Pre GE2025 Mbowe: Nimetoka mbali na Lissu, nilikuwa namlipia tiketi za ndege kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji madini

Pre GE2025 Mbowe: Nimetoka mbali na Lissu, nilikuwa namlipia tiketi za ndege kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji madini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimemsikiliza Mbowe ktk part 2 ya mahojiano na Kikee , ameongea mengi sana.
Jinsi alivyomsaidia Lissu ktk siasa
Lilinifurahisha zaidi kwamba uchaguzi live kwa kila kura itayopigwa itaonyeshwa live kapigiwa nani. Inaamaana TV zote mpaka za ubelgiji zitakuwepo ukumbini kuonesha kura hii kapigiwa nani na hii kapigiwa nani.
Hii ndio itayomuabisha lissu ktk uchaguzi na ashindwe kuamini, maana swala la kuibiwa kura kwake litakua halipo. Ataanguka vibaya sana
Namshauri Lissu ajitoe kinyang'anyiro hichi
Kwa hiyo alimsaidia Lissu kwa makubaliano ya aina gani?
 
Ukimpa mtu msaada usiutumie kama silaha ya kumuadhibu pale anapokuwa na mtizamo tofauti na wako.
Kabisa mkuu hata kama ulimsaidia mtu katika mdomo wa mauti huna guarantee ya kumwua Kwa kudai kuwa bila wewe angeshakufa/angeshakufa
 
Mbowe anapiga mikwara ya Asha Ngedere tu!!

Mbowe mwenyewe lazima ampigie kura Lissu!!!
 
Nimemsikiliza Mh. Mbowe kwa umakini na baadae nikagundua mambo kadha.

Amefanya mengi sana kwa Lissu as the brother, na alitegemea kwamba hata katika haya, hata katika tofauti hizi basi Lissu angemfichia Mbowe madhaifu yake.
 
Kwenye mahojiano na Kikeke.

View: https://www.youtube.com/watch?v=O6OAQjXmaXQ

Wapi hapa Mbowe kasema Lissu atachukuliwa hatua baada ya uchaguzi? Alichosema ni kuwa tatizo kubwa ndani ya Chadema ni ukosefu wa nidhamu. Ndio maana akasema uongozi utakaoingia itabidi uchukue hatua za kudhibiti hii hali bila kujali nafasi ya mhusika. Amesema hata kama yeye atashinda, Kamati Kuu mpya itakuwa na mamlaka ya kumchulia hatua kama itaona kuwa amehusika katika huo utovu wa nidhamu. Alipoulizwa kama atamchukulia hatua Lissu, alijibu kuwa huo utakuwa ni uamuzi wa Kamati Kuu na sio wa kwake. Hakusema mahali popote kuwa Lissu atachukuliwa hatua kwa sababu amemtukana. Huo ni uongo mtupu.

Amandla...
 
Lissu na Heche na wananchi wengine wameweka nchi mbele zaidi ya matakwa yao binafsi. Mbowe bado anafikiri kugombea kwao ni kwasababu yake wenyewe wanafikiri ni kwasababu ya kusaidia taifa. Mbowe inabidi atoke kwenye kufikiri kibinafsi. Lengo hapa ni taifa na wenyewe wanafikiri wanaweza kuamsha watu wote kwa manufaa ya nchi. Mbowe bado hajajibu swali ni kitu gani tofauti atafanya tofauti
Kwani mbowe ana sera? Mbowe Hana lengo la dhati la kuitoa ccm madarakani
 
..hapana.

..uchaguzi wa Chadema kushuhudiwa na viongozi wa Dini, na Mabalozi, ni kuionyesha DUNIA jinsi uchaguzi huo ulivyo safi, huru, na wa kuaminika.

..utakuwa fundisho hata kwa nchi nyingine marafiki, na hata taasisi za kidini.

Mbowe amelijibu. Amesema Lissu kama mwanasheria anajua au anapaswa kujua Vienna Protocol inapiga marfuk mabalozi kujihusisha na siasa za ndani.

Kasema watakachofanya ni kuruhusu kwa mara ya kwanza waandishi na camera kwenye ukumbi, kinyume na kanuni za uchaguzi za chama. Kamati Kuu itapitisha kwa madhumuni mapana.

Hatuhitaji foreign agents to monitor our elections. Huwezi hata kujisimamia uchaguzi wa chama cha upinzani we Mwafrika. Utaweza nini, mchango wako ni nini hapa duniani, kuchonga vinyago vya mpapule ?

We good. We got it.

Foreign agent yeyote atakaekuja kwenye ukumbi wa uchaguzi atapokelewa na tangazo la GTFO
 
..Mabalozi wamekuwa wakialikwa ktk matukio mbalimbali ya vyama vya siasa na wakati mwingine wamefadhili matukio hayo.

..Chombo kama TCD kimekuwa kikipokea fedha za ufadhili toka katika balozi mbalimbali hapa nchini.

..Hakuna mkataba wowote ule wa Kidiplomasia utakaokuwa umevunjwa ikiwa wawakilishi wa nchi marafiki wataalikwa kuwa waangalizi wa uchaguzi wa Chadema.
 
Back
Top Bottom