Mbowe: Rais Samia haaminiki, aweke hadharani mkataba wa bandari ili tuuone

Nime screenshot comment yako Kwa kumbukumbu. Asante Kwa maoni Bora Sana.
 
Rais Samia asifikiri kumweka Makonda kwenye nafasi hiyo ndio nafuu kwake, hapa, anajidanganya, tena huyo Makonda tuna kazi naye atakapokuja mtaani kwetu, lapili kama mkataba wa DP World umebeba maoni kweli ya wananchi atakuwa salama, kama kafanya janja janja hawezi kubaki salama kisiasa, sababu watu walifanya dua mbalimbali Na kwa makundi mbalimbali, tuone mwisho wake
 
Dua

La Kuku halimpati mwewe ujue
 
Kwa hiyo tumeachana na maandamano ya kina Mzee Slaa tunahamia kwny maombi?
 
We umewahi kushinda kesi gani?
 
Wewe ni mkongwe JF. Jaribu kubalance hisia hasa unapowaongelea viongozi wategemewa na wananchi.
 
Si mmesema imeshasainiwa,Sasa Ina maana gani kuwekwa public?
 
Nchi yetu imejaa wajinga wengi sana kiasi kwamba wale wenye akili wanaonekana ndio wajinga na wajinga wanawekwa kundi la werevu.

Huo ni mkataba wa biashara hauwezi kuanikwa hadharani tu, humo kuna siri za DP World na serikali ya Tanzania.

Na kina Mbowe wenye kufanya biashara kubwa kubwa kwa muda mrefu ni lazima haya mambo wanayafahamu, hapo wanapiga siasa kwa wananchi wanaowasikiliza. Kwa maneno mengine kwa Mbowe siku imeshaingiza pesa tayari, haijapita bure tu.
 
Kama Mbowe alidiriki kuchukua pesa mwaka 2015 kama unavyodai huoni maoni yako yanadharilisha mifumo yetu inayosimamia utawala bora hasa Takukuru ambayo walikuwa na wajibu wa kumkamata Mbowe kupokea rushwa au kuviolate sheria ya uchaguzi?Hizo allegation zisizo na kichwa wala miguu mtaziacha lini?

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
IGA iko vilevile.
Kitanzi kipo palepale
Samia akishaondoka
Majaliwa akishaondoka
Mpango akishaondoka
IGA IKO VILEVILE!
IGA bila ya kuziondoa zile sheria walizoanza kuzifanyia kazi na kupeleka mswada Bungeni, na baadae kuondoa kwa aibu; hiyo IGA haina nguvu.

Ninachokubaliana nawe ni kuwa, sasa hiyo IGA ipo 'mortuary'.
Na kwa bahati mbaya sana, waTanzania wasipostuka na kumpa Samia ngwe yake hapo 2025; hiyo IGA itafufuka, tena na kuwa jini la kutisha sana.
 
Tarehe 22 Oktoba, 2023 Mhe. Rais alitoa Hotuba mbele ya wageni waalikwa wakati wa kusaini Mkataba wa Uwekezaji wa Bandari kati ya TPA na DP World. Kama kweli yale maneno ya Mhe. Rais yatatekelezwa basi sisi Wananchi tunaona kuwa Bandari inaweza kuchangia kwa asilimia 50 ya Bajeti ya klla mwaka ya nchi yetu. Sisi wananchi tunaitaka Serikali iweke huo Mkataba WAZI kupitia magazeti, tovuti ya Serikali na Tovuti ya Bunge ili tupitie mstari kwa mstari. Ieleweke sisi ndiyo wenye nchi na hata Mhe. Rais yuko pale kwa ridhaa yetu.
 
Badala ya kupambana na SHUGHULI zetu ili kujikwamua KIUCHUMI, tunakazana kuwasikiliza Akina Mbowe ambao hata njaa HAWANA....maana utawakuta Ikulu wakinywa chai na Mama...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…