Sasa sie watoto wa Jumbe Tambaza tuliogawa ardhi yetu hapo Dar mpaka ikajengwa hiyo iliyo Ikulu leo, tuliojenga misikiti na kutoa ardhi yetu makaburi watu wazikwe, lakini kwa sababu ya maadili ya kifamilia hatujaenda hizo Disco na sie si watoto wa mjini?
Sie wajukuu wa Pazi Chamgui, wazee wetu waliojenga hilo kanisa la Azania Front na kulimaliza mwaka 1903, ambalo Mbowe kalikuta na kasali tu bila kujua nani kajenga, lakini hatukuenda disco kwa sababu ya maadili ya familia, utasema na sisi si watoto wa mjini?