Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

Mgombea ubunge wa jimbo la Hai ambaye ni mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Tundu Lisu atakuwa Rais wa Tanzania na Mungu akipenda yeye ( Mbowe ) atakuwa Waziri mkuu.

Source Jamii Forums

My take; Zitto Kabwe mbona mnamsahau mapema hivi!

Maendeleo hayana vyama!
 
Acha kufarakanisha
 
Habari ya Tundu kuapishwa kuwa raisi ubalozini huko nga'mbo ni za kweli au ni maluelue ya vijana wake?!!
 
Hata mimi kuna jamaa yangu alikuwepo kwenye semina na walielekezwa wafuate sheria na taratibu za uchaguzi. Hivyo ndivyo walivyoambiwa na kila mtu amuamini jamaa yake.
 
Ulibadili hadi gear angani na vyama vikaungana ila haukuwa waziri,kwahiyo utaka kuniambia kula hazikutosha wakati huo?
 
Pesa kidogo tu anajitangaza kuwa PM.
 
Usipanic ndugu yangu wajinga Kama hao unawaangalia walivyochanga yikiwa unawaacha
Acha magu achukue nchi aendelww kuwanyoosha
Wameshaona wameshindwa wanaanza kutunga uongo wakifikiri uongo utawaokoa
 
Yani nasikia kwenye mafunzo ya wasimamizi huko,wasimamizi wakuu wanafundishwa namna ya kuukandamiza upinzani na kuhakikisha jiwe anapita kwa kura nyingiiii
Ulitaka lisu ashinde!!?
Mmefele mbaya
List mwenyewe anajua hashindu ndio maana anaticket ya ndege mfukon
Tar 29 anatimka
 
Duh huyu mwamba sijui huwa anarukwa akili? Inamaana hajui hata mchakato wa kumpitisha waziri mkuu ukoje? Achilia mbali kibaraka wa wazungu lissu kushinda urais,elimu ni muhimu sana kwa viongozi wa CHADEMA maana kama mwenyekiti anaongea upuuzi huu si ni hatari sana
 
Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.
Hii kauli inazidi kumnyima kura Lissu! Hatuwezi kumchagua Rais anayepangiwa nini cha kufanya hasa kwenye majukumu mazito! Kumpata waziri Mkuu ni jukumu zito!

Na katika hili, imedhihirisha kuwa CHADEMA ni wabinafsi kama nilivyowahi kueleza. Wanawaza vyeo badala ya kuwaza ni namna gani Tanzania itaimarishwa kiuchumi na kijamii kwa uendelevu! CHADEMA wanaanza kugawana vyeo hata kabla ya uchaguzi kufanyika hii inaleta picha kuwa kuna uwezekano mkubwa hawa jamaa watatuuza watanzania ama kwa mafungu ama kwa jumla huko kwa wabaya wetu! Mwenyekiti wa chama ni kielelezo cha uimara na nia ya chama hicho kupitia taratibu za chama hicho! Mbowe ameonyesha nia ya chadema.

Shime watanzania! Tuwakate wawakilishi wa CHADEMA kuanzia udiwani mpaka urais kwa sababu chama hicho kimeonyesha nia ya ubinafsi uliopitiliza kupitia viongozi wao! Hawa hawatatujali sisi watanzania!

Nina imani na watanzania, kwa sababu tunaenda kuonyesha nia ya dhati ya kuilinda nchi yetu Tanzania kwa kutowapigia kura Chadema na vyama vingine vyenye mlengo wa Chadema.

Mungu ibariki Afrika na watu wake; Mungu ibariki Tanzania, Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…