Once a soldier u die a soldier! Wale wana viapo na wengi bado wanatumika na dola. Hapo Mbowe alijichanganya. Wengi wastaafu wanakua kama wapelelezi. Kupata wataoside na wewe in 100% ni ngumu mno.

Binafsi huwa sijawahi kuwaamini maaskari au wastaafu...wote wanoko tu!
kuna yule mmoja nafikiri ni Likwenya baada ya kufukuzwa jeshini kwa utovu wa nidhamu yeye aliamua kwenda kujishughulisha na upasuaji wa kokoto,na yeye anasema barua ya kuondolewa jeshini anayo,je angeishiji mtaani ama wao wanatakiwa waishi kwa kujikimu vipi
 
Vipi maombi yako yamesikilizwa au?,[emoji23][emoji23][emoji23] Shukrani zimwendee jaji anayesimamia kesi hii,Kama yumo humu naomba aje PM yangu nimpe ya bia[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani amesha wafunga au wanatakiwa kujibu kesi, kujitetea?!
 
Kama sio kamanda urio ambae ni kamanda wa jeshi.
Mbowe angekuwa na KESI GANI YA KUJIBU!?
Kwa maoni yako na kwa mujubu wa mwenendo wa kesi umeona kuna mahala pametajwa kwamba Mbowe anashtakiwa kwa kushirikiana na wanajeshi??
 
Back
Top Bottom